Mheshimiwa Spika, Nachukua fursa hii kwa kumshukuru Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutoa idhini ya ajira za watumishi wa Sekta ya Elimu na Afya 17,412 ambapo nafasi 9,800 ni za walimu na 7,612 ni za kada za afya ambao wataajiriwa katika mwaka huu wa Fedha 2021/22. Naomba kutoa taarifa rasmi kuwa Watanzania wenye sifa wanaelekezwa kuanza kuomba kuanzia leo. Aidha, napenda kuwaelekeza kuwa maombi ya ajira hizi ni bure na yanafanyika kupitia mfumo wa kielektroniki ambao maelekezo yake yatakuwa katika tangazo la ajira. Asilimia tatu (3%) ya ajira hizo ni kuajiri Watu wenye Ulemavu kulingana na Sheria. Aidha, naelekeza Wakurugenzi wote wa Halmashauri kuhakikisha wanawanunulia watu wenye ulemavu wa Ngozi (Albino)
