Mbunge wa jimbo la Tabora Kaskasini Mhe. Athuman Ayomas Maige ameiomba serikali ifanye utafiti mahususi kuhusu lugha ya kufundishia mashuleni itumike lugha ya Taifa Kiswahili na sio lugha ya nchi nyingine.
Mhe. Maige ameyasema hayo Bungeni jijini Dodoma ambapo ameiomba serikali ifanye utafiti wa Kiswahili kutumika katika kufundishia masomo yote na sio kiingeleza ambayo sio lugha yao watanzania.
Amesema hakuna kokote Duniani ambako watu wameendelea kwa sababu wanatumia lugha ya kwinginehivyo ameiomba serikali kuanzisha sera ya lugha ya kufundishia iwe Kiswahili.
“Waingereza wanatumia kiingeleza ,wafaransa wanatumia kifaransa,wachina wanatumia kichina wajerumani kijerumani,wahindi wanatumia kihindi lakini watanzania tunatumia lugha yakufundishia kiingeleza wakiwa wanasema Kiswahili kuanzia darasa la kwanza hadi la saba kuendelea sekondari kiingeleza nusu ya elimu nusu ya elimu yao wanajifunza lugha na sio elimu”
Naishauri Serikali ifanye tena utafiti, zipo tafiti Zaidi ya Arobaini kwa miaka 46 zote zinasema lugha inayofaa kufundishia Tanzania ni Kiswahili, naiomba serikali ifanyer utafiti mahususi kwaajili ya lugha ya kufundishia iwe Kiswahili itumie kanuni za kawaida za Bunge za mwaka 2020/2025.