HOTUBA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS – TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA, MHESHIMIWA INNOCENT LUGHA BASHUNGWA (MB.), AKIWASILISHA BUNGENI MAKADIRIO YA MAPATO
NA MATUMIZI KWA MWAKA
WA FEDHA 2022/23
- UTANGULIZI
- Mheshimiwa Spika, awali ya yote napenda kuchukua fursa hii kumshukuru Mwenyezi Mungu, mwingi wa rehema, kwa kunijalia afya njema na kuniwezesha kusimama mbele ya Bunge lako Tukufu.
- Mheshimiwa Spika, kufuatia taarifa iliyowasilishwa leo ndani ya Bunge lako Tukufu na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa, naomba kutoa hoja kwamba Bunge lako Tukufu sasa likubali kupokea na kujadili, Taarifa ya Utekelezaji wa Mpango na Bajeti ya Ofisi ya Rais – TAMISEMI (Fungu 56), Tume ya Utumishi wa Walimu (Fungu Na. 2) na Mafungu 26 ya Mikoa ikijumuisha Halmashauri (184) kwa Mwaka wa Fedha 2021/22. Aidha, naomba Bunge lako Tukufu lijadili na kupitisha Mpango na Bajeti ya Ofisi ya Rais – TAMISEMI (Fungu 56), Tume ya Utumishi wa Walimu Fungu (Na. 2) na Mafungu 26 ya Mikoa ikijumuisha Halmashauri (184) kwa Mwaka wa Fedha 2022/23.
- Mheshimiwa Spika, kwa heshima na unyenyekevu mkubwa ninampongeza Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa jitihada zake za kuwezesha upatikanaji wa fedha kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule za sekondari na vituo shikizi, fedha hizi zimewezesha kupunguza msongamano wa wanafunzi madarasani. Aidha, jitihada hizo zimewezesha pia upatikanaji wa fedha kwa ajili ya ujenzi wa mabweni kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum katika shule za msingi, ujenzi wa majengo ya wagonjwa mahututi, majengo ya kutolea huduma za dharura, nyumba za watumishi katika sekta ya afya, mashine za mionzi, mitambo ya kuzalisha hewa ya Oksijeni, kituo cha matibabu cha magonjwa ya kuambukiza na ununuzi wa magari ya kubeba wagonjwa kwa kila Halmashauri na magari ya usimamizi katika ngazi ya Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Mikoa na Halmashauri.
- Mheshimiwa Spika, natoa pole kwako, Naibu Spika na Waheshimiwa Wabunge wa Bunge lako Tukufu kwa kuondokewa na wapendwa wetu Mheshimiwa Elias Kwandikwa, aliyekuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa na Mbunge wa Jimbo la Ushetu; Mheshimiwa William Tate Olenasha aliyekuwa Naibu Waziri wa Uwekezaji (Ofisi ya Waziri Mkuu) na Mbunge wa Jimbo la Ngorongoro; na Mheshimiwa Khatibu Said Haji aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Konde Zanzibar). Aidha, napenda kutumia fursa hii kutoa pole kwa familia, ndugu, jamaa wa marehemu, marafiki na watanzania wenzangu kwa kuondokewa na wapendwa wao. Mwenyezi Mungu azilaze roho za marehemu wote mahali pema peponi, Amina.
- nitumie fursa hii kukupongeza wewe binafsi, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Naibu Spika Mheshimiwa Hassan Mussa Zungu Mbunge wa Jimbo la Ilala kwa kuchaguliwa kwa kishindo kuongoza Mhimili wa Bunge. Tunakuahidi kukupa ushirikiano katika utekelezaji wa majukumu yako.
- Mheshimiwa Spika, napenda pia kuwapongeza Wenyeviti wa Bunge, Mheshimiwa Najma Murtaza Giga (Mb) na Mheshimiwa David Mwakiposa Kihenzile (Mb) kwa kuendelea kukusaidia katika kutekeleza majukumu ya kuongoza Bunge lako.
- Mheshimiwa Spika, kipekee napenda kuchukua fursa hii kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa kuniamini na kuniteua kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR – TAMISEMI). Ninamshukuru pia kwa kuendelea kuwaamini Mheshimiwa Dkt. Festo John Dugange, Mbunge wa Jimbo la Wanging’ombe na Mheshimiwa David Ernest Silinde, Mbunge wa Jimbo la Tunduma kuwa Naibu Mawaziri Ofisi ya Rais – TAMISEMI na Waheshimiwa Wakuu wa Mikoa wote Tanzania Bara. Aidha, namshukuru Mheshimiwa Rais kuendelea kumuamini Katibu Mkuu, Profesa Riziki Silas Shemdoe, Naibu Makatibu Wakuu; Dkt. Grace Elias Magembe (Afya), Bw. Gerald Geofrey Mweli (Elimu) na kumteua Dkt. Switbert Zacharia Mkama kuwa Naibu Katibu Mkuu (TAMISEMI).
- Mheshimiwa Spika, tunamuahidi Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na watanzania kuwa tutaendelea kufanya kazi kwa bidii, weledi, ubunifu, uaminifu na utiifu kwake, na kwa nchi yetu, katika kumsaidia kusimamia shughuli za utawala na maendeleo katika Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa, hususan kwa kuhakikisha kuwa Mamlaka za Serikali za Mitaa zinaongeza ubunifu kwa kuongeza vyanzo vipya, kuimarisha vyanzo vilivyopo, na mbinu katika ukusanyaji wa Mapato ya Ndani, bila kusababisha kero kwa wananchi. Aidha, Mapato hayo yatumike katika kutekeleza vipaumbele vilivyowekwa, ikijumuisha Miundombinu ya huduma za Afyamsingi na Elimumsingi, barabara, Majengo ya Utawala, Makazi ya Viongozi na watumishi, Ununuzi wa Vifaa, Vifaa Tiba na Vitendanishi, na kuwawezesha wananchi kiuchumi kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Miongozo. Vilevile, tutaongeza jitihada za kusimamia matumizi ya fedha za umma katika Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa.
- Mheshimiwa Spika, kipekee, nampongeza Mheshimiwa Abdallah Jaffari Chaurembo, Mbunge wa Jimbo la Mbagala, kwa kuteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa; Mheshimiwa Denis Lazaro Londo, Mbunge wa Jimbo la Mikumi kuwa Makamu Mwenyekiti wa Kamati, pamoja na Wajumbe wote wa Kamati kwa mchango wao mkubwa, katika kuchambua utekelezaji wa Mpango na Bajeti ya Ofisi ya Rais – TAMISEMI (Fungu 56), Tume ya Utumishi wa Walimu (Fungu Na. 2) na Mafungu 26 ya Mikoa ikijumuisha Halmashauri 184 kwa Mwaka wa Fedha 2021/22. Aidha, Kamati ilijadili kwa kina Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Mafungu yote 28, kwa Mwaka wa Fedha 2022/23 na kupitisha kwa kauli moja. Vilevile, Kamati imekuwa ikitoa ushauri ambao umesaidia kuboresha utendaji wa Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Mikoa, Mamlaka za Serikali za Mitaa, Tume ya Utumishi wa Walimu na Taasisi nyingine zilizo chini ya Ofisi ya Rais – TAMISEMI.
- Mheshimiwa Spika, kwa namna ya pekee naomba niipongeze Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi mahiri wa Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Philip Isidor Mpango Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa kusimamia kikamilifu, kwa dhati na kwa umakini mkubwa utekelezaji wa Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025, Mpango wa Tatu wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2021/22 – 2025/26), Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2020 na Malengo Endelevu ya Maendeleo (2030).
- UTEKELEZAJI WA MPANGO NA BAJETI KWA MWAKA WA FEDHA 2021/22
- Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha 2021/22, Ofisi ya Rais – TAMISEMI na Taasisi zake, Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa iliidhinishiwa kukusanya Maduhuli na Mapato ya Ndani, jumla ya Shilingi bilioni 916.44. Kati ya fedha hizo, Shilingi bilioni 52.36 ni ya Ofisi ya Rais – TAMISEMI na Taasisi zake, Shilingi milioni 220.68 ni Maduhuli ya Mikoa, na Shilingi bilioni 863.85 ni Mapato ya Ndani ya Mamlaka za Serikali za Mitaa. Aidha, hadi Februari 2022 jumla ya Shilingi bilioni 615.61 zimekusanywa, sawa na asilimia 67.17 ya bajeti iliyoidhinishwa.
- Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha 2021/22 Ofisi ya Rais – TAMISEMI (Fungu 56), Tume ya Utumishi wa Walimu (Fungu Na. 2) na Mafungu 26 ya Mikoa ikijumuisha Halmashauri 184 iliidhinishiwa bajeti ya jumla ya Shilingi trilioni 8.56, ambapo Shilingi trilioni 4.72 ni Matumizi ya Kawaida, yakijumuisha Mishahara Shilingi trilioni 3.97, Shilingi bilioni 755.85 kwa ajili ya Matumizi Mengineyo, na Shilingi trilioni 3.84 ni Fedha za Maendeleo (Kiambatisho Na. 1).
- Mheshimiwa Spika, hadi Februari 2022 Mafungu 28 ya Ofisi ya Rais – TAMISEMI, yamekusanya na kupokea kiasi cha Shilingi trilioni 5.33, sawa na asilimia 62.26 (Kiambatisho Na. 1).Mchanganuo kwa kila Fungu ni kama ifuatavyo: –
Ofisi ya Rais – TAMISEMI na Taasisi zilizo chini yake (Fungu 56)
- Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha 2021/22 Ofisi ya Rais – TAMISEMI na Taasisi zilizo chini yake, iliidhinishiwa jumla ya Shilingi trilioni 1.04.Kati ya fedha hizo, Shilingi bilioni 57.51 ni mishahara, ambapo Shilingi bilioni 10.27 ni za Ofisi ya Rais – TAMISEMI Makao Makuu, na Shilingi bilioni 47.23 ni za Taasisi; Shilingi bilioni 11.37 ni zamatumizi mengineyo ambapo Shilingi bilioni 10.05 ni kwa ajili ya Ofisi ya Rais – TAMISEMI Makao Makuu na Shilingi bilioni 1.31 ni za Taasisi. Aidha, Shilingi bilioni 973.82 ni za miradi ya maendeleo ambapo fedha za ndani ni Shilingi bilioni 773.66 na fedha za nje ni Shilingi bilioni 200.15.
- Mheshimiwa Spika, hadi Februari 2022 Ofisi ya Rais – TAMISEMI (Fungu 56) imepokea jumla ya Shilingi bilioni 670.36.Kati ya fedha hizo, Shilingi bilioni 38.17 nikwa ajili ya mishahara, sawa na asilimia 66.38 ya fedha zilizoidhinishwa.Aidha, Shilingi bilioni 8.83 ni matumizi mengineyo, sawa na asilimia 77.66, na Shilingi bilioni 623.35 ni kwa ajili ya miradi ya maendeleo, sawa na asilimia 64.01.Vilevile,Fedha za Maendeleo zinajumuisha Shilingi bilioni 526.13 fedha za ndani na Shilingi bilioni 97.22 fedha za nje. (Kiambatisho Na. 1)
Tume ya Utumishi wa Walimu (Fungu Na.2)
- Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha 2021/22, Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC) iliidhinishiwa jumla ya Shilingi bilioni 14.86, kati ya fedha hizo Shilingi bilioni 7.76 ni kwa ajili ya mishahara, Shilingi bilioni 6.60 nimatumizi mengineyo, na Shilingi milioni 500.00 kwa ajili ya mradi wa maendeleo.
- Mheshimiwa Spika, hadi Februari 2022 Tume ya Utumishi wa Walimu (Fungu Na. 2) imepokea jumla ya Shilingi bilioni 9.51,sawa na asilimia 64.01 ya fedha zilizoidhinishwa.Kati ya fedha hizo, Shilingi bilioni 5.25 ni kwa ajili ya mishahara, sawa na asilimia 67.69, Shilingi bilioni 3.75 matumizi mengineyo sawa na asilimia 56.95, na Shilingi milioni 500.00 nikwa ajili ya ujenzi wa jengo la Ofisi ya Tume Makao Makuu Dododma sawa na asilimia 100 ya fedha zilizoidhinishwa (Kiambatisho Na. 1).
Mafungu 26 ya Mikoa ikijumuisha Halmashauri 184
Tawala za Mikoa
- Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha 2021/22, Mikoa iliidhinishiwa jumla ya Shilingi bilioni 242.84.Kati ya fedha hizo, Shilingi bilioni 71.26 ni mishahara, Shilingi bilioni 57.44 matumizi mengineyo, na Shilingi bilioni 114.12 miradi ya maendeleo ambayo inajumuisha Shilingi bilioni 90.32 fedha zandani, na Shilingi bilioni 23.79 fedha za nje.
- Mheshimiwa Spika, hadi Februari 2022 Mikoa ilipokea jumla ya Shilingi bilioni 173.99,kati ya fedha hizo Shilingi bilioni 45.58 nikwa ajili ya mishahara, sawa na asilimia 64.34, Shilingi bilioni 48.03 matumizi mengineyo, sawa na asilimia 83.62,na Shilingi bilioni 80.37 kwa ajili ya miradi ya maendeleo sawa na asilimia 70.42, ambapo fedha za ndani ni Shilingi bilioni 71.41 na fedha za nje ni Shilingi bilioni 8.95 (Kiambatisho Na. 1).
Halmashauri 184
- Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha 2021/22, Halmashauri ziliidhinishiwa jumla ya Shilingi trilioni 7.26,kati ya fedha hizo Shilingi trilioni 3.83 nikwa ajili ya mishahara, Shilingi bilioni 680.42 ni Matumizi Mengineyo yakijumuisha Shilingi bilioni 147.65 ruzuku kutoka Serikali Kuu, na Shilingi bilioni 532.77 Mapato ya Ndani ya Halmashauri. Aidha, Shilingi trilioni 2.75 nikwa ajili ya miradi ya maendeleo, ambapo Shilingi bilioni 957.51 niruzuku kutoka Serikali Kuu, Shilingi bilioni 331.08 ni Mapato ya Ndani ya Halmashauri na Shilingi trilioni 1.46 ni fedha za nje.
- Mheshimiwa Spika, hadi Februari 2022 Halmashauri zimepokea jumla ya Shilingi trilioni 4.47, kati ya fedha hizo Shilingi trilioni 2.64 ni kwa ajili ya mishahara, sawa na asilimia 68.96, Shilingi bilioni 492.66 sawa na asilimia 72.41 ni matumizi mengineyo, yakijumuisha Shilingi bilioni 122.70 ruzuku kutoka Serikali Kuu, na Shilingi bilioni 369.96 Mapato ya Ndani ya Halmashauri. Aidha, Shilingi trilioni 1.34 ni kwa ajili ya miradi ya maendeleo, sawa na asilimia 48.75 zikijumuisha Shilingi bilioni 696.25 ruzuku ya Serikali Kuu, Shilingi bilioni 216.11 Mapato ya Ndani ya Halmashauri, na Shilingi bilioni 429.10 nifedha za nje(Kiambatisho Na. 1).
Fedha za Nyongeza za Miradi ya Maendeleo
- , katika Mwaka wa Fedha 2021/22 Ofisi ya Rais – TAMISEMI iliidhinishiwa fedha za nyongeza Shilingi bilioni 686.55 ambapo kati ya fedha hizo, Shilingi bilioni 512.14 zimetokana na Mpango wa Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano Dhidi ya UVIKO – 19 (TCRP); Shilingi bilioni 93.00 zimetokananaTozo za Miamala ya simu; Shilingi bilioni 7.76 kutoka kwenye Programu Endelevu ya Usambazaji Maji na Usafi wa Mazingira (SRWSS); Shilingi bilioni 17.25 kutokaMradi wa Lipa Kulingana na Matokeo katika Elimu (EP4R).
- Mheshimiwa Spika, fedha nyingine za nyogeza ya bajeti ni Shilingi bilioni 12.62 kutokaMradi waKuimarisha Ufundishaji na Ujifunzaji kwa ElimuMsingi Awamu ya Pili (GPE-LANES); Shilingi bilioni 8.24 kutoka Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA); Shilingi bilioni 2.98 kwa ajili ya kulipa madeni ya watumishi (walimu wastaafu); Shilingi bilioni 9.19 kwa ajili ya utoaji wa chanjo; na Shilingi bilioni 22.87 ni kwa ajili ya kulipa madeni yawazabuni katika Mamlaka za Serikali za Mitaa.
- Mheshimiwa Spika, hadi Februari, 2022 zimepokelewa jumla ya Shilingi bilioni 535.07 ambapo Shilingi bilioni 360.66 ni kwa ajili yaMpango wa Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano Dhidi ya UVIKO – 19 (TCRP); Shilingi bilioni 93.00 ni za Tozo za Miamala ya simu; Shilingi bilioni 7.76 kutoka kwenye Programu Endelevu ya Usambazaji Maji na Usafi wa Mazingira (SRWSS); Shilingi bilioni 17.25 kutokaMradi wa Lipa Kulingana na Matokeo katika Elimu (EP4R).
- Mheshimiwa Spika, fedha nyingine zilizopokelewa ni Shilingi bilioni 12.62 kutokaMradi waKuimarisha Ufundishaji na Ujifunzaji kwa ElimuMsingi Awamu ya Pili (GPE-LANES); Shilingi bilioni 8.24 kutoka Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA); Shilingi bilioni 2.98 kwa ajili ya kulipa madeni ya watumishi (walimu wastaafu); Shilingi bilioni 9.19 kwa ajili ya utoaji wa chanjo; na Shilingi bilioni 22.87 ni kwa ajili ya kulipa madeni yawazabuni katika Mamlaka za Serikali za Mitaa.
Utekelezaji wa Bajeti ya Ofisi ya Rais – TAMISEMI kwa Mwaka wa Fedha 2021/22
- Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha 2021/22 Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Tume ya Utumishi wa Walimu, Mikoa na Halmashauri zimetekeleza shughuli zifuatazo: –
HUDUMA ZA AFYA YA MSINGI
- , katika Mwaka wa Fedha 2021/22 Ofisi ya Rais – TAMISEMI iliidhinishiwa Shilingi bilioni 28.20 kupitia ruzuku ya Serikali Kuu kwa ajili ya ukamilishaji wa ujenzi wa maboma 564 ya Zahanati katika Mamlaka za Serikali za Mitaa. Hadi kufikia Februari 2022, zimepokelewa Shilingi bilioni 23.32 sawa na asilimia 82.69 ya fedha zilizoidhinishwa. Ukamilishaji wa ujenzi upo katika hatua mbalimbali (Kiambatisho Na. 2).
- katika Mwaka wa Fedha 2021/22 Shilingi bilioni 110.60 ziliidhinishwa kupitia ruzuku ya Serikali Kuu kwa ajili ya kuendelea na ujenzi wa Vituo vya Afya 304. Kati ya hivyo, Vituo 52 vilianza kujengwa Mwaka wa Fedha 2019/20 na Vituo 252 vimeanza kujengwa Mwaka wa Fedha 2021/22 ambapo Vituo 18 vimejengwa kwenyeHalmashauri zenye Mapato madogo na Vituo 234 vimejengwakatika Tarafa zisizo kuwa na Vituo vya Afya na Kata za Kimkakati kupitia tozo za miamala ya simu. Hadi Februari, 2022 Shilingi bilioni 108.05 zimepokelewa sawa na asilimia 97.69 ya fedha zilizoidhinishwa na ujenzi unaendelea (Kiambatisho Na. 3).
- Spika, katika Mwaka wa Fedha 2021/22 Serikali ilitenga Shilingi bilioni 81.10 kwa ajili ya kuendelea na ujenzi wa Hospitali 68 zilizoanza kujengwa mwaka2018/19,Hospitali 31 zilizoanza kujengwa mwaka 2019/20 na kuanza ujenzi wa Hospitali mpya 28. Hadi Februari, 2022 Shilingi bilioni 66.80 sawa na asilimia82.36 zilikuwa zimepokelewa na ujenzi upo katika hatua mbalimbali (Kiambatisho Na. 3).
- Spika, katika Mwaka wa Fedha 2021/22 Ofisi ya Rais – TAMISEMI iliidhinishiwa Shilingi bilioni 11.30 kwa ajili ya ununuzi wa vifaa na vifaa tiba kwa Hospitali 31 za Awamu ya Pili zilizoanza kujengwa katika Mwaka wa Fedha 2018/19. Hadi Februari, 2022 zimepokelewa Shilingi bilioni 5.83 sawa na asilimia 51.59 ambapo fedha hizi zimepelekwa kwenye Halmashauri kumi na moja (11) kwa ajili ya ununuzi wa vifaa na vifaa tiba (Kimbatisho Na. 3).
Utekelezaji wa Miradi kupitia Mpango wa Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano Dhidi ya UVIKO-19
- , katika kuendelea kuimarisha huduma za Afya ya Msingi, katika Mwaka wa Fedha 2021/22 Ofisi ya Rais – TAMISEMI imepokea Shilingi bilioni 52.16 kati ya Shilingi bilioni 203.14 sawa na asilimia 25.67 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika sekta ya afya kupitia Mpango wa Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya UVIKO 19.
- fedha hizo zimeelekezwa katika ujenzi wa majengo 28 ya wagonjwa mahututi (ICUs); majengo 80 ya dharura (EMDs), nyumba 150 (3 in 1) kwa ajili ya watumishi wa Afya zinazoendelea kujengwa katika maeneo ya pembezoni; ujenzi wa kituo cha matibabu ya magonjwa ya mlipuko katika Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu; ajira 150 za mkataba kwa watumishi wa sekta ya Afya pamoja na uhamasishaji wa chanjo dhidi ya UVIKO – 19. Utekelezaji wa ujenzi upo katika hatua mbalimbali na unatarajiwa kukamilika ifikapo Mei, 2022.
- , vilevile, Ofisi ya Rais – TAMISEMI ilipokea Shilingi bilioni 9.19 kutoka Shirika la Global Alliance for Immunization(GAVI) kwa ajili ya utoaji wa chanjo ya kukabiliana na mlipuko wa UVIKO – 19 ambapo mafunzo kwa watoa huduma za afya, utoaji wa chanjo kwa njia ya mkoba na tembezi, uhamasishaji wa jamii na usimamizi wa usambazaji wa chanjo za UVIKO – 19 ulifanyika katika Mikoa yote 26 na Mamlaka za Serikali za Mitaa 184.
Huduma za Ustawi wa Jamii
- , kuanzia Julai 2021 hadi Februari 2022 mashauri 57,088 ya ukatili wa kijinsia na ukatili dhidi ya watoto yaliripotiwa. Kati ya hayo, mashauri 38,464 sawa na asilimia 67 ni ukatili dhidi ya wanawake na 18,624 sawa na asilimia 33 ni ukatili dhidi ya watoto. Mashauri 53,199 yalitatuliwa na Ofisi zaUstawi wa Jamii ngazi ya Halmashauri na mashauri 3,889 yalifikishwa mahakamani ambapo mashauri 1,501 sawa na asilimia 39 yametolewa hukumu.
- , vilevile, mashauri ya migogoro ya kifamilia 79,679 yaliripotiwa, kati ya hayo, mashauri 77,654 sawa na asimilia 97 yalitatuliwa na Ofisi za Ustawi wa Jamii ngazi ya Halmashauri na mashauri 2,025 sawa na asilimia 2.5 yalifikishwa mahakamani na kutolewa hukumu.
- Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha Julai 2021 hadi Februari 2022 jumla ya watoto 692,901 ambapo Wavulana ni 336,809 na Wasichana 356,092 walio katika mazingira hatarishi walitambuliwa na kupewa huduma za chakula, malazi, mavazi, matibabu na wengine 330,250 sawa na asilimia 48 waliunganishwa na familia zao.
- Mheshimiwa Spika, vilevile ununuzi wa pikipiki 68 zenye thamani ya Shilingi milioni 789.8 kwa ajili ya Maafisa Ustawi wa Jamii kwenye ngazi ya Kata umefanyika na kusambazwa katika Mamlaka za Serikali za Mitaa. Aidha, vifaa vya ofisi kwa ajili ya Ofisi za Ustawi wa Jamii katika Halmashauri zikiwemo meza 57, viti 156, makabati 1,033 vyote vikiwa na thamani ya Shilingi milioni 613.07 katika Halmashauri 81.
- Mheshimiwa Spika, watoto 3,605 walio kwenye mazingira hatarishi katika Halmashauri 81 walipewa mafunzo ya ufundi kupitia Vyuo vya Ufundi Stadi (VETA) na kupewa vifaa vya kuanzia kazi vyenye thamani ya Shilingi bilioni 15.6. Vilevile, watoto 117,513 wanaoishi katika mazingira hatarishi kwenye kaya 40,487 katika Halmashauri 71 wamepewa Kadi za Mfuko wa Afya ya Jamii iliyoboreshwa (iCHF) zenye thamani ya Shilingi bilioni 1.71.
- Mheshimiwa Spika, hadi Februari 2022 mfumo wa usajili na utoaji wa vyeti vya kuzaliwa bila malipo kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano uliozinduliwa katika Mikoa ya Arusha na Manyara umefanyika jumla ya watoto 634,222 ambao wamesajiliwa. Mpango huu unatarajia kuendelea katika mikoa yote. Aidha, jumla ya Watu Wenye Ulemavu 124,900 wametambuliwa ambapo wanawake ni 59,059 na Wanaume 65,841. Kati ya hao wanufaika 15,596 wamepatiwa huduma mbalimbali zenye thamani ya Shilingi bilioni 1.30 zikiwemo vifaa saidizi, huduma za utengamao na matibabu.
Huduma za Lishe
- Ofisi ya Rais – TAMISEMI imeendelea kusimamia utekelezaji wa Mkataba wa Lishe unaotekelezwa katika Mikoa na Halmashauri zote nchini ambao ulisainiwa mnamo Desemba 2017 baina ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais – TAMISEMI na Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri na Watendaji wa Kata, Watendaji wa Kata na Watendaji wa Vijiji/Mitaa. Mkataba wa lishe umesaidia kuongeza uwajibikaji na usimamizi wa utekelezaji wa Afua za Lishe.
- Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha 2021/22, Shilingi bilioni 11.9 zilitengwa katika Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa ajili ya kutekeleza afua za lishe ikiwemo kutoa elimu ya lishe ngazi ya jamii, nyongeza ya Vitamin A kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano (5), kutoa vidonge vya kuongeza damu kwa akina mama wajawazito na wanaonyonyesha. Fedha hizo zinatokana na Mpango wa kila Halmashauri kutenga Shilingi 1,000.00 kwa kila mtoto mwenye umri wa chini ya miaka mitano. Hadi Februari, 2022 Shilingi bilioni 6.62 sawa na asilimia 56 zilikuwa zimepokelewa na kutumika kutekeleza afua za lishe. Ofisi ya Rais – TAMISEMI itaendelea kuratibu na kusimamia utengaji na utolewaji wa fedha hizo katika Halmashauri.
USIMAMIZI NA UENDESHAJI WA ELIMU YA MSINGI NA SEKONDARI
- Spika, katika Mwaka wa Fedha 2021/22 Ofisi ya Rais – TAMISEMI imeendelea kusimamia uimarishaji wa utoaji wa huduma ya elimumsingi. Shughuli zilizotekelezwa ni pamoja na:
Elimumsingi
Uandikishaji wa Wanafunzi wa Elimu ya Awali
- , katika mwaka wa masomo 2021 wanafunzi wapya wa Darasa la Awali walioandikishwa ni 1,198,564 sawa na asilimia 94.19 ya lengo la kuandikisha wanafunzi 1,272,513. Mwaka wa masomo 2022 jumla ya wanafunzi 1,363,834 walitarajiwa kuandikishwa. Hadi Machi, 2022 wanafunzi 1,411,810 sawa na asilimia 103.52 ya lengo wakiwemo wanafunzi wenye mahitaji maalum 3,511 wameandikishwa. Uandikishwaji huo ni ongezeko la wanafunzi 213,246 sawa na asilimia 17.79 ikilinganishwa na wanafunzi walioandikishwa kwa kipindi kama hiki kwa mwaka 2021 (Kiambatisho Na. 4).
Uandikishaji wa Wanafunzi wa Darasa la Kwanza
- Spika, katika mwaka wa masomo 2021 wanafunzi 1,516,598 walitarajiwa kuandikishwa Darasa la Kwanza, walioandikishwa ni wanafunzi 1,549,279 sawa na asilimia 102.15 ya lengo. Katika mwaka wa masomo 2022 wanafunzi wa Darasa la Kwanza walioandikishwa hadi Machi, 2022 ni 1,726,165 wakiwemo wanafunzi wenye mahitaji maalum 4,723 ambapo wavulana ni 2,618 na wasichana ni 2,105 wenye mahitaji maalum sawa na asilimia 108.40 ya lengo la kuandikisha wanafunzi 1,592,375 (Kiambatisho Na. 5).
Uandikishaji wa Wanafunzi wa Kidato cha Kwanza
- jumla yawanafunzi 907,803 ambapo wavulana ni 467,967 na wasichana 439,836 walichaguliwa kujiunga na Kidato cha Kwanza mwaka 2022. Hadi Machi, 2022 wanafunzi 804,269 ambapo wavulana ni 400,469 na wasichana 403,800 wameandikishwa shule sawa na asilimia 88.60 ya wanafunzi waliochaguliwa. Kati ya wanafunzi walioandikishwa, wanafunzi wenye mahitaji maalum ni 1,247 ambapo wavulana ni 699 na wasichana 548 (Kiambatisho Na. 6).
Upimaji wa Kitaifa wa Darasa la Nne
- , katika matokeo ya Upimaji wa Kitaifa wa Darasa la Nne mwaka 2020, jumla ya Wanafunzi 1,551,599 kati ya wanafunzi 1,704,286 sawa na asilimia 91.04 walikidhi sifa za kuendelea Darasa la Tano. Aidha, katika mwaka 2021 jumla ya wanafunzi 1,681,791 ambapo wasichana ni 856,860 na wavulana 824,931 walisajiliwa kufanya mtihani wa upimaji wa darasa la nne. Waliofanya mtihani ni wanafunzi 1,561,599 ambapo wasichana ni 808,047 na wavulana 753,552 kati yao wanafunzi waliokidhi sifa za kuingia darasa la tano katika mwaka wa masomo 2022 ni 1,347,554 ambapo wasichana ni 708,203 na wavulana 639,351.
Mtihani wa Kuhitimu Elimu ya Msingi
- Spika, katika Mtihani wa Kuhitimu Darasa la Saba mwaka 2021 jumla ya wanafunzi 1,132,084 ambapo wasichana ni 584,614 na wavulana 547,470 walisajiliwa kufanya Mtihani wa Kuhitimu Elimu ya Msingi. Watahiniwa 1,108,023 ambapo wasichana ni 574,998 na wavulana 533,025 wakiwemo wanafunzi 3,279 wenye mahitaji maalum walifanya mtihani. Watahiniwa 907,802 ambapo wasichana ni 467,967 na wavulana 439,835 walifaulu wakiwemo wanafunzi wenye mahitaji maalum 2,673 ambapo wasichana ni 1,202 na wavulana 1,471.
Elimu ya Sekondari
Upimaji wa Kitaifa wa Kidato cha Pili
- , takwimu za matokeo ya Upimaji wa Kidato cha Pili zinaonesha kuwa kwa mwaka 2021, jumla ya wanafunzi 555,857 sawa na asilimia 92.32 kati ya wanafunzi 602,107 katika matokeo ya Upimaji wamepata ujuzi na maarifa ya kuwawezesha kuendelea na Kidato cha Tatu, ambapo wasichana ni 300,492 na wavulana ni 255,365. Mwaka 2020 wanafunzi 550,979 sawa na asilimia 91.61 walipata alama za kuwawezesha kuendelea na masomo ya Kidato cha Tatu. Hivyo, ufaulu wa Kidato cha Pili umepanda kwa asilimia 0.71 ikilinganishwa na mwaka 2020.
Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Nne
- , kwa upande wa Kidato cha Nne jumla ya Watahiniwa wa Shule 422,388 ikiwa wasichana ni 218,174 na wavulana 204,214 wamefaulu sawa na asilimia 87.30 ya watahiniwa 483,820 waliofanya mtihani wa kuhitimu Kidato cha Nne mwaka 2021. Mwaka 2020 watahiniwa 373,958 sawa na asilimia 85.84 ya Watahiniwa wa Shule walifaulu mtihani huo. Hivyo, ufaulu wa Watahiniwa wa Shule mwaka 2021 umeongezeka kwa asilimia 1.46 ikilinganishwa na mwaka 2020.
Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Sita
- , ufaulu wa Kidato cha Sita kwa mwaka 2021 ulikuwa ni asilimia 99.62 ambapo watahiniwa 79,596 kati ya watahiniwa 80,302 waliofanya mtihani walifaulu ikilinganishwa na mwaka 2020 ambapo watahiniwa 73,537 kati ya 74,284 ya waliofanya mtihani walifaulu sawa na asilimia 99.51 ya watahiniwa. Ufaulu wa Kidato cha Sita umeendelea kuwa bora zaidi kila mwaka.
Wanafunzi waliochaguliwa Kidato cha Tano mwaka, 2021
- , jumla ya wanafunzi 87,663 ambapo wasichana ni 41,885 na wavulana 45,778 sawa na asilimia 58.67 ya wanafunzi 148,127 wenye sifawalichaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano katika shule 476 za Serikali. Kati yao wanafunzi wenye mahitaji maalumu walikuwa ni 288 wakiwemo wasichana 123 na wavulana 165 sawa na asilimia 100 ya wenye mahitaji maalum waliokuwa na sifa za kujiunga Kidato cha Tano. Kati ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano, wanafunzi 41,504 wakiwemo wasichana 17,646 na wavulana 23,858 sawa na asilimia 47.34, wamechaguliwa kusoma tahasusi za Sayansina Hisabati; wanafunzi 46,159 wakiwemo wasichana24,239 na wavulana 21,920 sawa na asilimia 52.66 wamechaguliwa kusoma tahasusi za masomo ya Sanaa na Biashara.
Elimu ya Watu Wazima na Elimu Nje ya Mfumo Rasmi
- Spika, uandikishaji wa wanafunzi wa Mpango wa Elimu ya Msingi kwa Walioikosa (MEMKWA) umeendelea kupungua mwaka hadi mwaka. Matokeo ya uandikishaji kwa wanafunzi hao hadi mwezi Februari 2022 yanaonesha kupungua ambapo wanafunzi 12,421 wakiwemo wavulana 6,880 na wasichana 5,541 wameandikishwa. Idadi hiyo imepungua kwa asilimia 75.25 ikilinganishwa na wanafunzi 50,192 wakiwemo wavulana 27, 819 na wasichana 22,373 walioandikishwa mwaka 2021.
- kupungua kwa uandikishaji kunatokana na mafanikio ya utekelezaji wa Mpango wa Elimumsingi Bila Malipo ambapo kuanzia mwaka 2015 hadi Februari, 2022 mpango umewezesha wanafunzi wenye umri wa kwenda shule kuandikishwa kutokana na kuondolewa kwa ada na michango mbalimbali ambayo ilikuwa ni miongoni mwa vikwazo vilivyopunguza kiwango cha uandikishaji. Sababu nyingine ni kutokana na kusogeza huduma za Elimumsingi karibu na wanafunzi kwa kujenga na kuboresha Vituo shikizi vilivyowapunguzia wanafunzi kutembea umbali mrefu kufuata huduma ya elimu. Hii inaashiria kwamba wanafunzi waliokuwa wanakosa nafasi ya elimu katika mfumo rasmi sasa wanapata fursa hiyo. Aidha, uandikishaji wa watoto wenye umri wa kwenda shule unafanyika kwa wakati.
Elimu Maalum
- Ofisi ya Rais – TAMISEMI inasimamia Shule Maalum 37 za bweni, Vitengo Maalum 710 vinavyoshughulikia wanafunzi wenye mahitaji maalum katika Shule za Msingi na Shule Jumuishi 3,956 zenye wanafunzi wenye mahitaji maalum wa Shule za Msingi. Kwa upande wa Sekondari, kuna Shule Maalum moja ya Patandi na Shule Jumuishi 127. Vilevile,katika Mwaka wa Fedha 2021/22, Serikali imeajiri walimu 766 waliosomea taaluma ya Elimu Maalum ili kuhakikisha kuwa wanafunzi wenye mahitaji maalum wanapata elimu sawa na wanafunzi wengine. Aidha, Serikali imenunua na kusambaza vifaa visaidizi 82,919 vyenye thamani ya Shilingi bilioni 4.6 kwenye shule zenye wanafunzi wenye mahitaji maalum.
Michezo kwa Shule za Msingi na Sekondari
- Ofisi ya Rais -TAMISEMI imeendelea kuhimiza na kusimamia maendeleo ya michezo katika Shule za Msingi na Sekondari ikiwemo ufundishaji wa somo la Elimu kwa michezo darasani. Katika mwaka wa masomo 2021 ufaulu wa somo la Elimu kwa michezo kwa wanafunzi wanaomaliza Kidato cha Nne umeongezeka kutoka asilimia 45.3 mwaka 2020 hadi asilimia 83 mwaka 2021 ambapo watahiniwa 1,702 walifanya mtihani wa somo la elimu kwa michezo ikilinganishwa na idadi ya wanafunzi 1,669 wa mwaka 2020. Aidha, mashindano ya michezo ya Umoja wa Michezo na Taaluma Shule za Msingi Tanzania (UMITASHUMTA) na Umoja wa Michezo Shule za Sekondari Tanzania (UMISSETA) yaliendelea kufanyika kwa ubora zaidi na hivyo kuendelea kuwa kitalu cha kuendeleza na kuvuna wanamichezo wa kuunda timu za taifa za michezo mbalimbali kwa vijana.
Tathmini ya Mahitaji ya Walimu kwa Shule za Msingi na Sekondari
- , takwimu zilizopo zinaonesha kuwa kuna jumla ya Shule za Msingi 17,034 zenye jumla ya wanafunzi 12,033,594 wakiwemo wanafunzi wenye mahitaji maalum 60,825 na Shule za Sekondari 4,175 zenye jumla ya wanafunzi 2,607,142 wakiwemo wanafunzi wenye mahitaji maalum 11,106.Jumla ya walimu waliopo ni 258,291 wakiwemo walimu wa Shule za Msingi 173,591 na Sekondari walimu 84,700.
- , hadi Machi, 2022 mahitaji ya walimu katika Shule za Msingi ni 274,549 kwa kutumia uwiano wa 1:60 (Mwalimu mmoja kwa wanafunzi 60) walimu waliopo ni 173,591 na upungufu ni 100,958 sawa na asimilia 36.77 ya mahitaji. Aidha, mahitaji ya walimu kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum kwa Shule za Msingi ni walimu 3,631, waliopo ni 1,517 na upungufu ni walimu 2,143 sawa na asilimia 59.02 ya mahitaji. Vilevile, mahitaji ya walimu kwa Shule za Sekondari ni 159,443 waliopo ni 84,700 na upungufu ni walimu 74,743 sawa na asilimia 46.87.
Ujenzi na Ukamilishaji wa Miundombinu ya Elimu ya Msingi na Sekondari
Ujenzi wa Miundombinu ya Elimu
- , kipekee nichukue fursa hii kumshukuru Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuzipatia Mamlaka za Serikali za Mitaa Shilingi bilioni 304.00, kutokana na mkopo wenye masharti nafuu kutoka Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) kwa ajili ya kukabiliana na athari za kiuchumi zilizotokana na ugonjwa wa UVIKO-19.
- Spika, fedha hizi zimetumika katika ujenzi wa vyumba vya madarasa 12,000 katika Shule za Sekondari, vyumba vya madarasa 3,000 katika Vituo shikizi na mabweni 50 kwa ajili ya wanafunzi wenye mahitaji maalum. Hadi Februari, 2022 vyumba vya madarasa 11,988 kati ya vyumba 12,000 vya Shule za Sekondari vimejengwa na kukamilika sawa na asilimia 99.99. Vilevile, vyumba vya madarasa 2,978 kati ya 3,000 vimejengwa na kukamilika katika Vituo shikizi sawa na asilimia 99.26. Aidha, mabweni 49 yanaendelea kujengwa na yanategemewa kukamilika ifikapo tarehe 30 Aprili, 2022. Kupitia Mpango huo, ofisi za walimu 3,184, matundu ya vyoo 557 yamejengwa, ajira zilizozalishwa 21,872 wakiwemo wanaume 17,354 na wanawake, 4,518, madawati 47,149 na seti ya meza na viti 451,918 vimetengenezwa.
- , utekelezaji wa mpango huo umepunguza uhaba wa miundombinu ya shule katika Shule za Msingi na Sekondari. Hii imewezesha wanafunzi wote 907,803 waliofaulu mtihani wa darasa Saba mwaka 2021 kupata nafasi ya kuanza Kidato cha Kwanza Januari, 2022 bila kuwa na chaguo la pili.
- , katika Mwaka wa Fedha 2021/22 kupitia Programu ya Uboreshaji wa Elimu katika Shule za Sekondari (Secondary Education Quality Improvement Program-SEQUIP) jumla ya Shilingi bilioni 30 zimepokelewa ambapo kila Shule imepokea Shilingi bilioni 3.00 kwa ajili ya kuanza ujenzi wa Shule za Sekondari za masomo ya sayansi kwa Wasichana (Kiambatisho Na. 7).
- , kupitia SEQUIP katika Mwaka wa Fedha 2021/22 Ofisi ya Rais – TAMISEMI imepokea Shilingi bilioni 109.57 kwa ajili ya ujenzi wa Shule za Sekondari 232 ambazo zitajengwa kwenye kata zisizokuwa na Shule za Sekondari kwa Awamu ya Kwanza ambapo kila Shule imepokea Shilingi milioni 470 kwa ajili ya kuanza ujenzi huo. Aidha, Shule moja kati ya shule hizo imepokea Shilingi bilioni 1.00 kwa ajili ya kuanza ujenzi wa shule ya sekondari ya Kidato cha Tano na Sita (Kiambatisho Na. 7).
- katika Mwaka wa Fedha 2021/22 Ofisi ya Rais – TAMISEMI imepokea Shilingi bilioni 8.24 kutoka Mamlaka ya Elimu Tanzania (Tanzania Education Authority-TEA) kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya Shule za Msingina Sekondari. Miundombinu itakayojengwa ni pamoja na vyumba vya madarasa 210 katika shule 65 (Shule za Msingi 53 na Sekondari 12), ujenzi wa maabara sita (6) katika Shule za Sekondari mbili (2), matundu 1,920 ya vyoo katika shule 80 (Shule za Msingi 58 na Sekondari 22), miundombinu kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum katika shule 9 ambapo Shule za Msingi 8 na shule moja (1) ya Sekondari na ofisi za walimu katika shule mbili (2) za Sekondari.
- , katika Mwaka wa Fedha 2021/22 Ofisi ya Rais – TAMISEMI imepokea jumla ya Shilingi bilioni 17.25 kwa ajili ya ujenzi wa Shule mpya za Sekondari 15 na Shule za Msingi 9 kupitia Programu ya Lipa Kulingana na Matokeo (Education Performance for Results – EP4R).
- , katika Mwaka wa Fedha 2021/22 Ofisi ya Rais – TAMISEMI imepokea Shilingi bilioni 12.37 kupitia Mradi wa Kuimarisha Ufundishaji na Ujifunzaji katika Elimu ya Msingi (Global Partnership for Education – GPE LANES II). Kazi zinazoendelea kufanyika ni ujenzi wa vyumba 304 vya madarasa, mabweni nane (8) ya wanafunzi wenye mahitaji maalum katika Shule za Msingi, nyumba 11 za walimu, matundu 548 ya vyoo, ujenzi wa shule mpya 10 za Msingi na majengo manne (4) ya utawala.
Ukamilishaji wa Ujenzi wa Maboma ya Madarasa na Maabara kupitia Ruzuku ya Serikali Kuu
- , katika Mwaka wa Fedha 2021/22 Serikali iliidhinisha jumla ya Shilingi bilioni 23.16 kwa ajili ya ukamilishaji wa ujenzi wa maboma ya vyumba vya madarasa 1,853 katika Shule za Msingi. Hadi Februari 2022, Shilingi bilioni 20.31 zimetolewa sawa na asilimia 87.71 ya fedha iliyoidhinishwa. Aidha, ukamilishaji wa ujenzi wa maboma ya vyumba vya madarasa unaendelea (Kiambatisho Na. 8).
- katika Mwaka wa Fedha 2021/22 jumla ya Shilingi bilioni 23.00 ziliidhinishwa kwa ajili ya ukamilishaji wa ujenzi wa vyumba 1,840 vya madarasa katika Shule za Sekondari. Hadi Februari, 2022 zimetolewa Shilingi bilioni 23.00 sawa na asilimia 100 ambapoukamilishaji wa ujenzi wa madarasa haya upo katika hatua mbalimbali. (Kiambatisho Na. 8)
- katika kuimarisha Elimu ya Sayansi kwa Vitendo Serikali imeendelea kutenga fedha kwa ajili ya ukamilishaji ujenzi wa vyumba vya maabara ya masomo ya sayansi katika Shule za Sekondari. Katika Mwaka wa Fedha 2021/22, Ofisi ya Rais – TAMISEMI iliidhinishiwa Shilingi bilioni 26.07 kwa ajili ya ukamilishaji waujenzi wavyumba 869 vya maabara za masomo ya sayansi. Hadi Februari, 2022 zimetolewa Shilingi bilioni 22.27 sawa na asilimia 85.42 ya fedha zilizoidhinishwa na ukamilishaji wa ujenzi upo katika hatua mbalimbali (Rejea Kiambatisho Na. 8).
- katika Mwaka wa Fedha 2021/22 Serikali ilianzisha tozo ya miamala ya simu kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya kutolea huduma ambapo Ofisi ya Rais – TAMISEMI ilipokea jumla ya Shilingi bilioni 7.00 kwa ajili ya kukamilisha maboma 560 ya vyumba vya madarasa katika Shule za Sekondari ambapo utekelezaji upo katika hatua mbalimbali (Kiambatisho Na. 8).
ElimuMsingi bila Malipo
- , katika Mwaka wa Fedha 2021/22 ziliidhinishwa jumla ya Shilingi bilioni 312.05 kwa ajili ya utekelezaji wa Mpango wa Elimumsingi Bila Malipo. Kati ya fedha hizo, Shilingi bilioni 142.72 ni kwa ajili ya Shule za Msingi na Shilingi bilioni 169.33 kwa Shule za Sekondari. Hadi Februari, 2022 jumla yaShilingi bilioni 192.44 zimepelekwa katika shule sawa na asilimia 61.67 ambapo Shilingi bilioni 89.62 ni kwa ajili ya Shule za Msingi na Shilingi bilioni 102.82 kwa ajili ya Shule za Sekondari. Fedha hizi ni zinatumika katika maeneo ya uendeshaji wa shule, chakula kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum wa Shule za Msingi na wanafunzi wa bweni wa Shule za Sekondari, fidia ya ada kwa wanafunzi wa kutwa na bweni wa Kidato cha Kwanza hadi cha Nne na posho ya madaraka kwa Wakuu wa Shule na Maafisa Elimu Kata (Kiambatisho Na. 9 & 10).
Ajira katika Sekta ya Afya na Elimu
- Mheshimiwa Spika, kutokana na upungufu wa watumishi katika sekta ya afya na elimu chini ya Ofisi ya Rais – TAMISEMI Serikali imeendelea kutoa ajira za watumishi katika maeneo hayo. Katika Mwaka wa Fedha 2021/22 Serikali kupitia Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora imetoa vibali vya nafasi za ajira 17,412 ambapo 7,612 ni ajira za watumishi wa kada za afya na 9,800 ni ajira za walimu wa shule za msingi na sekondari. Naomba nitumie fursa hii kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimwa Samia Suluhu Hassan kwa kutoa kibali cha ajira hizo za watumishi.
MAPATO YA NDANI YA HALMASHAURI
- Spika, katika mwaka wa fedha 2021/22 Halmashauri ziliidhinishiwa kukusanya Shilingi bilioni 863.85 kutoka kwenye vyanzo vyake vya Mapato ya Ndani ikiwa ni ongezeko la Shilingi bilioni 48.94 ikilinganishwa na bajeti ya Shilingi bilioni 814.96 ya Mwaka wa Fedha 2020/21.
- Mheshimiwa Spika, hadi Februari, 2022 Halmashauri zimekusanya jumla ya Shilingi bilioni 586.07 sawa na asilimia 67.84 ya makisio kwa Mwaka wa Fedha 2021/22. Makusanyo haya ni ongezeko la Shilingi bilioni 112.13 ikilinganishwa na makusanyo ya Shilingi bilioni 473.94 yaliyokusanywa kwa kipindi kama hiki mwaka 2020/21 (Kiambatisho Na. 11).
- Mheshimiwa Spika, kuongezeka kwa Mapato kumetokana na Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kuweka mikakati ya pamoja ya kubuni vyanzo vipya, kuimarisha vilivyopo na mikakati zaidi ya ukusanyaji wa mapato.
- Mheshimiwa Spika,Ofisi ya Rais – TAMISEMI itaendelea kuzisimamia Halmashauri ili ziongeze wigo wa ukusanyaji wa mapato ya ndani. Mikakati iliyowekwa ni pamoja na kuwajengea uwezo maafisa wanaokusanya mapato, kuboresha mfumo wa ukusanyaji mapato na utambuzi wa fursa na uibuaji wa vyanzo vipya vya mapato. Aidha, utendaji wa Halmashauri utapimwa kwa kuzingatia upelekaji wa asilimia 40/60 za fedha zinazotokana na makusanyo ya mapato ya ndani yasiyolindwa katika miradi ya maendeleo, utoaji wa mikopo ya asilimia 10 kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu Wenye Ulemavu, na urejeshaji wa mikopo na ujibuji wa hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa wakati.
Miradi ya Maendeleo iliyotekelezwa kupitia Fedha za Mapato ya Ndani ya Halmashauri
- Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha 2021/22 ziliidhinishwa jumla ya Shilingi bilioni 331.08 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo kupitia fedha za Mapato ya Ndani ya Halmashauri. Hadi Februari, 2022 jumla ya Shilingi bilioni 216.11 sawa na asilimia 65.27 zimetumika kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo ikiwa ni asilimia 40/60 ya Mapato yasiyolindwa kulingana na makundi ya Halmashauri.
- Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha 2021/22 Ofisi ya Rais -TAMISEMI iliidhinishiwa Shilingi bilioni 17.68 kwa ajili ya ukamilishaji wa ujenzi wa maboma 1,415 ya vyumba vya madarasa kwa Shule za Msingi kupitia Mapato ya Ndani ya Halmashauri. Hadi Machi, 2022 jumla ya Shilingi bilioni 19.43 zimetolewa sawa na asilimia 109.89 ya fedha zilizoidhinishwa kwa ajili ya ukamilishaji wa ujenzi wa vyumba madarasa. Ongezeko hilo limetokana na baadhi ya Halmashauri kuanza kujenga madarasa mapya kutokana na kutokuwa na maboma ya madarasa ya kumalizia.
- , katika Mwaka wa Fedha 2021/22 Ofisi ya Rais – TAMISEMI iliidhinishiwa Shilingi bilioni 9.95 kwa ajili ya ukamilishaji wa ujenzi wa Zahanati 199 kupitia Mapato ya Ndani ya Halmashauri. Hadi Machi, 2022 Shilingi bilioni 4.06 sawa na asilimia 40.84 ya fedha zilizoidhinishwa zimetolewa kwa ajili ya ukamilishaji wa ujenzi wa Zahanati ambao upo katika hatua mbalimbali za utekelezaji. (Kiambatisho Na. 2).
- , katika Mwaka wa Fedha 2021/22 Ofisi ya Rais – TAMISEMI iliidhinishiwa Shilingi bilioni 51.50 kupitia Mapato ya Ndani ya Halmashauri kwa ajili ya ujenzi wa Vituo vya Afya 103. Hadi Machi, 2022 kiasi cha Shilingi bilioni 17.90 kimetolewa sawa na asilimia 34.14 kwa ajili ya ujenzi wa Vituo vya Afya ambavyo vipo katika hatua mbalimbali za ujenzi (Kiambatisho Na. 3).
Uwezeshaji wa Wananchi Kiuchumi Kutokana na Asilimia 10 ya Mapato ya Ndani ya Halmashauri
- Mheshimiwa Spika, Ofisi ya Rais – TAMISEMI imeendelea kusimamia utoaji wa Mikopo ya Uwezeshaji kwa Wanawake, Vijana na Watu Wenye Ulemavu kwa mujibu wa Kifungu cha 37A cha Sheria ya Fedha za Serikali za Mitaa, Sura 290 na Kanuni za Utoaji na Usimamizi wa Mikopo kwa Vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu Wenye Ulemavu za mwaka 2019 kwa ajili ya utoaji wa mikopo na riba isiyo na riba kwa vikundi hivyo.
- Mheshimiwa Spika, hadi Februari 2022 Halmashauri zimekopesha kiasi chaShilingi bilioni 35.55 ambapo Shilingi bilioni 19.36 zimetolewa kwa vikundi vya Wanawake 2,881, Shilingi bilioni 13.51 zimetolewa kwa vikundi vya Vijana 1,441 na Shilingi bilioni 2.68 zimetolewa kwa vikundi 580 vya Watu Wenye Ulemavu.
- Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha 2021/22 fedha zilizokusanywa kutokana na marejesho ni Shilingi bilioni 34.81 kutoka kwenye vikundi 29,443. Fedha zilizorejeshwa kiasi cha Shilingi bilioni 28.80 zimekopeshwa kwa vikundi 2,950 vya Wanawake, Vikundi 1,334 vya Vijana na Vikundi 322 vya Watu Wenye Ulemavu. Ofisi ya Rais – TAMISEMI kwa kushirikiana na Taasisi nyingine inaandaa mkakati wa kuimarisha ukopeshaji na urejeshaji wa fedha hizo.
- Mheshimiwa Spika, baadhi ya miradi mikubwa iliyotekelezwa kupitia fedha za asilimia 10 ni pamoja na Kikundi cha MIOMBO Beekepers Iniciateves Group kilicho katika Halmashauri ya Manispaa ya Tabora. Kikundi hiki kilikopeshwa Shilingi milioni 50.00 kwa ajili ya kuanzisha kiwanda cha kuchakata mazao yanayotokana na asali; Ujenzi wa kiwanda kidogo cha kutengeneza sabuni na dawa za usafi kinachomilikiwa na Kikundi cha Wanawake cha Juhudi ambapo kikundi hiki kilikopeshwa Shilingi milioni 380; Kiwanda cha kutengeneza Batiki kinachomilikiwa na Kikundi cha Wanawake cha Hand Product of Tanzania kilichokopeshwa Shilingi milioni 150; na Kikundi cha NURU Disabled kinajishughulisha na usafirishaji wa mizigo kwenda mikoani, kikundi hiki kinamiliki Lori aina ya SCANIA na kilikopeshwa Shilingi milioni 100. Vikundi vyote hivi vinapatikana katika Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Aidha, kikundi cha Bulldozer Youth Group kutoka Halmashauri ya Jiji la Tanga kinachojihusisha na shughuli za uvuvi na uuzaji wa samaki kimepata mkopo wa Shilingi milioni 50.00 na kununua boti ya uvuvi. Kikundi hiki kinafanya vizuri na kimetoa ajira za kudumu kwa vijana kumi (10) na kinatarajia kutoa ajira zaidi kwa anawake na vijana katika eneo linapojengwa bomba la mafuta. Nitumie fursa hii kutoa maelekezo kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa kuendelea kutoa elimu ya ujasiriamali na kutoa mikopo kwenye miradi yenye tija ili kuhakikisha fedha hizi zinaleta mabadiliko chanya kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu Wenye Ulemavu.
Maboresho ya Miundombinu ya Wafanyabiashara Wadogo (Machinga)
- Mheshimiwa Spika, kupitia Mpango wa Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya UVIKO-19 Ofisi ya Rais – TAMISEMI imepokea Shilingi bilioni 5.00 mwezi Machi, 2022 kwa ajili ya kufanya maboresho ya miundombinu ya maeneo ya wafanyabiashara wadogo (machinga) katika Halmashauri. Halmashauri zilizonufaika na fedha hizo ni za Majiji ya Dar es Salaam (Shilingi milioni 263.13), Arusha (Shilingi milioni 500.00), Mwanza (Shilingi milioni 500.00), Mbeya (Shilingi milioni 540.96), Dodoma (Shilingi milioni 500.00) na Tanga (Shilingi milioni 540.34); Halmashauri za Manispaa za Morogoro (Shilingi milioni 490.20), Kinondoni (Shilingi milioni 441.89), Temeke (Shilingi milioni 441.94), Ubungo (Shilingi milioni 398.50); na Halmashauri ya Mji Tunduma (Shilingi milioni 383.00). Utekelezaji wa miradi hiyo unaendelea katika maeneo yote yaliyopokea fedha. Serikali itaendelea kutafuta rasilimali fedha kwa ajili ya kujenga miundombinu ya machinga kwenye maeneo mengine ili yaweze kunufaika na mpango huo.
Miradi ya Kimkakati
- Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha 2021/22 ziliidhinishwa jumla ya Shilingi bilioni 68.70 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya kimkakati ili kuziwezesha Halmashauri kuongeza mapato kwa lengo la kupunguza utegemezi wa Serikali Kuu, miradi hiyo ni pamoja na ujenzi wa stendi za kisasa za mabasi, maegesho ya malori, ujenzi wa viwanda vya chaki na vifungashio pamoja na masoko yanayojengwa katika Halmashauri mbalimbali.
- Mheshimiwa Spika, hadi Februari, 2022 jumla ya Shilingi bilioni 22.01 sawa na asilimia 32.03 zimetolewa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi hiyo. Halmashauri 12 ambazo zinaendelea na utekelezaji wa miradi ni; Halmashauri za Majiji ya Dar es Salaam (ujenzi wa Soko la kisasa Kisutu umekamilika kwa asilimia 97), Tanga (ujenzi wa kituo cha mabasi Kange umekamilika kwa asilimia 80) na Mwanza (ujenzi wa soko la mjini kati katika Kata ya Pamba umekamilika kwa asilimia 71 na ujenzi wa kituo cha mabasi Nyegezi umekamilika kwa asilimia 73); Halmashauri za Manispaa za Kinondoni (ujenzi wa soko la kisasa Tandale umekamilika kwa asilimia 70) na Iringa (ujenzi wa machinjio ya kisasa Ngelewala umekamilika kwa asilimia 93).
- Mheshimiwa Spika, vilevile miradi mingine ya kimkakati inaendelea kutekelezwa katika Halmashauri za Miji ya Tunduma (ujenzi wa maegesho ya malori mpakani mwa Tanzania na Zambia umekamilika kwa asilimia 95 na ujenzi wa kituo cha mabasi Mpemba umekamilika kwa asilimia 70), Kibaha (ujenzi wa soko la kisasa katika eneo la kitovu cha Mji umekamilika kwa asilimia 90), Halmashauri za Wilaya za Maswa (ujenzi wa kiwanda cha chaki umekamilika kwa asilimia 99), Hanang (ujenzi wa kituo cha mabasi Kateshi Mjini umekamilika kwa asilimia 5) na Biharamulo (ujenzi wa kituo cha maegesho ya magari makubwa Nyakanazi umekamilika kwa asilimia 98). Aidha, miradi ya ujenzi wa kituo cha mabasi na maegesho ya malori katika Kata ya Nyamhongolo Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela na Soko la Magomeni katika Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni imekamilika.
UTAWALA BORA, USIMAMIZI WA RASILIMALI, UJENZI WA MAJENGO YA UTAWALA NA NYUMBA ZA VIONGOZI
Utawala Bora na Usimamizi wa Rasilimali
- Mheshimiwa Spika, Ofisi ya Rais – TAMISEMI imeendelea kusimamia Utawala Bora katika Tawala za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa na maeneo yaliyopatiwa kipaumbele kama ifuatavyo: –
Ushughulikiaji wa Kero na Malalamiko ya Wananchi katika Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa
- Mheshimiwa Spika, katika kuendelea kuimarisha Utawala bora, Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa zimeendelea kutekeleza dhana ya ‘‘TAMISEMI ya Wananchi’’. Katika kutekeleza dhana hiyo, Ofisi ya Rais – TAMISEMI imeendelea kuimarisha Kituo cha Huduma ya Mawasiliano kwa Mteja (Call Centre) kwa ajili ya kurahisisha utoaji wa huduma kwa wananchi bila ya kuhitajika kufika katika Ofisi ya Rais – TAMISEMI Dodoma.
- Mheshimiwa Spika, hadi Februari 2022, Kituo hiki kimehudumia jumla ya wananchi 126,000 kuhusu kero, malalamiko na ufafanuzi tangu kilipoanza kutoa huduma tarehe 06 Agosti, 2020. Pamoja na mafanikio yaliyopatikana, Kituo hiki kimesaidia kupunguza changamoto ya upatikanaji wa taarifa zinazohitajika kwa wananchi, naendelea kuwasisitiza Waheshimiwa Wakuu Mikoa kuanzisha Vituo vya Huduma ya Mawasiliano kwa Wateja (Call Centre) katika maeneo yao ili kuwapunguzia wananchi adha ya kusafiri umbali mrefu kutafuta huduma.
- Spika, Ofisi ya Rais – TAMISEMI imeendelea kuboresha na kuimarisha utendaji kazi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa ili zitoe huduma bora kwa wananchi. Katika kutekeleza azma hii, watumishi waliokaa kwenye vituo vya kazi kwa muda mrefu hususan Wakuu wa Idara na Vitengo wameanza kuhamishwa kutoka vituo vya zamani na kupelekwa katika vituo vipya. Aidha, Ofisi ya Rais – TAMISEMI itaendelea kuchukua hatua za kinidhamu kwa watumishi wasiozingatia Sheria, Kanuni na Taratibu za kazi ikiwa ni pamoja na kuwashusha vyeo na kuwaondoa kazini watumishi wazembe na wabadhirifu wa mali za umma.
- Mheshimiwa Spika, kupitia Bunge lako Tukufu naomba nitoe maelekezo kwa watumishi wote wa Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Taasisi zilizo chini yake, Tawala za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kuendelea kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia Sheria na Taratibu.
Usimamizi wa Fedha katika Mamlaka za Serikali za Mitaa
- Spika, Ofisi ya Rais – TAMISEMI imeendelea kutoa maelekezo kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa kuhusu usimamizi wa fedha kwa kuzingatia Sheria, Taratibu na Miongozo inayotolewa mara kwa mara ili kujenga nidhamu ya matumizi ya fedha za umma. Lengo ni kuhakikisha kazi zinazotekelezwa zinalingana na thamani ya fedha iliyotumika. Aidha, taarifa kwa umma kuhusu mwenendo wa makusanyo ya Mapato ya Ndani katika Halmashauri zote imeendelea kutolewa kupitia vyombo vya habari kila robo mwaka.
- Spika, taarifa ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (Controller and Auditor General – CAG) kuhusu Hesabu za Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa mwaka wa fedha 2020/21 imebainisha Halmashauri 178 sawa na asilimia 96 zimepata Hati Safi, Halmashauri 6 sawa na asilimia 3 zimepata Hati Zenye Shaka na Halmashauri 1 sawa na asilimia 1 imepata Hati Mbaya.
- Spika, matokeo ya ukaguzi wa hesabu za mwaka wa fedha 2020/21 yanaonesha mwenendo mzuri wa aina ya Hati za Ukaguzi zilizotolewa ikilinganishwa na ukaguzi wa hesabu za mwaka wa fedha wa 2019/20 ambapo Halmashauri zilizopata Hati Safi zilikuwa 124 sawa na asilimia 67, Halmashauri zilizopata Hati Zenye Shaka zilikuwa 53 sawa na asilimia 29 na Halmashauri zilizopata Hati Mbaya zilikuwa 8 sawa na asilimia 4.
- Spika, matokeo hayo mazuri yametokana na jitihada mbalimbali zilizofanywa na Serikali, Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa (USEMI) na wadau wengine katika kuhakikisha kuwa changamoto zilizojitokeza katika ukaguzi uliotangulia wa mwaka wa fedha 2019/20 zinafanyiwa kazi kama ilivyoshauriwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.
- Spika, kuhusu hatua zinazochukuliwa dhidi ya vitendo vya matumizi mabaya ya fedha za umma kwenye baadhi ya Halmashauri ni kwamba, Ofisi ya Rais – TAMISEMI imekuwa ikiratibu na kusimamia uchukuaji wa hatua stahiki za kinidhamu na kisheria kwa Watumishi, Wakandarasi, Wahandisi Washauri na Wazabuni wengine ambao wamekuwa wakibainishwa kwenye taarifa za ukaguzi kujihusisha na vitendo vya ubadhirifu wa fedha za umma.
- hadi Februari 2022, Ofisi ya Rais – TAMISEMI imepokea na kuchambua taarifa za ukaguzi maalum uliofanywa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwenye Halmashauri 64. Ofisi za Wakuu wa Mikoa zimeelekezwa kusimamia uchukuaji wa hatua stahiki za kinidhamu kwa watumishi zaidi ya 1,000 waliotajwa kuhusika na kasoro mbalimbali zilizobainishwa kwenye taarifa hizo.
- Spika, Ofisi ya Rais – TAMISEMI tayari imewasiliana na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) ili izifanyie kazi taarifa hizo kwenye maeneo yanayohusu ubadhirifu wa fedha na mali za Halmashauri. Vile vile, Ofisi ya Rais – TAMISEMI inakamilisha uchambuzi wa Wakandarasi na Wahandisi Washauri wote waliotajwa kwenye taarifa za ukaguzi ili wafikishwe kwenye Bodi ya Usajili wa Wahandisi (ERB) na Bodi ya Usajili wa Makandarasi (CRB) kwa hatua stahiki kufuatia ukiukaji wa maadili ya taaluma zao.
Matumizi ya Fedha za Mfuko wa Jimbo
- Spika, katika Mwaka wa Fedha 2021/22 Ofisi ya Rais –TAMISEMI iliidhinishiwa Shilingi bilioni 11.00 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika Majimbo ya Uchaguzi 214 ya Tanzania Bara. Hadi Februari, 2022 fedha zote zilizokuwa zimeiidhinishwa zilikuwa zimetolewa sawa na asilimia 100. Fedha za Mfuko wa Jimbo zimeelekezwa katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo iliyoanzishwa kwa nguvu za Wananchi ikiwa ni pamoja na ukamilishaji wa ujenzi wa miundombinu ya kutolea huduma za kijamii hususan katika sekta ya afya na elimu.
Matumizi ya Mifumo ya TEHAMA
- Spika, Ofisi ya Rais – TAMISEMI imeendelea kuimarisha mifumo ya kielektroniki na miundombinu ya TEHAMA kwenye Mikoa, Mamlaka za Serikali za Mitaa, Taasisi zilizo chini yake na vituo vya kutolea huduma ambayo imeongeza ufanisi na uwajibikaji. Mifumo mbalimbali imefanyiwa usanifu na kusimikwa kwenye maeneo ya kutolea huduma nchini.
- Spika, Mifumo iliyosanifiwa na kusimikwa na Ofisi ya Rais – TAMISEMI ni pamoja na Mfumo wa Kuandaa Mipango, Bajeti na Utoaji wa Taarifa (PlanRep); Mfumo wa Ukusanyaji wa Mapato ya Ndani katika Mamlaka za Serikali za Mitaa (LGRCIS); Mfumo wa Usimamizi wa Fedha na Utoaji wa Taarifa za Kihasibu (FFARS); Mfumo wa Usimamizi na Uendeshaji wa Vituo vya Kutolea Huduma za Afya (GoTHOMIS) na Mfumo wa Takwimu za Elimumsingi (BEMIS). Aidha, Ofisi ya Rais – TAMISEMI inaendelea kukamilisha Mfumo wa Mikopo ya asilimia Kumi (10% LMIS) ambao utapunguza changamoto zilizopo.
- Spika, mifumo mingine inayosimamiwa na Ofisi ya Rais-TAMISEMI ni Mfumo wa Maombi ya Ajira TAMISEMI; Mfumo wa Tovuti za Serikali (GWF); Kituo cha Kutoa Huduma kwa Wananachi (Call Centre), Mfumo Jumuishi wa Ufuatiliaji na Tathmini (iMES) na Mfuko wa Afya ya Jamii Uliyoboreshwa (iCHF). Matumizi ya mifumo hii imeiwezesha Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kutoa huduma kwa wakati na ufanisi.
- Spika, hadi Februari, 2022 mifumo imefanyiwa maboresho ili kuongeza ufanisi katika Mipango na Bajeti na ukusanyaji na usimamizi wa fedha katika Mamlaka za Serikali za Mitaa ni pamoja na Mfumo wa Kuandaa Mipango, Bajeti na Utoaji Wa Taarifa (PlanRep); na Mfumo wa Usimamizi wa Fedha na Utoaji wa Taarifa za Kihasibu (FFARS). Mifumo hii imeboreshwa ili kuwezesha Kata, Vijiji na Mitaa kupanga mipango na bajeti na kufanya matumizi.
- Spika, katika kuhakikisha Wizara na Idara za Serikali zinashirikiana na kupunguza wingi wa mifumo, Mfumo wa PlanRep unaboreshwa ili kuweza kuanza kutumika katika kupanga Mipango na Bajeti Tanzania Bara na Visiwani. Vilevile, mfumo huu unatumika katika Taasisi 236 zinazosimamiwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina.
Ujenzi wa Majengo ya Ofisi za Wakuu wa Mikoa, Wilaya na Tarafa
- Spika, katika Mwaka wa Fedha 2021/22 Ofisi za Wakuu wa Mikoa ziliidhinishiwa jumla ya Shilingi bilioni 31.72 kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa Ofisi za Wakuu wa Mikoa, Ofisi za Wakuu wa Wilaya na Ofisi za Maafisa Tarafa. Hadi Februari, 2022 jumla ya Shilingi bilioni 16.50 sawa na asilimia 52.01 ya bajeti iliyoidhinishwa na utekelezaji wa miradi hiyo upo katika hatua mbalimbali.
Ujenzi wa Nyumba za Viongozi katika Tawala za Mikoa
- katika Mwaka wa Fedha 2021/22 Ofisi za Wakuu wa Mikoa ziliidhinishiwa jumla ya Shilingi bilioni 21.65 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za makazi za Viongozi katika Mikoa na Wilaya. Kati ya fedha hizo, Shilingi bilioni 2.89 ziliidhinishwa kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa nyumba za Wakuu wa Mikoa 12 ya; Arusha, Dar es Salaam, Kagera, Iringa, Geita, Katavi, Manyara, Mtwara, Njombe, Rukwa, Ruvuma na Shinyanga. Aidha, Shilingi bilioni 8.71 ni kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa nyumba za Wakuu wa Wilaya 39, Shilingi bilioni 10.05 kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa nyumba 11 za Makatibu Tawala wa Mikoa, Makatibu Tawala Wasaidizi 11, Makatibu Tawala wa Wilaya 26, Ikulu Ndogo sita (6) na Maafisa Tarafa 19.
- kufikia Februari, 2022 jumla ya Shilingi bilioni 9.13 zimetolewa sawa na asilimia 42.17 ya fedha zilizoidhinishwa. Kati ya fedha hizo Shilingi bilioni 4.20 kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa nyumba za Wakuu wa Mikoa 12 na nyumba za Wakuu wa Wilaya 39. Vilevile,Shilingi bilioni 4.93 nikwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa nyumba 11 za Makatibu Tawala wa Mikoa, Makatibu Tawala Wasaidizi 11, Makatibu Tawala wa Wilaya 26, Ikulu Ndogo sita (6) na Maafisa Tarafa 19.
Ujenzi wa majengo ya Utawala katika Halmashauri
- Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha 2021/22 jumla ya Shilingi bilioni 85.22 ziliidhinishwa kwa ajili ya ujenzi wa majengo ya utawala 90. Hadi Februari, 2022 jumla ya Shilingi bilioni 64.42 sawa na asilimia 75.59 zimetolewa kwa ajili ya kuendelea na ujenzi pamoja na ukamilishaji wa majengo ya utawala ambapo jumla ya majengo 12 yamefikia asilimia 90 ya ujenzi, majengo 9 yamefikia asilimia 80 na mengine yapo katika hatua mbalimbali za ukamilishaji. (Kiambatisho Na. 12)
- Mheshimiwa Spika, majengo hayo yapo katika hatua mbalimbali za ujenzi ambapo majengo sita (6) ya Halmashauri za Wilaya za Mkalama, Malinyi, Madaba, Itilima, Wanging’ombe na Chalinze yamekamilika na yanatumika, Majengo saba (7) ya Halmashauri za Wilaya za Songwe, Misungwi, Kakonko, Nsimbo, Pangani, Chamwino na Mji Geita yanaendelea na ujenzi. Aidha, majengo nane (8) yapo katika hatua za ukamilishaji. Majengo 61 yapo katika hatua mbalimbali za ujenzi ikiwemo kuta, usimikaji wa nguzo na hatua za msingi.
- Mheshimiwa Spika, ujenzi wa majengo 12 ya utawala katika Halmashauri za Wilaya za Nzega, Kigoma, Kwimba, Ulanga, Kisarawe, Kilwa, Kongwa, Ukerewe pamoja na Manispaa za Moshi na Shinyanga haujaanza kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo Halmashauri kuchelewa kukubaliana eneo la ujenzi. Halmashauri zilizokuwa na changamoto hii ni Halmashauri za Wilaya za Kigoma, Nzega na Kisarawe. Aidha, kwa sasa makubaliano yamefikiwa na ujenzi upo katika hatua za awali za kusafisha eneo na kupima udongo.
Ujenzi wa Nyumba za Viongozi katika Mamlaka za Serikali za Mitaa
- Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha 2021/22 jumla ya Shilingi bilioni 10.60 ziliidhinishwa kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za Wakurugenzi na Wakuu wa Idara. Hadi Februari, 2022 jumla ya Shilingi bilioni 6.55 sawa na asilimia 61.79 zimetolewa kwa ajili ya kuendelea na ujenzi wa nyumba hizo 106 (Rejea Kiambatisho Na. 12).
- Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha 2021/22 Ofisi ya Rais- TAMISEMI iliidhinishiwa Shilingi bilioni 12.58 kwa ajili ya ununuzi wa magari 70 ya Wakurugenzi na Wakuu wa Idara wa Mamlaka za Serikali za Mitaa nchini. Hadi Februari 2022 jumla ya Shilingi milioni 801 zimepokelewa sawa na asilimia 6.52 na taratibu za manunuzi zinaendelea. Aidha, kufuatia maelekezo ya Serikali magari mengine yaliyobaki utaratibu wa manunuzi unaendelea na magari hayo yatanunuliwa kwa pamoja.
- Spika, katika Mwaka wa Fedha 2021/22 Ofisi ya Rais- TAMISEMI iliidhinishiwa Shilingi bilioni 3.88 kwa ajili ya ununuzi wa magari 14 kwa ajili ya Viongozi wa Tawala za Mikoa. Hadi Februari, 2022 zimepokelewa Shilingi milioni 900.00 kwa ajili ya ununuzi wa magari matatu (3) Ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma na Makatibu Tawala wa Mikoa ya Mbeya na Pwani na taratibu za ununuzi wa magari hayo zinaendelea.
Huduma za Kiuchumi na Uzalishaji
- Mheshimiwa Spika, Ofisi ya Rais – TAMISEMI kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo na Wadau mbalimbali imeendelea kuratibu huduma za ugani. Hadi Februari 2022, jumla ya mashamba darasa 116 yameandaliwa katika Mikoa ya Katavi, Dar es salaam, Mwanza, Simiyu, Tabora, Rukwa, Iringa, Morogoro, Arusha, Geita na Songwe ili kutoa elimu kwa vitendo kwa wakulima kuhusu mbinu bora za kilimo kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa.
- Ofisi ya Rais TAMISEMI kwa kushirikiana na Taasisi ya AGRA imekamilisha kuandaa Mipango ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa 37 kwenye Mikoa 12 ikiainisha maeneo ya kipaumbele kwenye sekta za kilimo-mazao, mifugo na uvuvi. Wizara yangu itaendelea kushirikiana na Wizara za Kisekta na Washirika wengine wa Maendeleo katika kuhakikisha kuwa rasilimali fedha zinapatikana ili kuwezesha utekelezaji wa afua hizo.
Maliasili na Mazingira
- Mheshimiwa Spika, Ofisi ya Rais-TAMISEMI imeendelea kuratibu na kusimamia utekelezaji wa Sera na mikakati mbalimbali ya kuhifadhi maliasili na usimamizi wa mazingira katika ngazi ya Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa kushirikiana na Wadau mbalimbali. Hadi Februari, 2022 Ofisi ya Rais – TAMISEMI imeratibu na kusimamia shughuli za upandaji miti ambapo jumla ya miti milioni 127.5 imepandwa kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa.
- Mheshimiwa Spika, sambamba na jitihada za upandaji miti, wananchi wamekuwa wakihimizwa kutunza misitu ya asili kwa ajili ya kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi na uuzaji wa hewa ukaa. Biashara ya hewa ukaa imeanza katika Mkoa wa Katavi katika Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika. Hadi Februari, 2022 jumla ya tani 403,500 zimeuzwa kwa Shilingi bilioni 2.30 ambapo jumla ya wananchi 21,000 katika vijiji nane (8) kutoka katika Halmashauri Wilaya ya Tanganyika wamenufaika na biashara ya hewa ukaa.
- Mheshimiwa Spika, Ofisi ya Rais – TAMISEMI kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mitaji ya Maendeleo (United Nation Capital Development Fund-UNCDF) imewajengea uwezo wananchi kuhusu kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi. Hadi Februari, 2022 jumla ya Shilingi milioni 413.88 zimetolewa kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa kusaidia jamii kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi katika Halmashauri za Wilaya ya Chamwino, Kondoa na Mpwapwa katika Mkoa wa Dodoma.
- Mheshimiwa Spika, Ofisi ya Rais – TAMISEMI imeendelea kuzisimamia Mamlaka za Serikali za Mitaa katika kuhakikisha zinatenga maeneo kwa ajili ya shughuli mbalimbali za uzalishaji. Hadi Februari, 2022 jumla ya hekta 7,186,312.44 zimetengwa kwa ajili ya shughuli mbalimbali ikiwemo hekta 175,951.19 kwa ajili ya uwekezaji wa viwanda, hekta 3,003,352.03 kwa ajili ya malisho ya mifugo, hekta 261,897.30 kwa ajili ya machimbo ya madini, hekta 29,644.79 kwa ajili ya biashara za aina mbalimbali na hekta 3,715,467.13 kwa ajili ya kilimo.
- , Serikali imekuwa ikifanya kazi na Asasi za Kiraia katika kuboresha huduma kwa jamii ambapo hadi Februari, 2022, Ofisi ya Rais TAMISEMI imeratibu AZAKI 265 kwa kutoa vibali ili zikatekeleze majukumu yake kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu zilizopo katika Mamlaka za Serikali za Mitaa kwenye Mikoa mbalimbali nchini.
- Mheshimiwa Spika, Ofisi ya Rais – TAMISEMI imefanya ufuatiliaji wa shughuli za Wadau hao katika Mikoa ya Mara, Kilimanjaro, Arusha, Manyara, Dodoma, Morogoro, Mwanza, Kagera, Tabora, Tanga, Iringa, Njombe, Mbeya, Songwe, Rukwa na Katavi. Miradi iliyotembelewa ni ya Kilimo, Ufugaji, Ujasiliamali Utunzaji wa Mazingira, Maji na Usafi wa Mazingira. Ofisi ya Rais – TAMISEMI inazipongeza AZAKI zote kwa namna zinavyotoa ushirikiano katika uboreshaji wa huduma kwa jamii.
Uendelezaji wa Miji na Vijiji
- Mheshimiwa Spika, Ofisi ya Rais – TAMISEMI imeendelea kushirikiana na Wizara za Kisekta katika kuandaa na kutekeleza mipango ya Uendelezaji wa Vijiji na Miji nchini. Hadi Februari, 2022. Mipango kabambe imekamilika na kusajiliwa kwa Majiji 5 ya Arusha, Mwanza, Dodoma, Tanga na Mbeya; Manispaa 14 za Ilemela, Kigoma – Ujiji, Mtwara – Mikindani, Lindi, Songea, Iringa, Morogoro, Singida, Tabora, Bukoba, Musoma, Mpanda, Sumbawanga na Shinyanga na Miji 6 ya Babati, Njombe, Geita, Korogwe, Kibaha na Bariadi. Aidha, Ofisi ya Rais TAMISEMI inaendelea kuandaa Mipango Kabambe kwa Halmashauri zilizobakia.
- Spika, Ofisi ya Rais-TAMISEMI kwa kushirikiana na Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari imeendelea kubainisha majina ya mitaa, njia na barabara, kusimamia ukusanyaji wa taarifa za nyumba, wakazi na makazi na uwekaji wa miundombinu kwenye majengo na barabara kwa kuwashirikisha wananchi wenyewe kwenye maeneo yao. Utekelezaji wa kazi hizo ni sehemu ya utekelezaji wa Mpango wa Anwani za Makazi ambao utatumika wakati wa zoezi la Sensa ya Watu na Makazi linalotarajiwa kufanyika Agosti, 2022.
UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA TAASISI ZILIZO CHINI YA OFISI YA RAIS – TAMISEMI
- Mheshimiwa Spika, Ofisi ya Rais-TAMISEMI inasimamia Taasisi Saba (7) ambazo ni Chuo Cha Serikali za Mitaa (LGTI), Shirika la Elimu Kibaha (KEC), Shirika la Masoko ya Kariakoo (KMC), Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka Dar es Salaam (DART), Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA), Bodi ya Mikopo ya Serikali za Mitaa (LGLB) na Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC). Aidha, utekelezaji uliofanyika katika Mwaka wa Fedha 2021/22 hadi Februari, 2022 kwa kila taasisi ni kama ifuatavyo: –
Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA)
- Mheshimiwa Spika, mtandao wa barabara chini ya TARURA una jumla ya kilomita 144,429.77 ambazo zimetangazwa rasmi kwenye Gazeti la Serikali Na. 463 la tarehe 25 Juni 2021. Mtandao wa barabara unaosimamiwa na TARURA una jumla ya madaraja 3,191, makalavati 69,317, barabara za lami zenye urefu wa kilomita 2,473.55, barabara za Changarawe zenye urefu wa kilomita 30,756.51 na barabara za udongo zenye urefu wa kilomita 111,199.72.
- Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha 2021/22 TARURA iliidhinishiwa jumla ya Shilingi bilioni 900.45 kwa ajili ya ujenzi, matengenezo na ukarabati wa miundombinu ya barabara za Wilaya, kati ya fedha hizo Shilingi bilioni 722.16 ni fedha za ndani na Shilingi bilioni 178.29 ni fedha za nje. Fedha za ndani Shilingi bilioni 722.16 zinajumuisha Shilingi bilioni 272.50 kutokana nafedha za Mfuko wa Barabara, Shilingi bilioni 322.16 kutokana natozo ya mafuta ya Shilingi 100 kwa kila lita ya mafuta ya petroli/diseli na Shilingi bilioni 127.50 kupitia Mfuko Mkuu wa Serikali.
- Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha 2021/22, TARURA ilipanga kujenga barabara za lami zenye urefu wa kilomita 232.94, changarawe kilomita 13,727.76, madaraja 736, na utunzaji wa barabara kilomita 22,202.84. Hadi Februari 2022, Shilingi bilioni 461.75 zimepokelewa na kukamilisha ujenzi wa barabara za lami zenye urefu wa kilomita 129.02, changarawe kilomita 1,198.78, madaraja 181, na matengenezo ya barabara kilomita 19,257.76.
Ujenzi wa Barabara katika Mji wa Serikali Mtumba
- Mheshimiwa Spika, TARURA inaendelea na ujenzi wa barabara kilomita 51.2 kwa kiwango cha lami katika Mji wa Serikali Mtumba, mradi huo ulianza kutekelezwa katika Mwaka wa Fedha 2019/20 kwa gharama ya Shilingi bilioni 89.13. Mradi umekamilika kwa asilimia 90 na hadi Februari 2022, malipo ya Shilingi bilioni 76.16 yamefanyika. Kazi zilizokamilika ni pamoja na Ujenzi wa barabara za lami zenye urefu wa kilomita 51.2, taa za barabarani 196 na ujenzi wa mifereji ya maji ya mvua kilomita 62.8. Aidha, Wakala unaendelea na ukamilishaji wa kazi ndogo ndogo zilizobakia.
Mradi wa Uboreshaji Miundombinu katika Jiji la Dar es Salaam (DMDP)
- Mheshimiwa Spika, katika mradi wa DMDP Serikali imetoa jumla ya Shilingi bilioni 83.11 kwa ajili ya ukamilishaji wa ujenzi wa barabara zenye urefu wa kilomita 16 kwa kiwango cha lami na ujenzi wa mifereji ya Maji ya mvua kilomita 17.9 katika Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, Temeke na Jiji la Dar es Salaam; Ununuzi wa magari 20 ya kusomba taka ngumu pamoja na vyombo 65 vya kukusanyia taka (skip bucket). Hadi Februari, 2022, ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami kilomita 5.39, mifereji ya maji ya mvua kilomita 4.75 imekamilika pamoja na soko la Mtoni Kijichi katika Halmashauri ya Manispaa ya Temeke.
Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka,
Dar es Salaam
- Mheshimiwa Spika, hadi Februari, 2022 Wakala umefanya mapitio ya mtandao wa usafiri kwa kuongeza barabara za Kimara hadi Kibamba kilomita 13.7 na Mbagala Rangi Tatu hadi Vikindu kilomita 4.5 ambazo zimejumuishwa kwenye awamu ya sita ya mradi na hivyo kuwa na mtandao wa barabara zenye jumla ya urefu wa kilomita 154.4.
- Mheshimiwa Spika, pamoja na mtandao huo wa barabara, jumla ya vituo vikuu vipatavyo 24 vitahitajika. Aidha, mpango huu mpya umeainisha maeneo 14 kwa ajili ya kujenga karakana zitakazohitaji kuhudumia awamu zote sita (6) za mradi. Tayari maeneo yote haya yameainishwa na kuingizwa kwenye mpango wa utwaaji wa maeneo ya mradi.
- Mheshimiwa Spika, Wakala umefanya Tathmini ya mahitaji ya usafiri wa umma katika Mkoa wa Dar es Salaam ambayo imeonesha kuongezeka kwa mahitaji ya usafiri wa umma ambapo hadi mwaka 2025 kutakuwepo na watumiaji wa usafiri wa umma 2,590,000 kwa siku ambapo kutahitajika jumla ya mabasi 1,975. Kati ya mabasi hayo, mabasi 695 ni yenye urefu wa mita 18 na mabasi 1,280 ni yenye urefu wa mita 12.
- Mheshimiwa Spika, Mradi wa DART awamu ya pili unatekelezwa kupitia ufadhili wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) kwa kiasi cha Dola za Kimarekani milioni 141.71. Serikali imelipa fidia ya Shilingi bilioni 30.25 kwa wananchi 92 ambao maeneo yao yaliathiriwa na utekelezaji wa mradi huu. Aidha, kwa kazi za barabara zimepangwa kutekelezwa kwa muda wa miaka mitatu (3) kwa gharama ya Shilingi bilioni 217.48. Ujenzi ulianza rasmi mwezi Mei, 2019 na umefikia asilimia 48 ambapo unatarajia kukamilika ifikapo Machi, 2023.
- Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha 2021/22 Wakala umeendelea na Awamu ya Pili ya ujenzi wa miundombinu ya Mabasi Yaendayo Haraka katika Mkoa wa Dar es Salaam ambapo miradi inayohusika ni ujenzi kuanzia Mjini Kati hadi Mbagala Rangitatu na kutoka Mgulani hadi Magomeni kupitia Chang’ombe na Kawawa barabara yenye urefu wa kilomita 20.3. Kazi nyingine zinazoendelea kutekelezwa katika awamu hii ni ujenzi wa vituo 28 vya mabasi, karakana moja (1) na madaraja ya juu mawili katika barabara za Kilwa na Mandela na makutano ya barabara ya Chang’ombe na Nyerere, vituo mlisho vinne (4), vituo vikuu viwili (2) katika eneo la Mbagala Rangitatu na Gerezani Kariakoo na daraja moja (1) katika eneo la BP.
- Spika, Ofisi ya Rais – TAMISEMI kwa kushirikiana na Wizara ya Fedha na Mipangona Wakala waSerikali Mtandao unatengeneza mfumo wa kielektroniki wa kukusanya nauli. Kazi hiyo inaendelea na mfumo umeanza kufanya kazi ambapo mpaka sasa vituo ishirini (20) vya DART vinatumia mfumo mpya vikiwemo vituo vikuu vyote, na vingine vitakamilisha kuwekewa mfumo huo mwezi Juni 2022, baada ya kukamilisha ununuzi wa vifaa.
Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC)
- Spika, Dhima ya Tume ya Utumishi wa Walimu ni kuhakikisha walimu wa Shule za Msingi na Sekondari Tanzania bara wanapata huduma bora kuhusu masuala ya ajira, kupandishwa vyeo na kukuza maadili katika Utumishi wa walimu. Katika kutekeleza Dhima hiyo, walimu 6,949 kati yao walimu 3,949 wa Shule za Msingina walimu 3,000 wa Shule za Sekondari walioajiriwa mwezi Juni, 2021 walisajiliwa na kupewa namba za TSC,Walimu 591 walipewa vibali vya kustaafu, mikutano 223 ya Kisheria imefanyika kati ya mikutano 278 iliyopangwa kufanyika kwa mwaka.
- katika mikutano hiyo ya kisheria iliyofanyika, Walimu 1,872 walipandishwa vyeo ambapo walimu 914 wa shule za msingi na 958 wa shule za sekondari; walimu 222 walithibitishwa kazini na walimu 460 walibadilishiwa vyeo. Vilevile, mashauri ya kinidhamu ya walimu 642 kati ya 793 yalihitimishwa, na mashauri ya walimu 151 yapo katika hatua mbalimbali za ukamilishaji. Aidha, hadi Februari, 2022 rufaa za walimu 147 kati ya rufaa 152 zilitolewa uamuzi na Tume. Pia, malalamiko ya walimu 405 kuhusu upandishwaji vyeo, ubadilishwaji vyeo na mashauri ya kinidhamu yalipokelewa na kushughulikiwa.
- , Tume ya Utumishi wa Walimu imeanza kutekeleza ujenzi wa Ofisi ya Makao Makuu katika eneo la Njedengwa, Dodoma utakaogharimu Shilingi bilioni 3.86 hadi kukamilika.Katika Mwaka wa Fedha 2021/22 jumla ya Shilingi milioni 500 ziliidhinishwa. Hadi Februari 2022, Shilingi milioni 500 zimepokelewa sawa na asilimia 100 ya fedha zilizoidhinishwa kwa mwaka husika ambapo kati ya fedha hizo, Shilingi milioni 386 zimetumika kumlipa Mkandarasi SUMA – JKT ikiwa ni malipo ya awali na kazi imeanza.
- , Tume ya Utumishi wa Walimu katika kutekeleza majukumu yake imekuwa ikikabiliana na changamoto mbalimbali za walimu ikiwemo: upungufu wa walimu 100,958 wa shule za msingi na walimu 74,743 wa shule za sekondari hususan masomo ya sayansi; malalamiko ya walimu ikiwemo kutopandishwa vyeo kwa wakati; na wastaafu kucheleweshewa kulipwa stahili na mafao yao baada ya kustaafu.
- , katika kushughulika kero za wastaafu, Tume ya Utumishi wa Walimu imeanzisha dawati maalumu la kupokea malalamiko na kero za wastaafu. Aidha, Tume inaendelea na ujenzi wa Mfumo wa Kielektroniki wa Usimamizi wa Masuala ya Walimu (Teachers Service Commission Management Information System -TSC-MIS) ambao utasaidia kurahisisha utoaji wa huduma kwa walimu.
- ,Tume ya Utumishi wa Walimu imesaidia kupunguza kero na malalamiko ya walimu nchini ambapo tathmini iliyofanywa imeonesha kwamba asilimia 69 ya wadau hasa walimu wanaridhishwa na huduma zinatolewa na Tume ya Utumishi wa Walimu. Aidha, ajira za walimu zimepanda kutoka 10,629 mwaka wa fedha 2018/19 hadi kufika 14,949 mwaka wa fedha 2020/21 sawa na asilimia 40.66.Vilevile, Kamati za Wilaya 139 za Tume ya Utumishi wa Walimuzimejengewa uwezo ili ziweze kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi katika mwaka 2021/22.
Shirika la Elimu Kibaha
- , katika Mwaka wa Fedha 2021/2022 Shirika la Elimu Kibaha limeendelea kuwa mstari wa mbele katika kutimiza malengo ya kuanzishwa kwake ambayo ni kupambana na maadui watatu wa maendeleo yaani Maradhi, Ujinga na Umaskini. Hadi Februari, 2022, Elimu ya Kinga na tiba kupitia Hospitali Teule ya Rufaa ya Mkoa Pwani (Tumbi) ilitolewa kwa wagonjwa wa nje 60,867 sawa na wastani wa wagonjwa 338 kwa siku ambao ni asilimia 68 ya malengo, kati ya idadi hiyo, wazazi wa watoto chini ya umri wa miaka mitano walikuwa 10,064.
- Spika, Shirika limeendelea kusimamia utoaji wa huduma za afya ambapo hadi Februari, 2022 wagonjwa 4,264 walilazwa ikiwa ni pamoja na watoto chini ya umri wa miaka mitano 491 na watoto wachanga 641. Vilevile, huduma kwa wazazi waliojifungua kawaida walikuwa 452, waliojifungua kwa njia ya upasuaji walikuwa 582 na wazazi 3 walipoteza maisha wakati wa kujifungua kutokana na kupoteza damu nyingi.
- Spika, Hospitali pia imeendelea kutoa huduma kwa waraibu wa madawa ya kulevya ambapo kuanzia Julai 2021 hadi Februari, 2022 waraibu 273 wamesajiliwa na wanaendelea na tiba. Aidha, katika kipindi hicho, jumla ya majeruhi 810 wa ajali za barabarani walihudumiwa.
- Spika, katika Mwaka wa Fedha 2021/22, Shirika limeendelea kutoa Elimu ya utabibu na uuguzi kupitia Chuo cha Afya na Sayansi Shirikishi Kibaha kwa wanachuo 514. Aidha, huduma nyingine zinazotolewa katika Hospitali Teule ya Tumbi ni mafunzo tarajari ambapo madaktari 79, wauguzi 20 na wafamasia 10 wanaendelea na mafunzo.
- Spika, Hospitali Teule ya Tumbi ni miongoni mwa Hospitali za Rufaa za Mikoa, ambazo zimehamishiwa Wizara ya Afya kutokana na agizo la aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Awamu ya Tano alilolitoa tarehe 25 Novemba, 2017 ili kuimarisha utendaji na utoaji wa huduma bora za Afya kwa wananchi.
- Spika, katika Mwaka wa Fedha 2021/22 Shirika limeendelea kutoa Elimu kwa wanafunzi 3,013 wakiwemo wanafunzi 825 wa Shule ya Sekondari Kibaha, 819 Shule ya Sekondari Tumbi, 339 Shule ya Sekondari ya Wasichana Kibaha, 890 Shule ya Msingi Tumbi pamoja na watoto 140 wa elimu ya awali. Kwa mwaka wa masomo 2021 kuna ongezeko la wanafunzi 111 ikilinganishwa na wanafunzi wa mwaka wa masomo 2020 ambao walikuwa 2,902. Ongezeko hili limetokana na ujenzi wa vyumba vinne vya madarasa katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Kibaha na Shule ya Sekondari Tumbi ambapo vimejengwa vyumba viwili vya madarasa kwa kila shule.
- , katika Mwaka wa Fedha 2021/22 Shirika limeendelea kutoa mafunzo ya muda mrefu na mfupi ya nadharia na vitendo kupitia Chuo cha Maendeleo ya Wananchi kwa wanachuo 330 ambao wamesajiliwa (Wanaume 210 na Wanawake 120). Mafunzo yaliyotolewa ni Kilimo, Mifugo, Ujenzi, Ushonaji, Upishi, Ufundi wa Magari, Uundaji na Uungaji vyuma na Umeme wa majumbani. Katika mwaka wa masomo 2021/22, kuna ongezeko la wanachuo 38 ikilinganishwa na Mwaka wa Masomo 2020/21 ambapo walikuwa Wanachuo 292 kutokana na kuongeza wigo wa kukitangaza Chuo.
- , mafunzo mengine yaliyotolewa ni mafunzo ya muda mfupi kwa wahitaji 476 yakijumuisha udereva kwa wahitaji 68 ambapo wanaume ni 55 na wanawake 13, wanajamii 408 ambapo Wanaume ni 101 na wanawake 307 ambao walijengewa uwezo kupitia mafunzo ya Ujasiriamali, Elimu ya kifedha-Mikopo na Kilimo cha Bustani kwa njia ya matone. Mwaka 2020/21 walikuwa wanufaika 267 ambapo kwa Mwaka 2021/22 kuna wanufaika 476 sawa na ongezeko la wanufaika 209 kutokana na kuanza kutoa mafunzo kwa wanufaika wa mikopo inayotolewa na Halmashauri kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu Wenye Ulemavu.
Chuo Cha Serikali za Mitaa
- Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha 2021/22 Chuo cha Serikali za Mitaa kimeendelea kutekeleza kazi na majukumu yake yakiwemo mafunzo, utafiti na ushauri. Katika mwaka wa masomo 2021/22 Chuo kimedahili jumla ya wanafunzi 5,166 ambapo kati yao wanafunzi wa Astashada ya awali (National Technical Award 4) ni 1,930, Astashahada ya kati (National Technical Award 5) ni 1,925, Stashahada (National Technical Award 6) 1,997 na Shahada (National Technical Award 7-8) 214. Aidha, Chuo kimeendesha mafunzo katika programu kuanzia ngazi ya Astashahada mpaka Shahada ya kwanza. Programu hizo ni Utawala na Uongozi katika Serikali za Mitaa; Menejimenti ya Rasilimali watu, Maendeleo ya Jamii; Uhasibu na Fedha katika Serikali za Mitaa; Nyaraka na Utunzaji wa Kumbukumbu na Ununuzi na Ugavi.
- Mheshimiwa Spika, Chuo kimeendelea kutoa mafunzo ya muda mfupi ya kujenga uwezo kwa Halmashauri mbalimbali nchini. Hadi Februari, 2022 Chuo kimetoa mafunzo ya kuwajengea uwezo jumla ya Waheshimiwa Madiwani 482 wa Halmashauri 14 za Tanzania Bara zikijumuisha Halmashauri za Wilaya ya Bahi (27); Same (54); Meru (36); Karatu (27); Hai (27); Mbinga (27); Ushetu (27) na Buhigwe (27). Pia, mafunzo hayo yalijumuisha Halmashauri ya Mji Mbinga (25); Manispaa za Songea (27), Kinondoni (61) na Ilemela (27). Vilevile, mafunzo hayo yalijumuisha Halmashauri za Majiji ya Dar es Salaam (54) na Arusha (36). Nitumie fursa hii, kuwaelekeza Wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini kutumia Chuo hiki katika kuwajengea uwezo Waheshimiwa Madiwani, Watendaji na Viongozi wengine katika Halmashauri zao.
- Mheshimiwa Spika, Chuo kimeendesha mafunzo ya Mfumo wa Fursa na Vikwazo kwa Maendeleo Ulioboreshwa (Improved Oppotunities & Obstacles to Development – O&OD) kwa Halmashauri 184 nchini na mafunzo kwa Wenyeviti wa Mitaa 11 wa Manispaa ya Kinondoni kwa lengo la kuimarisha uwezo wa kutekeleza majukumu yao. Nitumie fursa hii tena, kuwaelekeza Wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini kutumia Chuo hiki katika kuwajengea uwezo Wenyeviti wa Mitaa na Vijiji katika Halmashauri zao.
- Mheshimiwa Spika, Chuo kimetoa mafunzo kwa viongozi na watendaji wa Halmashauri mbalimbali kwa kutumia Mfumo wa Ujifunzaji Kielektroniki (MUKI). Washiriki wa mafunzo hayo ni pamoja na Waheshimiwa Madiwani 757, watumishi wapya katika Mamlaka za Serikali za Mitaa 1,103, Watendaji wa Kata 8 na wasimamizi wa vituo vya kutolea huduma za Afya 25. Naendelea kuelekeza Wakurugenzi wa Halmashauri kuhakikisha wanatumia Mfumo huo kuwajengea uwezo viongozi na watendaji wa Halmashauri katika ngazi zote.
- Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha 2021/2022 chuo cha Serikali za Mitaa kimetekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo, ikiwemo ujenzi na ukamilishaji wa madarasa pacha ya wanafunzi 500 kwa gharama ya Shilingi milioni 500 na ukarabati wa majengo ya chuo uliogharimu Shilingi milioni 550 kwa kutumia fedha ya Mapato ya Ndani.
Bodi ya Mikopo ya Serikali za Mitaa
- Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha 2021/22 Bodi ya Mikopo ya Serikali za Mitaa imetoa mikopo ya Shilingi milioni 300 kwa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe kwa ajili ya ujenzi wa vibanda vya biashara vinavyozunguka Kituo cha Mabasi katika Makao Makuu ya Halmashauri.Hadi Februari 2022, Bodi imeratibu urejeshwaji wa mikopo jumla ya Shilingi milioni 147.00 kutoka katika Halmashauri. Vilevile, Bodi imeendelea kukusanya michango ya akiba na nyongeza ya mtaji ambapo kiasi cha Shilingi milioni 83.50 kimekusanywa kuanzia Julai 2021 hadi Februari 2022. Nachukua fursa hii kuziagiza Halmashauri zote zilizokopa kurejesha Mikopo yake kama ilivyo kwenye Mikataba yao na kuchangia Michango yao ya Akiba kwa Mujibu wa Sheria.
Shirika la Masoko ya Kariakoo
- Mheshimiwa Spika, Shirika la Masoko Kariakoo lilianzishwa kwa Sheria ya Bunge Na. 36 ya Mwaka 1974 kwa lengo la kusimamia na kuendesha masoko ya mazao ya chakula, zana za kilimo na pembejeo za kilimo katika Mkoa wa Dar es salaam. Tarehe 07 Julai, 2021 kulitokea ajali ya moto katika jengo kuu la Shirika la Masoko ya Kariakoo. Moto huo uliteketeza bidhaa zote za wafanyabiashara 224 ambapo kati yao 120 walikuwa wanaendesha biashara zao katika ghorofa ya chini, wafanyabiashara 100 katika ghorofa ya kwanza na wafanyabiashara wanne (4) maeneo ya matangazo. Naomba kutumia fursa hii kutoa pole kwa wafanyabiashara wote waliopoteza mali zao katika janga hilo la moto. Aidha, ajali hiyo iliteketeza mali zote za Shirika ambazo ni Ofisi 31, samani, vifaa na nyaraka zote za kumbukumbu.
- Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa tathmini iliyofanywa na Kampuni ya Ushauri ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (BICO) imebaini kuwa Jengo halikuathirika kiasi cha kutoweza kukarabatiwa. Katika Mwaka wa Fedha 2021/22 Serikali imetenga Shilingi bilioni 26.28 kwa ajili ya ukarabati wa jego lililoungua na ujenzi wa soko jipya. Hadi Februari, 2022 ukarabati wa soko lililoungua umefikia asilimia 40 na ujenzi wa soko jipya umefikia asilimia 15. Aidha, fedha zilizotolewa na kulipwa kwa Mkandarasi ESTIM CONSTRUCTION ikiwa ni malipo ya awali ni Shilingi bilioni 3.94 na mradi unategemewa kukamilika mwezi Oktoba, 2023. Baada ya mradi kukamilika jumla ya wafanyabiashara 2,313 wataweza kupata nafasi za biashara ikilinganishwa na wafanyabiashara 1,598 waliokuwepo kabla ya soko kuungua ikiwa ni ongezeko la wafanya biashara 715.
- Mheshimiwa Spika, natoa shukrani zangu za dhati kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimwa Samia Suluhu Hassan, kwa kusikia kilio cha wafanyabiashara wa Soko la Kariakoo waliokuwa wanafanya biashara mbalimbali katika soko hilo ambalo linahudumia wakazi wa Jiji la Dar es Salaam, Mikoa mingine na wafanyabiashara kutoka nchi za jirani kwa kutoa fedha za ujenzi wa soko jipya na kukarabati soko lililoungua.
- MPANGO NA BAJETI YA MATUMIZI YA KAWAIDA NA MAENDELEO KWA MWAKA WA FEDHA 2022/23 KWA OFISI YA RAIS – TAMISEMI (FUNGU 56), TUME YA UTUMISHI WA WALIMU (FUNGU NA. 2) NA MAFUNGU 26 YA MIKOA IKIJUMUISHA MAMLAKA ZA SERIKALI ZA MITAA 184
- Mheshimiwa Spika, Mpango na Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2022/23 umeandaliwa kwa kuzingatia Malengo ya Maendeleo Endelevu 2030, Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025, Mpango wa Tatu wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2021/22-2025/26), Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi ya Mwaka 2020, Hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Awamu ya Sita, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, aliyoitoa katika Bunge la 12 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mwongozo wa Kuandaa Mpango na Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2022/23, maelekezo ya Viongozi wengine wa Kitaifa, Sera za Kisekta, Miongozo ya Serikali na Mipango Mikakati iliyohuishwa ya Ofisi ya Rais-TAMISEMI Fungu 56, Tume ya Utumishi wa Walimu Fungu Na. 2 na Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa Mafungu 26 kwa kipindi cha 2021/22-2025/26.
- Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha 2022/23, Ofisi ya Rais-TAMISEMI imepanga kutekeleza Mipango na Bajeti kwa kuzingatia vipaumbele vifuatavyo: –
- Kuratibu na kusimamia utekelezaji wa shughuli za utoaji wa Elimumsingi katika Mamlaka za Serikali za Mitaa ikijumuisha utekelezaji wa Elimumsingi Bila Malipo;
- Kuratibu na kusimamia Mkakati wa kuongeza ukusanyaji wa mapato na kudhibiti matumizi katika Mamlaka za Serikali za Mitaa;
- Kuratibu na kusimamia utekelezaji wa shughuli za utoaji wa Huduma za Afya ya Msingi, Lishe na Ustawi wa Jamii katika Mamlaka za Serikali za Mitaa;
- Kushughulikia malalamiko ya walimu ikiwemo kutopandishwa vyeo kwa wakati; na wastaafu kucheleweshewa kulipwa stahili na mafao yao baada ya kustaafu ambapo Tume ya Utumishi wa Walimu imeanzisha dawati maalumu la kupokea malalamiko na kero za wastaafu;
- Kuchochea na kuhimiza ukuaji wa uchumi shindani kwa maendeleo ya wananchi na Taifa kwa ujumla kwa kuiwezesha Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kuweka mazingira mazuri ya biashara na uwekezaji, hasa katika Kilimo, Mifugo na Viwanda. Utekelezaji wa jambo hili utahusisha uimarishaji wa sehemu ya uchumi na uzalishaji katika ngazi ya Mikoa kwa kuhakikisha kuna rasilimali watu wenye weledi pamoja uwepo wa fedha na vitendea kazi. Aidha, Serikali itaendelea kuboresha mazingira ya utendaji kazi kwa maafisa ugani katika Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa kushirikiana na Wizara za kisekta ili kuboresha mazingira ya kilimo, mifugo, uwekezaji, viwanda na biashara;
- Kusimamia utekelezaji wa majukumu ya msingi ya Ofisi ya Rais-TAMISEMI ikiwa ni pamoja na kufanya Ukaguzi, Ufuatiliaji na Tathmini kuhusu utekelezaji wa shughuli za Serikali, Taasisi, Programu na miradi katika ngazi ya Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa;
- Kusimamia matumizi ya TEHAMA katika ngazi zote za Ofisi ya Rais -TAMISEMI.
- Kuendeleza rasilimaliwatu katika ngazi zote za Ofisi ya Rais-TAMISEMI kwa kuwaongezea ujuzi kwa lengo la kuongeza ufanisi katika utendaji kazi;
- Kuratibu shughuli za utendaji kazi kwa Taasisi zilizopo chini ya Ofisi ya Rais – TAMISEMI;
- Kuratibu ujenzi, ukarabati na matengenezo ya miundombinu ya maeneo ya utawala ya Mikoa, Wilaya, na Halmashauri;
- Kusimamia matumizi ya rasilimali fedha katika ngazi zote za Ofisi ya Rais-TAMISEMI;
- Kuratibu shughuli za kuboresha mazingira ya kufanyia kazi kwa watumishi wa Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa; na
- Kusimamia shughuli za utawala bora, kukuza demokrasia, ushirikishwaji wa wananchi na Ugatuaji wa Madaraka kwa Umma (D by D).
MALENGO YA TAASISI ZILIZO CHINI YA OFISI YA RAIS-TAMSEMI KWA MWAKA WA FEDHA 2022/23
Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA)
- Spika, Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) umeendelea kutekeleza majukumu yake ya msingi ya ujenzi, matengenezo na ukarabati wa barabara za Wilaya. Katika Mwaka wa Fedha 2019/20 Shilingi bilioni 251.73 ziliidhinishwa, 2020/21 Shilingi bilioni 275.03 ziliidhinishwa na Mwaka wa Fedha 2021/22 Shilingi bilioni 722.16 ziliidhinishwa.
- kumekuwa na ongezeko katika bajeti ya TARURA kwa Shilingi bilioni 447.13 sawa na asilimia 162.59 kati ya Mwaka wa Fedha 2020/21 na 2021/22kutokana na Serikali kuongeza vyanzo vya fedha vya tozo ya Shilingi 100 kwa kila lita ya mafuta ya petroli/dizeli na fedha kutoka Mfuko Mkuu wa Serikali ambavyo havikuwepo hapo awali.
- Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha 2022/23 Wakala umetengewa Shilingi bilioni 802.29 kutoka vyanzo mbalimbali kwa ajili ya utekelezaji wa kazi za ujenzi, ukarabati na matengenezo ya miundombinu ya barabara. Katika kipindi cha Mwaka wa Fedha 2022/23, Wakala unatarajia kujenga barabara za lami Kilomita 411.80, barabara za changarawe kilomita 10,666.11, matengenezo ya barabara kilomita 24,015.77 madaraja na vivuko 322 pamoja na matengenezo ya miundombinu ya barabara zenye urefu wa mita 12,542.50.
- Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha 2022/23 Wakala umetengewa Shilingi bilioni 257.04 kutoka Mfuko wa Barabara kutekeleza kazi za matengenezo ya barabara kilomita 24,015.77, ujenzi wa barabara za lami kilomita 40.78, ujenzi wa barabara za changarawe kilomita 2,532.51 na madaraja 28.
- Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha 2022/23 Wakala umetengewa Shilingi bilioni 325.77 kutokana na tozo ya mafuta kwa ajili ya utekelezaji wa kazi za ujenzi wa barabara za lami kilomita 157.49, changarawe kilomita 5,735.42, madaraja 218 na mifereji ya maji ya mvua yenye urefu wa mita 4,093.5.
- Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha 2022/23 Wakala umetengewa Shilingi bilioni 127.50 kutoka Mfuko Mkuu wa Serikali kwa ajili ya utekelezaji wa kazi za ujenzi wa barabara za lami kilomita 94.33, changarawe kilomita 2,326.93, madaraja 75 na mifereji ya maji ya mvuayenye urefu wa mita 8,449.
Miradi Inayotekelezwa kupitia Benki ya Dunia na Jumuiya ya Nchi za Ulaya
- Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha 2022/23 Wakala umetengewa Shilingi bilioni 9.68 kutoka Benki ya Dunia kupitia Mradi wa Uboreshaji wa Miundombinu Dar es Salaam (DMDP) kwa ajili ya kuendelea kukamilisha ujenzi wa kilomita 3 za lami, mifereji ya maji ya mvua na gharama za maandalizi ya miradi mipya ya Tanzania Cities Transforming Infrastructure competitiveness (TACTIC) na Bonde la Msimbazi.
- Mheshimiwa Spika, Katika mwaka wa fedha 2022/23, TARURA umetengewa Shilingi bilioni 6.00 kutoka Benki ya Dunia kupitia Mradi wa Maendeleo ya Barabara kwa Ushirikishaji Jamii na Ufunguaji Fursa za Kijamii na Kiuchumi Vijijini (Roads to Inclusion and Social Economic Opportunities – RISE). Mradi huu utatekelezwa kwa miaka mitano kuanzia mwaka 2022/23 utahusisha ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami urefu wa kilomita 530 katika kipindi kizima cha mradi. Mradi pia utahuisha matengenezo ya maeneo korofi katika Halmashauri zote nchini na matengenezo ya kawaida ya barabara kwa kutumia vikundi vya jamii inayoishi kandokando ya barabara husika. Katika mwaka wa fedha 2022/23 kazi zilizopangwa kutekelezwa ni ujenzi wa barabara za Wenda – Mgama kilomita 19 na Mtili – Ifwagi kilomita 14 katika Halmashauri za Wilaya za Iringa na Mufindi mtawalia;
- Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha 2022/23 Wakala umetengewa bajeti ya Shilingi bilioni 16.08 kutoka Benki ya Dunia kwa ajili ya uboreshaji wa Bonde la Mto Msimbazi. Mradi huu utahusisha ujenzi wa daraja jipya la Jangwani, kupanua, kuongeza kina na kuimarisha kingo za mto Msimbazi.
- Mheshimiwa Spika, TARURA imetengewa Shilingi bilioni 16.80 kwa ajili ya kuanza utekelezaji wa mradi wa uboreshaji wa Miundombinu katika Halmashauri 45 za Majiji, Manispaa na Miji kupitia mradi wa Tanzania Cities Transforming Infrastructure and Competitivenes -TACTIC. Mradi huu utatekelezwa katika Madaraja Matatu (Three Tiers – Tier 1, Tier 2 na Tier 3). Mradi huu ni mwendelezo wa Mradi wa Uendelezaji Miji ya Kimkakati nane (8) (Tanzania Strategic Cities Project – TSCP), Mradi wa Uimarishaji Miji 18 (Urban Local Government Strengthening Project-ULGSP) ambayo utekelezaji wake umefikia kikomo na pia utajumuisha Miji mingine 19 ambayo haikuwepo kwenye awamu zilizopita. Aidha, Shilingi bilioni 30.45 zimetengwa kutoka Mapato ya Ndani ya TARURA kwa ajili ya ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami kilomita 3.2, ujenzi wa barabara kwa kiwango cha changarawe kilomita 71.25, ujenzi wa daraja moja, ukamilishaji wa mfumo wa ukusanyaji wa mapato ya ndani ya TARURA pamoja na utelekezaji wa ahadi za Viongozi;
- , fedha hizi zitaelekezwa kwenye uboreshaji wa miundombinu ya barabara kwenye maeneo ya Vijijini na Mijini kwa lengo la kuimarisha huduma za kiuchumi (uzalishaji) na kijamii (huduma za afya na elimu) kwa wananchi. Naomba kutumia fursa hii kuwashukuru Waheshimiwa Wabunge kwa namna wanavyojitoa katika kusimamia shughuli za ujenzi, ukarabati na matengenezo ya miundombinu ya barabara katika majimbo yao.
- Mheshimiwa Spika, utaratibu uliokuwepo awali wa kuwapata Makandarasi wa ujenzi, matengenezo na ukarabati wa miundombinu ya barabara mchakato wa manunuzi ulikuwa unaanza mwezi Julai, mara baada ya Bajeti ya Serikali kuidhinishwa mwezi Juni ambapo mchakato huo ulikuwa ukienda hadi mwezi Oktoba. Utaratibu huo ulisababisha Makandarasi kwa maeneo mengi kupatikana wakati wa kipindi cha mvua, hivyo kusababisha ucheleweshaji wa utekelezaji wa kazi hizo.
- Mheshimiwa Spika, katika kukabiliana na changamoto ya ucheleweshwaji wa ujenzi, matengenezo na ukarabati wa miundombinu ya barabara, Wakala umeanzisha utaratibu wa kuanza mchakato wa ununuzi wa Kandarasi kuanzia mwezi Mei kila mwaka ili fedha zinapoidhinishwa na Bunge Mwezi Juni ya kila mwaka utekelezaji uanze mapema kuliko ilivyokuwa awali. Hii itasaidia kuwapata Makandarasi kwa wakati watakaoweza kutekeleza kazi za ujenzi, matengenezo na ukarabati wa miundombinu ya barabara itakayosaidia wananchi kuendelea kutekeleza shughuli zao za kiuchumi na kijamii.
Tume ya Utumishi wa Walimu
- Mheshimiwa Spika, Tume ya Utumishi wa Walimu imeendelea kutekeleza majukumu yake ya msingi kwa mujibu wa Sheria Sura 448, Kanuni za Mwaka, 2016, Taratibu na miongozo inayohusu kusimamia ajira, maadili na maendeleo ya walimu nchini.
- Mheshimiwa Spika, Serikali imeendelea kuiongezea Tume Bajeti ya matumizi mengineyo (OC) ili kuiwezesha kutekeleza majukumu yake. Kwa Mwaka wa Fedha 2018/19 Tume ilitengewa Shilingi bilioni 4.62, mwaka wa fedha 2019/20 Shilingi bilioni 6.00, Mwaka wa fedha 2020/21 Shilingi bilioni 6.10 na mwaka wa fedha 2021/22 Tume ilitengewa Shilingi bilioni 6.60.
- Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa fedha 2022/23 Tume imetengewa Shilingi bilioni 6.70 kwa ajili ya kutekeleza majukumu yake ya msingi. Aidha, Tume imetengewa Shilingi milioni 670.00 kwa ajili ya kuendelea na ujenzi wa ofisi ya Tume Makao Makuu na kuendelea na ukamilishaji wa ujenzi wa Mfumo wa TSC- MIS. Vilevile, Tume itaendelea kuboresha mazingira ya kazi kwa wafanyakazi kwa kuwaongezea ujuzi, kuwapatia Ofisi na vitendea kazi.
Chuo cha Serikali za Mitaa
- Mheshimiwa Spika, Chuo cha Serikali za Mitaa kimeendelea kutoa mafunzo ya muda mfupi na mrefu ambapo Waheshimiwa madiwani 2,688 na Watendaji wa Kata na Vijiji 3,547 wamepewa mafunzo juu ya uongozi, usimamizi na uendeshaji wa Mamlaka za Serikali za Mitaa ili kuimarisha utoaji wa huduma kwa wananchi. Naomba nichukue fursa hii kuwaelekeza Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kuhakikisha wanatenga fedha kila mwaka kwa ajili ya kuwajengea uwezo Waheshimiwa Madiwani na Watumishi wa kada mbalimbali ili kuboresha utendaji kazi wao ili Chuo hiki kitumike kwa malengo ya kuanzishwa kwake.
- Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha 2022/23 Chuo kitaendelea na majukumu yake ya kutoa elimu, kufanya utafiti na kutoa ushauri wa kitaalam. Katika kutekeleza jukumu la kutoa mafunzo ya muda mrefu Chuo kimepanga kudahili wanafunzi wapya 7,300 kwa ngazi mbalimbali na kuanza kufundisha Shahada ya Kwanza ya Menejimenti ya Rasilimali watu. Pia, Chuo kimepanga kuandaa mitaala ya Shahada ya Kwanza katika Nyaraka na Utunzaji Kumbukumbu na kuanza mchakato wa kuanzisha Shahada ya Uzamili ya Maendeleo ya Jamii, kuandaa Mtaala wa Mafunzo ya “Local Economic Development” na kuanza hatua za awali za uanzishaji wa Kampasi ya Tanzania Zanzibar.
- Spika, katika Mwaka wa Fedha 2022/23 Chuo kimepanga kuanza ujenzi wa jengo la Utawala la chuo lenye ghorofa mbili litakalogharimu Shilingi milioni 907.09 na ujenzi wa majengo ya Chuo cha Serikali za Mitaa Kampasi ya Dodoma Mjini kwa gharama ya Shilingi milioni 255. Ujenzi wa majengo hayo utagharamiwa kwa fedha za mapato ya ndani.
Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka,
Dar es Salaam
- Spika, Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka, Dar es Salaam umeendelea kuboresha huduma za usafiri wa umma katika Mkoa wa Dar es Salaam, ambapo muda wa kusafiri umepungua kutoka masaa matatu na nusu hadi dakika arobaini kutoka Kimara kwenda Kivukoni ambao ndio umbali mrefu unaohudumiwa na mabasi ya mwendo kasi. Aidha, abiria 180,000 wanatumia usafiri huu kwa siku. Napenda kuchukua fursa hii kumshukuru Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri wa Tanzania kwa kutoa fedha kwa ajili ya kuongeza mtandao wa huduma ya usafiri wa Mabasi Yaendayo Haraka.
- Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha 2022/23 Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka, Dar es Salaam utaendelea na uboreshaji wa huduma za usafiri katika Mkoa wa Dar es Salaam na maeneo ya jirani ikiwa ni pamoja na kuendelea na usimamizi wa utoaji wa huduma ya usafiri wa Haraka Mkoani Dar es Salaam awamu ya kwanza, kukamilisha taratibu za manunuzi ya Mtoa Huduma wa Mabasi 95 ya nyongeza kwenye awamu ya kwanza ya BRT; Kubadilisha mfumo wa uendeshaji na ulipaji wa watoa huduma kutoka kupokea tozo ya kupita katika mfumo wa DART na kuanza kutumia utaratibu wa malipo ya umbali ambao mabasi yatakuwa yanatembea.
- Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha 2022/23 Serikali itaendelea kuongeza Mtandao wa Miundombinu ya Mabasi Yaendayo Haraka, Dar es Salaam (BRT) kwa kuendelea na ujenzi wa miundombinu ya BRT Awamu ya Pili (2) yenye urefu wa kilomita 20.6 unaojumuisha barabara za Kilwa (kutoka mzunguko wa Mtaa wa Bandari hadi Mbagala Rangi Tatu); Barabara ya Chang’ombe (kutoka mzunguko wa Mgulani JKT katika barabara ya Kilwa hadi makutano ya Barabara ya Nyerere); Barabara ya Kawawa (kutoka makutano ya Barabara ya Nyerere hadi Magomeni); Mtaa wa Gerezani, Sokoine Drive (kutoka kwenye makutano ya mitaa ya Railway na Gerezani hadi Mtaa wa Zanaki, na Mtaa wa Bandari.
- Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha 2022/23Serikali itaanza ujenzi wa Miundombinu ya Mabasi Yaendayo Haraka Mkoani Dar es Salaam awamu ya tatu (3) yenye urefu wa kilomita 24.3 itakayojumuisha barabara za Nyerere hadi Gongo la Mboto; barabara ya Mandela kutoka TAZARA hadi makutano ya barabara ya Uhuru na Mandela; barabara ya Uhuru kutoka Makutano ya Barabara ya Mandela hadi makutano ya Mtaa wa Shaurimoyo; Mtaa wa Shaurimoyo kutoka makutano ya Barabara ya Uhuru hadi Mtaa wa Lindi; Mtaa wa Lindi kutoka makutano ya Mtaa wa Shaurimoyo hadi Kituo Kikuu cha Gerezani – Kariakoo; Nkurumah kutoka makutano ya Barabara ya Nyerere hadi makutano ya Mtaa wa Bibi Titi; Mtaa wa Maktaba na Mtaa wa Azikiwe hadi makutano na Barabara ya Kivukoni.
- Mheshimiwa Spika, katika kuendelea kuboresha huduma ya usafiri katika mkoa wa Dar es Salaam, DART itaendelea kukamilisha usanifu ambapo awamu ya nne (4) itahusu barabara za Bibi Titi, Alli Hassan Mwinyi na Bagamoyo hadi Tegeta pamoja na barabara ya Sam Nujoma yenye urefu wa kilomita 30.1; awamu ya tano (5) itajumuisha barabara za Nelson Mandela kuanzia Ubungo hadi daraja la Mwalimu Nyerere – Kigamboni; Tabata na Kigogo kuanzia Tabata Segerea kupitia Tabata Dampo, Kigogo hadi barabara ya Kawawa zenye urefu wa kilomita 27.6; usanifu wa awamu ya sita itajumuishabarabara ya Mwai Kibaki hadi Kawe; nyongeza ya Barabara ya Morogoro kutoka Kimara hadi Kibamba na Barabara ya Kilwa kutoka Mbagala Rangi tatu hadi Vikindu yenye urefu wa kilomita 26.5.
Shirika la Elimu Kibaha
- Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha 2022/23 Shirika la Elimu Kibaha litaendelea kutoa elimu ya uuguzi na utabibu katika Chuo cha Afya na Sayansi Shirikishi Kibaha kwa kuongeza udahili kutoka wanachuo 500 kwa mwaka hadi 700 kupitia kozi mpya mbili za Ufamasia na Maabara zinazotarajiwa kuanzishwa.
- Mheshimiwa Spika, Shirika la Elimu Kibaha litaendelea kubuni na kuibua fursa mbambali za kuwawezesha wananchi hasa Vijana, Wanawake na Watu Wenye Ulemavu kufanya shughuli mbalimbali za kiuchumi kupitia Chuo cha Maendeleo ya Wananchi ikiwa ni pamoja na kilimo, ufundi, na biashara ili kuongeza thamani katika shughuli zao za kujikomboa na umasikini na kuongeza pato la taifa.
Bodi ya Mikopo ya Serikali za Mitaa
- Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha 2022/23 Bodi ya Mikopo ya Serikali za Mitaa imetengewa Shilingi bilioni 2.67 zikiwemo ruzuku kutoka Serikali Kuu Shilingi milioni 61.95 naMapato ya Ndani Shilingi bilioni 2.61 ambazo zitatumika kutoa mikopo ya Shilingi bilioni 2.38 kwa Halmashauri zitakazokidhi vigezo vya kukopeshwa, kusimamia na kuratibu urejeshwaji wa mikopo ya Shilingi milioni 940.02 kutoka Halmashauri 9 zinazodaiwa deni hilo, kusimamia na kuratibu ukusanyaji wa michango ya akiba na nyongeza ya mtaji ambapo Shilingi bilioni 1.44 zitakusanywa na Shilingi milioni 233.40 zitakusanya kutoka vyanzo vingine vya mapato.
Shirika la Masoko ya Kariakoo
- Mheshimiwa Spika, Soko la Kariakoo lipo kwenye kitovu cha biashara katika Jiji la Dar es Salaam na linabeba historia ya biashara ya mji Mkuu wa biashara nchini. Uendeshaji wa Soko hili umekuwa na changamoto mbalimbali ikiwemo uchakavu wa majengo na miundombinu ya mifumo ya maji na umeme. Kutokana na changamoto hizo, Serikali imefanya mabadiliko makubwa ikiwa ni pamoja na kubadilisha Menejimenti ya Shirika, kujenga soko jipya badala ya soko la zamani ambalo miundo mbinu yake ilichakaa kwa kiasi kikubwa na kukarabati soko kuu lililoungua moto.
- Mheshimiwa Spika, mradi huu umelenga kubadilisha kabisa mandhari ya soko la Kariakoo, kuongeza maeneo ya biashara, kuboresha mazingira ya kufanyia biashara, kuongeza idadi ya wafanyabiashara na wateja watakaohudumiwa na soko hili kutoka ndani na nje ya nchi wakiwemo watalii pamoja na kuongeza ajira zisizo za moja kwa moja zipatazo 4,626. Faida nyingine itakayopatikana ni kuongeza mapato ya Shirika na Serikali kwa ujumla.
- Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha 2022/23, Shirika la Masoko ya Kariakoo limetengewa Shilingi bilioni 10.00 kwa ajili ya ujenzi na ukarabati kupitia Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam. Mradi huu una sehemu kuu mbili ambapo sehemu ya kwanza ni ukarabati wa soko lililoungua na sehemu ya pili ni ujenzi wa soko la ghorofa sita (6) za juu na ghorofa mbili (2) za chini katika eneo lilipokuwa soko dogo ambalo limebomolewa. Aidha, Shirika litaendelea kusimamia maeneo mengine ya Shirika yaliyopo Tabata Bima, Mbezi Beach Makonde na kuweka mikakati na mifumo thabiti ya uendeshaji wa biashara.
- MALENGO MAHSUSI YALIYOPANGWA KUTEKELEZWA NA OFISI YA RAIS – TAMISEMI KATIKA MWAKA WA FEDHA 2022/23
- , katika Mwaka wa Fedha 2022/23, Ofisi ya Rais -TAMISEMI imepanga kutekeleza malengo mahsusi yafuatayo: –
Mfuko wa Kuchochea Maendeleo ya Jimbo
- Mfuko wa Kuchochea Maendeleo ya Jimbo umeongezewa Shilingi bilioni 4.99 kutoka Shilingi bilioni 11.00 iliyokuwa katika bajeti ya kuanzia mwaka wa fedha 2016/17 – 2021/22 hadi Shilingi bilioni 15.99 kwa mwaka wa fedha2022/23 sawa na ongezeko la asilimia 45.36 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi;
Mchango wa Bima ya Afya kwa Waheshimiwa Madiwani
- Serikali ilianza kulipa posho za Waheshimiwa Madiwani kwa mwaka wa fedha 2021/22 ambapo mchango wa bima ya afya haukujumuishwa kwenye posho hizo. Kwa Mwaka wa Fedha 2022/23, Serikali imetenga fedha ya kuchangia mchango wa mwajiri kwa ajili ya Waheshimiwa Madiwani Shilingi milioni 607.57;
Kuimarisha Usalama na Usimamizi wa Shughuli za Serikali
- Mikoa imeongezewa fedha za uendeshaji wa vikao vya Kamati za Usalama vya mikoa kutoka Shilingi milioni 416.00 hadi Shilingi milioni 780.00 sawa na ongezeko la Shilingi milioni 364.00;
- Mikoa 12 inayopakana na nchi jirani imetengewa jumla ya Shilingi milioni 730.00 kwa ajili ya kuimarisha usalama mipakani;
- Ofisi za Wakuu wa Wilaya zimeongezewa fedha za matumizi mengineyo kutoka Shilingi bilioni 17.13 hadi Shilingi bilioni 26.68 sawa na ongezeko la Shilingi bilioni 9.55 ambalo niongezeko la asilimia 55.75 kwa ajili ya kuwawezesha kusimamia usalama na utekelezaji wa shughuli za Serikali katika maeneo yao;
Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA)
- imetengewa Shilingi bilioni 802.29 kwa ajili ya ujenzi, ukarabati na matengenezo ya miundombinu ya barabara ambapo barabara za lami zenye urefu wa kilomita 411.80, changarawe urefu wa kilomita 10,666.11, ujenzi wa mifereji ya maji yenye urefu wa mita 12,542.50, matengenezo ya barabara kilomita 24,015.77 na madaraja na vivuko 322 vitajengwa. Aidha, TARURA itaanza taratibu za ununuzi mwezi Mei, 2022 ya asilimia 60 ya kazi zilizopangwa ili utekelezaji ufanyike kwa wakati;
Mapato ya Ndani na Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi
- Katika Mwaka wa Fedha 2022/23, Halmashauri zinakadiria kukusanya Mapato ya Ndani ya jumla ya Shilingi trilioni 1.01 ikilinganishwa na Shilingi bilioni 863.85 zilizoidhinishwa kwa Mwaka wa Fedha 2021/22 ambayo ni ongezeko la Shilingi bilioni 148.42 sawa na asilimia 17.18.Ongezeko hili limetokana na Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kuweka mikakati ya pamoja ya kubuni vyanzo vipya, kuimarisha vilivyopo na mikakati zaidi ya ukusanyaji wa mapato (Kiambatisho Na. 11);
- Shilingi bilioni 394.80 zimetengwa kupitia mapato ya ndani ya Halmashauri kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo. Kati ya fedha hizo Shilingi bilioni 75.98 ni mikopo ya asilimia 10 na Shilingi bilioni 318.82 ni kwa ajili ya miradi mingine ya maendeleo kama ifuatavyo:- Shilingi bilioni 35.32 zitatumika kuboresha miundombinu ya afya. Miradi itakayotekelezwa ni pamoja na kuendeleza ujenzi na ukarabati wa wa Hospitali 6 za Halmashauri, vituo vya afya 101, zahanati 205, vituo vya kukusanyia taka 59, majengo ya huduma kwa wagonjwa wa nje (OPD) katika vituo vya afya na Hospitali 9 pamoja na huduma za lishe na ununuzi wa madawa; Shilingi bilioni 25.89 zitatumika kuboresha miundombinu ya biashara ikiwemo ujenzi, ukamilishaji na ukarabati wa stendi 74, masoko 110, maegesho ya magari 38, kuweka mazingira wezeshi ya viwanda vidogo 26, maeneo ya kupumzikia 4 pamoja na kuboresha vituo vya kukusanyia mapato 61; Shilingi bilioni 51.52 zimetengwa kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya elimu ikiwemo ujenzi, ukamilishaji na ukarabati wa vyumba vya madarasa 2,935, matundu ya vyoo 4,787, daharia (hosteli) 102, maabara za masomo ya sayansi 78, mabwalo ya chakula 20 na kutengeneza madawati 56,049; Shilingi bilioni 7.57 zitatumika kuboresha miundombinu ya kilimo, mifugo na uvuvi ikiwemo ujenzi, ukamilishaji na ukarabati wa machinjio 124, miundombinu ya umwagiliaji 50, maghala 12, majosho 52, mashamba darasa 28, mabwawa ya samaki 31, malambo 10 na mashine za usindikaji 8; Shilingi bilioni 93.71 zitatumika kuboresha mazingira ya kufanyia kazi kwa watumishi ikiwemo ujenzi, ukamilishaji na ukarabati wa majengo ya utawala yakijumuisha ofisi za walimu na ofisi za Halmashauri 482, nyumba za watumishi 303, uzio wa majengo 87, ofisi za kata 113, kumbi 30, ofisi za vijji 98, ofisi za Mitaa 16, ununuzi wa pikipiki 65, malori manne (4), ufuatiliaji wa miradi ya maendeleo na utoaji wa mafunzo, mifumo ya umeme na TEHAMA; Shilingi bilioni 13.32 zitatumika kwa ajili ya mipango miji na matumizi bora ya ardhi, vituo vya utalii na viwanja vya michezo; na Shilingi bilioni 21.95 zitatumika kwa ajili ya matengenezo ya barabara, madaraja 20, uwekaji wa taa za barabarani na ujenzi wa mifereji ya maji; na Shilingi bilioni 68.99 zimepangwa kutumika katika miradi mingine;
- Shilingi bilioni 75.97 zinazotokana na asilimia 10 ya Mapato ya Ndani ya Halmashauri ambayo ni sehemu ya miradi ya amendeleo zimetengwakwa ajili ya mikopo ya vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu Wenye Ulemavu ambayo ni sehemu ya fedha za maendeleo zinazotokana na asilimia 40/60. Kati ya fedha hizo, Shilingi bilioni 30.39 ni kwa ajili ya vikundi vya Wanawake, Shilingi bilioni 30.39 ni kwa ajili ya vikundi vya Vijana na Shilingi bilioni 15.19 ni kwa ajili ya vikundi vya Watu Wenye Ulemavu (Kiambatisho Na. 13).Aidha, Ofisi ya Rais – TAMISEMI imeweka mikakati mbalimbali ili kuhakikisha mikopo hii inasimamiwa kwa ufanisi. Moja ya mikakati iliyowekwa ni kuweka kigezo cha utoaji wa mikopo, usimamizi wa matumizi ya mikopo hiyo pamoja na marejesho kuwa sehemu ya kuwapima Wakurugenzi wa Halmashauri ambayo itafanyika kila robo mwaka na tathmini ya kina itafanyika mwisho wa mwaka. Mkakati mwingine ni matumizi ya Mfumo wa Kielektroniki utakaosaidia kuondoa changamoto katika ukopeshaji, usimamizi na urejeshaji wa mikopo. Hivyo, itakuwa ni kazi ya Wakurugenzi kuhakikisha mfumo unatumika ipasavyo na kuongeza ufanisi; na
- Jumla ya Shilingi bilioni 4.76 zimetengwa kwa ajili ya uratibu wa Huduma Ndogo za Fedha ambapo Taasisi na vikundi vinavyojishughulisha na shughuli za fedha ambavyo siyo rasmi katika Mamlaka za Serikali za Mitaa vitarasimishwa kupitia utaratibu huu;
Sekta ya Afya
- Kuendelea na ujenzi wa Hospitali 28 za Halmashauri ambazo zimetengewa Shilingi bilioni 24.65 (Kiambatisho Na. 14);
- Kuendelea na ujenzi wa Hospitali 31 za Halmashauri ambazo zimetengewa Shilingi bilioni 15.50 (Kiambatisho Na. 14);
- Ukarabati wa Hospitali kongwe 19 za Halmashauri ambazo zimetengewa Shilingi bilioni 16.55 (Kiambatisho Na. 14);
- Ukamilishaji wa ujenzi wa maboma ya Zahanati 300 ambazo zimetengewa Shilingi bilioni 15.00 (Kiambatisho Na. 14);
- Shilingi bilioni 15.15 zimetengwa kwa ajili ya ununuzi wa Vifaa Tiba kwa Zahanati 300, Shilingi bilioni 47.70 za ununuzi wa Vifaa Tiba kwa Vituo vya Afya 159 na Shilingi bilioni 7.10 zaununuzi wa Vifaa Tiba ya afya ya kinywa na macho kwa ajili ya hospitali za Halmashauri 71 zilizokamilika (Kiambatisho Na. 15);
Sekta ya Elimu
- Elimumsingi Bila Malipo kiasi cha Shilingi bilioni 346.49 zimetengwasawa na ongezeko la Shilingi bilioni 34.44 ya fedha zilizoidhinishwa mwaka wa fedha 2021/22 ambayo ni Shilingi bilioni 312.05 (Kiambatisho Na 16);
- Shilingi bilioni 55.57 zimetengwa kwa ajili ya ujenzi wa nyumba 809 za walimu zenye uwezo wa kuchukua kaya 1,916. Kati yake, nyumba za walimu wa shule za msingi ni 298 za (3 in1) ambazo zitajengwa kupitia fedha za ruzuku kutoka Serikali Kuu kwa Shilingi bilioni 30.02 na Shilingi bilioni 25.55 zitatumika kujenga nyumba 511 (2 in1) za walimu wa shule za sekondari kupitia mradi wa Uboreshaji wa Elimu ya Sekondari (SEQUIP) (Kiambatisho Na. 17);
- Ujenzi wa matundu ya vyoo 9,700 katika Vituo shikizi 970 ambapo Shilingi bilioni 10.67 zimetengwa (Kiambatisho Na. 17);
- Kuanza Awamu ya Kwanza ya ujenzi wa vyumba vya madarasa 1,700 katikaShule Kongwe za Msingi Shilingi bilioni 34.00 zimetengwa (Kiambatisho Na. 17) ;
- Ujenzi wa Shule Mpya 39 za MsingiShilingi bilioni 15.60 zimetengwa(Kiambatisho Na. 17);
- Ujenzi wa uzio wa mabweni 99 ya wanafunzi wenye mahitaji maalum ambapo Shilingi bilioni 2.97 zimetengwa (Kiambatisho Na. 17);
- Ukamilishaji wa maboma ya vyumba vya madarasa 1,911 katika Shule za Msingi ambapo Shilingi bilioni 23.88 zimetengwa (Kiambatisho Na. 18);
- Ukamilishaji wa ujenzi wa vyumba vya maabara 291 katika Shule za Sekondari ambapo Shilingi bilioni 8.73 zimetengwa (Kiambatisho Na. 18);
- Ukamilishaji wa mabwalo 86 ambapo mabwalo 80 katika shule za sekondari na mabwalo sita (6) katika Shule za Msingi Shilingi milioni 4.30 zimetengwa (Kiambatisho Na. 18);
- Ukamilishaji wa mabweni 461 ambapo mabweni 28 katika shule za Msingi zenye wanafunzi wenye mahitaji maalum na mabweni 433 kwa Shule za Sekondari ambapo Shilingi bilioni 9.21 zimetengwa (Kiambatisho Na. 18);
- Kuwezesha kufanyika kwa mitihani ya Taifa ya Darasa la Nne, la Saba, Kidato cha Pili, Kidato cha Nne na Kidato cha Sita Shilingi bilioni 142.33 zimetengwa(Kiambatisho Na. 19);
- Shilingi milioni 670.00 zimetengwa kwa ajili ya ujenzi wa jengo la Tume ya Utumishi wa Walimu pamoja na uundaji wa mfumo;
Utawala Bora
- Jumla ya Shilingi bilioni 36.11 zimetengwa kwa ajili ya ujenzi, ukamilishaji na ukarabati wa majengo ya ofisi na nyumba za viongozi kama ifuatavyo: Shilingi bilioni 1.15 zimetengwa kwa ajili ya upanuzi wa Ofisi za Wakuu wa Mikoa 3 ya Dodoma, Kilimanjaro na Singida; Shilingi bilioni 3.58 kwa ajili ya ukarabati wa Ofisi za Wakuu wa Mikoa 9; Wakuu wa Wilaya 15 na Ofisi moja (1) ya Afisa Tarafa; Shilingi milioni 967.89 zimetengwa kwa ajili ya ukarabati wa nyumba mbili (2) za Wakuu wa Mikoa, nyumba 18 za Wakuu wa Wilaya, nyumba moja (1) ya Katibu Tawala wa Mkoa na nyumba 4 za Makatibu Tawala wa Wilaya; Shilingi bilioni 2.38 zimetengwa kwa ajili ya Ujenzi na ukamilishaji wa Ikulu ndogo saba (7) na ukarabati wa Ikulu Ndogo tatu (3); Shilingi bilioni 6.75 zimetengwa kwa ajili ya ujenzi na ukamilishaji wa nyumba za Viongozi 40; Shilingi bilioni 19.43 kwa ajili ya ujenzi, ukamilishaji na ukarabati wa majengo ya ofisi 61 yakiwemo ya Wakuu wa Mikoa 10; Wakuu wa Wilaya 19 na ofisi za Tarafa 32.
- Serikali imetenga Shilingi bilioni 10.00 kwa ajili ya kuendeleza ujenzi wa Soko jipya la Kariakoo na kukarabati Soko Kuu liloungua moto tarehe 10 Julai, 2021;
- Serikali imetenga Shilingi bilioni 8.90 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba 111 za Wakuu wa Idara na Shilingi bilioni 7.20 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba 48 za Wakurugenzi (Kiambatisho Na. 21);
- Halmashauri 83 zimetengewa Shilingi bilioni 68.85 kwa ajili ya kuendelea na ujenzi wa majengo ya utawala (Kiambatisho Na. 21);
- Halmashauri 13 zimetengewa Shilingi bilioni 13.00 kwa ajili ya ujenzi wa majengo mapya ya utawala (Kiambatisho Na. 21);
- Jumla ya Shilingi bilioni 2.05 zimetengwa kwa ajili ya ununuzi wa boti: Halmashauri za Wilaya za Mafia (boti mbili), Kilwa (boti moja), Ukerewe (boti mbili), Muleba (boti moja), Kalambo (boti moja) na Momba (boti moja);
- Halmashauri 20 zimetengewa jumla yaShilingi bilioni 40.11 kwa ajili ya kuendelea na utekelezaji wa miradi ya kimkakati (Kiambatisho Na. 22);
Programu mbalimbali
- Jumla ya Shilingi bilioni 1.41 zimetengwa kupitia Programu ya Kuimarisha Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa ajili ya kuimarisha Mfumo wa Ugatuaji utakaosaidia kuboresha huduma za jamii, utawala bora na kuwa na maendeleo endelevu;
- Jumla ya Shilingi bilioni 135.43 zimetengwa kupitia Programu ya Uboreshaji wa Elimu ya Sekondari (SEQUIP) kwa ajili ya uendelezaji wa ujenzi wa shule 10 za sekondari za wasichana za bweni kwa masomo ya sayansi, shule za sekondari 232 za Kata, ujenzi wa shule mpya za kata 184, ujenzi wa shule mpya tano (5) za sekondari za wasichana za bweni kwa masomo ya sayansi na fedha kwa ajili ya ufuatiliaji na tathmini;
- Jumla ya Shilingi bilioni 55.38 zimetengwa kupitia Programu ya Maji na Usafi wa Mazingira (SRWSS) kwa upande wa elimu na Afya kwa ajili ya kuimarisha shughuli za afya na usafi wa mazingira;
- Jumla ya Shilingi bilioni 237.36 zimetengwa kupitia Programu ya BOOST kwa ajili ya kuimarisha ujifunzaji na ufundishaji katika elimu ya awali na msingi;
- Jumla ya Shilingi bilioni 17.27 zimetengwa kupitia DART kwa ajili ya kununua Mfumo wa kusimamia magari na kusimika vifaa vya kukusanyia nauli kwa mfumo wa kielektroniki; na
- Jumla ya Shilingi bilioni 83.29 zimetengwa kupitia Programu ya Mfuko wa Pamoja wa Afya kwa ajili ya uboreshaji wa huduma za afya katika vituo vya kutolea huduma.
- , Ofisi ya Rais – TAMISEMI itaendelea kusimamia na kuratibu maandiko ya miradi ya kimkakati kwa kushirikiana na Timu ya Kitaifa iliyoundwa na Wizara ya Fedha na Mipango kwa ajili ya kuratibu maandiko ya miradi inayoweza kukopesheka kupitia Programu ya ugharamiaji wa miradi mbadala. Timu hii imeundwa ili kutatua changamoto ya uandishi wa maandiko ya miradi kutoka katika Halmashauri mbalimbali na hivyo kuzisababishia Halmashauri kutokidhi vigezo vilivyowekwa na Serikali ili kupata fedha za utekelezaji wa miradi hiyo. Naomba kutumia fursa hii kuzielekeza Halmashauri ziibue miradi ili iweze kugharamiwa kupitia utaratibu wa ugharamiaji mbadala wa miradi ikijumuisha Hati Fungani za Halmashauri.
- Mheshimiwa Spika, Ofisi ya Rais – TAMISEMI itazielekeza Halmashauri kuhakikisha zinatekeleza miradi maalum kupitia mapato ya ndani ya Halmashauri kupitia vipaumbele vilivyopo. Vipaumbele hivyo vitajumuisha: ukamilishaji wa ujenzi wa maboma ya vyumba vya madarasa, zahanati, maabara ya masomo ya sayansi, ujenzi wa matundu ya vyoo kwa Shule za Msingi na Sekondari, ununuzi wa vifaa, vifaa tiba na vitendanishi, nyumba za watumishi na kuendeleza ujenzi wa maeneo ya wafanyabiashara wadogo (wamachinga). Vilevile, Halmashauri zenye Mapato ya Ndani zaidi ya Shilingi bilioni 5.00 zinaelekezwa pia kuchangia asilimia 10 kwa ajili ya ujenzi wa barabara zinazosimamiwa na TARURA.
- Mheshimiwa Spika, Halmashauri zote zinaelekezwa kuendelea na utengaji, uboreshaji, upangaji na ujenzi wa miundombinu ya maeneo ya kufanyia biashara wafanyabiashara wadogo (machinga) pamoja na kuwaunganisha na Taasisi za kifedha, ili kuwaongezea fursa za kiuchumi na Serikali itanufaika na ushuru pamoja na kodi mbalimbali kupitia shughuli zao. Kwa sasa Halmashauri kumi na moja (11) yakiwemo Majiji sita (6) Manispaa Nne (4) na Halmashauri ya Mji moja (1) zimeanza ujenzi wa miundombinu rafiki kwa ajili ya wafanyabiashara wadogo (machinga). yatakayowawezesha kurasimisha biashara zao ili watambulike na kuunganishwa na Taasisi za kifedha.
- Mheshimiwa Spika, wanafunzi wanaotarajiwa kuandikishwa Kidato cha Kwanza Januari 2023, kwa ufaulu wa asilimia 82 ni 1,257,996 kati ya wanafunzi 1,534,141 waliopo darasa la saba mwaka 2022. Ongezeko hili linatokana na wanafunzi wa kundi la kwanza la mpango wa elimumsingi bila malipo wanaotarajiwa kuhitimu darasa la saba mwaka 2022. Kutokana na ongezeko hilo, mahitaji ya vyumba vya madarasa ya wanafunzi wa sekondari yatakuwa 15,186 vyumba vya madarasa vitakavyokuwepo baada ya wanafunzi wa Kidato cha Nne kuhitimu ni 7,200 na kusababisha upungufu wa vyumba 7,986. Hivyo, Serikali itajenga madarasa haya kupitia ruzuku ya Serikali Kuu, mapato ya ndani ya Halmashauri na fedha za Washirika wa maendeleo wakiwemo SEQUIP.
- Mheshimiwa Spika, naomba kuchukua fursa hii kuzielekeza Mamlaka za Serikali za Mitaa kutenga na kupeleka asilimia 20 ya Mapato yatokanayo na tozo ya mazao ya kilimo (crop cess) kwa ajili ya shughuli za kilimo ikiwemo kuendeleza uzalishaji wa mazao ya kimkakati. Aidha, Halmashauri zitenge asilimia 15 ya mapato yatokanayo na mazao ya mifugo kwa ajili ya shughuli za kuendeleza ufugaji kwa mujibu wa Waraka wa Rais Na.01 wa mwaka 2002 kuhusu hatua za kuchukua kuzuia kuenea kwa magonjwa ya mifugo nchini. Vilevile, Halmashauri zitenge asilimia tano (5) ya mapato yatokanayo na mazao ya uvuvi kwa mujibu wa Sheria ya Uvuvi Na. 22 ya mwaka 2003 na Kanuni zake za mwaka 2009.
- SHUKRANI
- Mheshimiwa Spika, kabla ya kuhitimisha Hotuba yangu, naomba kukushukuru wewe binafsi, Naibu Spika na Wenyeviti wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa uongozi imara katika kutekeleza shughuli za Bunge. Vilevile, naishukuru Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa (USEMI) inayoongozwa na Mheshimiwa Abdallah Jaffari Chaurembo Mbunge wa Jimbo la Mbagala, Mwenyekiti wa Kamati, na Mheshimiwa Denis Lazaro Londo Mbunge wa Jimbo la Mikumi, Makamu Mwenyekiti wa Kamati kwa kazi nzuri katika kusimamia utendaji wa Ofisi ya Rais – TAMISEMI. Maoni na ushauri wa Kamati umesaidia kuleta mageuzi makubwa yaliyotokea katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo na utoaji wa huduma katika Tawala za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa.
- Mheshimiwa Spika, napenda kumshukuru Mheshimiwa Daniel Barran Sillo Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti na Mheshimiwa Omary Mohammed Kigua Makamu Mwenyekiti na wajumbe wa Kamati kwa maoni, maagizo na maelekezo mengine ambayo wanaendelea kutuelekeza kuhusu utekelezaji wa Mipango na Bajeti.
- Spika, kipekee naishukuru Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) inayoongozwa na Mheshimiwa Grace Victor Tendegu Mbunge wa Viti Maalum, Mwenyekiti wa Kamati na Mheshimiwa Selemani Jumanne Zeddy Mbunge wa Jimbo la Bukene Makamu Mwenyekiti wa Kamati kwa maoni, maelekezo na maagizo yao katika uboreshaji wa usimamizi wa fedha katika Mamlaka za Serikali za Mitaa.
- Mheshimiwa Spika, Ofisi ya Rais – TAMISEMI inatambua na kuthamini mchango mkubwa wa Wadau wa Maendeleo katika utekelezaji wa Programu, Miradi na shughuli mbalimbali za Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa.Washirika hawa ni pamoja na Benki ya Dunia (WB), Shirika la Afya Duniani (WHO), Shirika la Ushirikiano wa Kimataifa la Japan (JICA), Jumuiya ya Ulaya (EU), Global Partnership for Education, Shirika la Maendeleo la Uingereza (Foreign, Commonwealth and Development Office-FCDO), Shirika la Maendeleo la Marekani (USAID), Shirika la Maendeleo la Ujerumani (GIZ), Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF), Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu (UNFPA), Shirika la Kuleta Mapinduzi ya Kijani (AGRA) na Nchi zinazochangia kupitia Mfuko wa Pamoja wa Afya ambazo ni Denmark, Ireland, Jamhuri ya Korea (KOICA), Shirika la Maendeleo (SIDA), Global Partnership for Education- (GPE), Switzerland na Shirika la Umoja wa Mataifa na Mitaji na Maendeleo (UNCDF).
- Mheshimiwa Spika, Ofisi ya Rais – TAMISEMI itaendelea kushirikiana na Wadau wa Maendeleo katika utekelezaji wa shughuli za kiuchumi na kijamii ili kuboresha utoaji wa huduma na kupunguza umaskini. Aidha, ninawashukuru wananchi kwa mchango mkubwa katika utekelezaji wa Miradi na Programu mbalimbali kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa.
- Mheshimiwa Spika, napenda kutambua mchango mkubwa wa Viongozi wenzangu katika kufanikisha utekelezaji wa majukumu ya Ofisi ya Rais-TAMISEMI. Kipekee, nawashukuru Naibu Mawaziri,Mheshimiwa Dkt. Festo John Dugange, Mbunge wa Jimbo la Wanging’ombe na Mheshimiwa David Ernest Silinde, Mbunge wa Jimbo la Tunduma, kwa msaada mkubwa wanaotoa kwangu katika kutekeleza majukumu ya Ofisi ya Rais – TAMISEMI.
- Mheshimiwa Spika, aidha, namshukuru Katibu Mkuu, Prof. Riziki Silas Shemdoe kwa mchango wake katika kufanikisha maandalizi ya Mpango na Bajeti na Naibu Makatibu Wakuu Bw. Gerald Geofrey Mweli, Dkt. Grace Elias Magembe na Dkt. Switbert Zacharia Mkama katika usimamizi wa majukumu ya Ofisi ya Rais – TAMISEMI.Vilevile, nimpongeze Bi. Paulina Mbena Nkwama Katibu wa Tume ya Utumishi wa Walimu kwa kusimamia vyema Tume ya Utumishi wa Walimu. Aidha, ninawashukuru Waheshimiwa Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Waheshimiwa Madiwani, Wakuu wa Taasisi zilizo chini ya Ofisi ya Rais -TAMISEMI, Wakurugenzi wa Ofisi ya Rais – TAMISEMI na Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa pamoja na Watumishi wote wa Ofisi ya Rais – TAMISEMI na Taasisi zake kwa ushirikiano wanaonipa katika kutekeleza majukumu ya Ofisi ya Rais – TAMISEMI.
- Mheshimiwa Spika, naomba kutumia fursa hii pia kuwashukuru Viongozi wenzangu katika Ofisi ya Rais, Mheshimiwa Jenista Joakim Mhagama Mbunge wa Jimbo la Peramiho, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Utumishi wa Umma na Utawala Bora; na Mheshimiwa George Huruma Mkuchika Mbunge wa Jimbo la Newala Mjini, Waziri Asiyekuwa na Wizara Maalum kwa ushirikiano wao katika utekelezaji wa majukumu ya Ofisi ya Rais.
- Mheshimiwa Spika, napenda pia kuwashukuru WaheshimiwaMawaziri wenzangu wote kwa ushirikiano walionipa katika kipindi cha Mwaka wa Fedha 2021/22 katika utekelezaji wa majukumu ya Ofisi ya Rais –TAMISEMI.
- Mheshimiwa Spika, kwa heshima na unyenyekevu mkubwa ninawashukuru wananchi wa Jimbo la Karagwe kwa kuniamini na kunichagua tena kuwa Mbunge wao. Ninawaahidi wana Karagwe kuwa nitaendelea kuwatumikia kwa nguvu zangu zote ili kuifanya Karagwe yetu ipate maendeleo zaidi ya kiuchumi na kijamii. Kipekee, ninaishukuru familia yangu kwa kuniombea na kwa uvumilivu wao muda wote ninapokuwa mbali nao katika kutekeleza wa majukumu ya kitaifa.
- MAOMBI YA FEDHA KWA MWAKA WA FEDHA 2022/23
Maduhuli na Makusanyo ya Mapato ya Ndani
- Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha 2022/23, Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Taasisi zilizo chini yake, Mikoa 26 na Halmashauri 184 inaomba idhini ya kukusanya Maduhuli na Mapato ya Ndani jumla ya Shilingi Trilioni moja Bilioni Sabini na Moja Milioni Mia Saba na Thelathini Mia Nane na Themanini na Sita Elfu Mia Nne na Kumi na Tano na Senti Hamsini (Shilingi 1,071,730,886,415.50).Makusanyo haya yatatokana na mauzo ya vifaa chakavu, ada za wanafunzi, tozo na ushuru unaotozwa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kulingana na Sheria ya Fedha za Serikali za Mitaa, Sura 290. Mchanganuo wa makusanyo ya mapato hayo ni kama ifuatavyo:
Jedwali Na. 1: Mchanganuo wa Maduhuli na Mapato ya Ndani kwa Mwaka wa Fedha 2022/23 | |
OFISI/TAASISI | MAKADIRIO |
Ofisi ya Rais – TAMISEMI | 0 |
Taasisi | 59,195,516,103.50 |
Mikoa | 249,281,312.00 |
Halmashauri | 1,012,286,089,000.00 |
JUMLA KUU | 1,071,730,886,415.5 |
- Mheshimiwa Spika, sasa naomba Bunge lako Tukufu likubali kuidhinisha Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2022/23 jumla ya Shilingi Trilioni Nane Bilioni Mia Saba Sabini na Nane Milioni Mia Sita na Saba Mia Saba Sitini na Tatu Elfu na Mia Mbili (Shilingi 8,778,607,763,200.00) kwa ajili ya Ofisi ya Rais – TAMISEMI Fungu 56, Tume ya Utumishi wa Walimu Fungu Na. 2 na Mafungu 26 ya Mikoa yanayojumuisha Halmashauri 184.
- Mheshimiwa Spika, kati ya fedha zinazoombwa, Shilingi Trilioni Tano Bilioni Mia Tano Kumi na Moja Milioni Mia Moja Kumi na Tano Mia Moja Tisini na Tatu Elfu (Shilingi 5,511,115,193,000.00) ni kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida yanayojumuisha Mishahara Shilingi Trilioni Nne Bilioni Mia Sita Ishirini na Sita Milioni Mia Mbili Hamsini na Tatu Mia Nane Sitini na Nane Elfu (Shilingi 4,626,253,868,000.00) na Shilingi Bilioni Mia Nane Themanini na Nne Milioni Mia Nane Sitini na Moja Mia Tatu Ishirini na Tano Elfu (Shilingi 884,861,325,000.00) kwa ajili ya Matumizi Mengineyo. Aidha, jumla ya Shilingi Trilioni Tatu Bilioni Mia Mbili Sitini na Saba Milioni Mia Nne Tisini na Mbili Mia Tano Sabini Elfu na Mia Mbili (Shilingi 3,267,492,570,200.00) zinaombwa kwa ajili ya Miradi ya Maendeleo ambapo kati ya fedha hizo Shilingi Trilioni Mbili Bilioni Mia Moja Arobaini na Saba Milioni Mia Moja Themanini na Sita Mia Tatu Sabini na Moja Elfu na Mia Mbili (Shilingi 2,147,186,371,200.00) ni fedha za ndani na Shilingi Trilioni Moja Bilioni Mia Moja Ishirini Milioni Mia Tatu na Sita Mia Moja Tisini na Tisa Elfu (Shilingi 1,120,306,199,000.00) ni fedha za nje(Mchanganuo wa fedha zinazoombwa katika Mwaka wa Fedha 2022/23 umeoneshwa katika Jedwali Na. 2.
Jedwali Na. 2: Mchanganuo wa Makisio katika Mafungu 28 ya Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Tume ya Utumishi wa Walimu, Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa Mwaka wa Fedha 2022/23
AINA YA MATUMIZI | BAJETI KWA MWAKA WA FEDHA 2022/23 |
Matumizi ya Kawaida Ofisi ya Rais -TAMISEMI | |
Mishahara | |
Mishahara Makao Makuu | 9,556,977,000.00 |
Mishahara ya Taasisi | 53,823,523,000.00 |
Jumla Mishahara Ofisi ya Rais – TAMISEMI | 63,380,500,000.00 |
Matumizi Mengineyo | |
Makao Makuu | 12,494,284,000.00 |
Taasisi | 2,643,670,000.00 |
Jumla ya Matumizi Mengineyo | 15,137,954,000.00 |
Jumla Matumizi ya Kawaida | 78,518,454,000.00 |
TUME YA UTUMISHI WA WALIMU (TSC) | |
Mishahara | 8,276,293,000.00 |
Matumizi Mengineyo | 6,708,202,000.00 |
Jumla ya Matumizi ya Kawaida TSC | 14,984,495,000.00 |
MIKOA NA HALMASHAURI | |
MIKOA: | |
Mishahara | 76,205,297,000.00 |
Matumizi Mengineyo | 79,099,078,000.00 |
Jumla ya Matumizi ya Kawaida | 155,304,375,000.00 |
HALMASHAURI | |
Mishahara | 4,478,391,778,000.00 |
Matumizi Mengineyo (SK) | 166,430,744,000.00 |
Matumizi Mengineyo (MSM) | 617,485,347,000.00 |
Jumla Matumizi ya Kawaida | 5,262,307,869,000.00 |
MIRADI YA MAENDELEO | |
OFISI YA RAIS -TAMISEMI | |
Fedha za Ndani | 758,726,035,200.00 |
Fedha za Nje | 124,312,896,000.00 |
Jumla Maendeleo | 883,038,931,200.00 |
TUME YA UTUMISHI WA WALIMU | |
Fedha za Ndani | 670,000,000.00 |
Jumla | 670,000,000.00 |
MIKOA | |
Fedha za Ndani | 66,018,770,000.00 |
Fedha za Nje | 18,508,243,000.00 |
Jumla Maendeleo | 84,527,013,000.00 |
HALMASHAURI | |
Fedha za Ndani (SK) | 926,970,824,000.00 |
Fedha za Ndani (MSM) | 394,800,742,000.00 |
Fedha za Nje | 977,485,060,000.00 |
Jumla Maendeleo Halmashauri | 2,299,256,626,000.00 |
JUMLA KUU | 8,778,607,763,200.00 |
SK – Serikali Kuu na MSM – Mapato ya Ndani ya Mamlaka za Serikali za Mitaa
- Mheshimiwa Spika, pamoja na hotuba hii yapo majedwali ambayo yanafafanua kwa kina makadirio ya mapato na matumizi ya fedha ya Ofisi ya Rais – TAMISEMI Fungu 56, Tume ya Utumishi wa Walimu Fungu Na. 2, Mikoa na Halmashauri Mafungu 26 ambayo ni sehemu ya hotuba hii.
- Mheshimiwa Spika, hotuba hii inapatikana pia kwenye Tovuti ya Ofisi ya Rais – TAMISEMI ambayo ni www.tamisemi.go.tz.
- Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja.