Mbunge wa Viti maalumu mkoa wa Tanga Mhe. Mwamtumu Mzami Mzodo ameiomba Wizara ya Tamisemi kuwapatia elimu watendaji kata kupitia vyuo vya ufundi na kuwanunulia vifaa vya usafili madiwani
Mh Mzodo ameyasema hayo leo Bungeni Jijini Dodoma ambapo amesema watendaji kata na madiwani wanafanya kazi kubwa kupita hata wabunge maana wao wapo kalibu sana na wananchi wanajua shida za wananchi na vitu vingi kuhusu wananchi
Mh Mbunge amesema madiwani wapewe vifaa vya usafiri kwaajili ya kulahisisha kazi ili kazi iendelee kwa uhalaka na watendaji kupata elimu kwasababu kazi walionayo ni kubwa kupita hata wabunge
“Madiwani na watendaji Kata wanafanya kazi kubwa kupita hata wabunge kwa sababu wapo karibu sana na wananchi na mwananchi na anamwangalia sana mtendaji kupita hata Mkurugenzi kwahiyo naiomba wizara ya tamisemi itoe hela kwaajili ya watendaji kupata elimu kwani ni muhimu sana”
Amesema Tofauti iliyopo kati ya wabunge na madiwani wabunge wanaingia Bungeni na madiwani wanabaki kwanye Halmashauri zao ila kazi wanayoifanya ni zaidi ya wabunge.