WATOTO ZAIDI YA ELFU TATU WALIO KATIKA MAZINGIRA HATARISHI WAPEWA MAFUNZO


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamismi Mhe. Inncocent Bashungwa amesema watoto 3,605 walio kwenye mazingira hatarishi katika Halmashauri 81 walipewa mafunzo ya ufundi kupitia Vyuo vya Ufundi Stadi (VETA) na kupewa vifaa vya kuanzia kazi vyenye thamani ya Shilingi bilioni 15.6. Vilevile, watoto 117,513 wanaoishi katika mazingira hatarishi kwenye kaya 40,487 katika Halmashauri 71 wamepewa Kadi za Mfuko wa Afya ya Jamii iliyoboreshwa (iCHF) zenye thamani ya Shilingi bilioni 1.71.
Aidha Bashungwa aliongeza, kuwa mwaka 2022 mfumo wa usajili na utoaji wa vyeti vya kuzaliwa bila malipo kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano uliozinduliwa katika Mikoa ya Arusha na Manyara umefanyika ambapo jumla ya watoto 634,222 ambao wamesajiliwa.
“Mpango huu unatarajia kuendelea katika mikoa yote. Aidha, jumla ya Watu Wenye Ulemavu 124,900 wametambuliwa ambapo wanawake ni 59,059 na Wanaume 65,841. Kati ya hao wanufaika 15,596 wamepatiwa huduma mbalimbali zenye thamani ya Shilingi bilioni 1.30 zikiwemo vifaa saidizi, huduma za utengamao na matibabu.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *