Waziri wa TAMISEMI, Innocent Bashungwa amewasilisha Bungeni makadirio ya mapato na matumizi ya mwaka wa fedha 2022/2023 ambapo amesema katika kuendelea kuboresha huduma ya usafiri mkoa wa DSM, DART itaendelea kuongeza Mtandao wa Miundombinu ya Mabasi ya Mwendokasi, kwa kuendelea na ujenzi wa miundombinu ya BRT katika maeneo mbalimbali ikiwemo Kigamboni na Tabata.
Bashungwa amesema awamu ya pili itajumuisha barabara za Kilwa, Barabara ya Chang’ombe, barabara ya Kawawa, Mtaa wa Gerezani na Sokoine Drive na awamu 3 itajumuisha barabara za Nyerere hadi Gongo la Mboto; barabara ya Mandela, barabara ya Uhuru kutoka Makutano ya Barabara ya Mandela; Mtaa wa Shaurimoyo, Mtaa wa Lindi, Nkurumah, Mtaa wa Maktaba na Mtaa wa Azikiwe hadi makutano na barabara ya Kivukoni.
Kwa upande mwingine alisema, “TAMISEMI imeomba kibali cha kuajiri Walimu wapya Elfu 10.”
