NEEMA YAJA OFISI ZA WAKUU WA WILAYA. MIKOA YAONGEZEWA FEDHA KUIMARISHA USALAMA

Ofisi za Wakuu wa Wilaya zimeongezewa fedha za matumizi mengineyo kutoka Shilingi bilioni 17.13 hadi Shilingi bilioni 26.68 sawa na ongezeko la Shilingi bilioni 9.55 ambalo ni ongezeko la asilimia 55.75 kwa ajili ya kuwawezesha kusimamia usalama na utekelezaji wa shughuli za Serikali katika maeneo yao.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tamisemi. Mhe Innocent Bashungwa Bungeni Jijini Dodoma wakati akiwasilisha Bajeti ya makadirio ya Mapato na Matumizi Ofisi ya Rais Tamisemi kwa Mwaka wa Fedha 2022/ 2023
Aidha alisema, Mikoa imeongezewa fedha za uendeshaji wa vikao vya Kamati za Usalama vya mikoa kutoka Shilingi milioni 416.00 hadi Shilingi milioni 780.00 sawa na ongezeko la Shilingi milioni 364.00;

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *