CHIKOTA ASHAURI MABADILIKO YA SHERIA YA TAWALA ZA MIKOA

Mbunge wa Nanyamba (CCM), Abdallah Chikota ameshauri kufanyika mapitio ya Sheria ya Tawala za Mikoa ya mwaka 1997 ili kuangalia muundo wa sasa wa Sekretarieti za Mikoa ili kukidhi mahitaji yaliyopo.

Akichangia leo hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kwa mwaka 2022/23 bungeni jana, Chikota amesema Sheria hiyo na sera ya ugatuaji ya mwaka 1998 inabainisha majukumu ya sekretarieti za mikoa katika kusimamia na kuzishauri Halmashauri.

“Tulitegemea kwenye sekretarieti za mikoa kuwe na wabobezi ili wakienda wakashauri lakini changamoto iliyopo sasa hivi sekretarieti hazina wataalamu hao unakuta mtaalamu anakwenda kushauri ni junior kuliko anayemkuta kwenye Halmashauri unakuta ushauri wake hausikilizwe lakini hata cha kushauri hana,”amesema.

Ameongeza “Kama tungekuwa na mfumo imara wa Sekretarieti za mikoa Mawaziri msingekimbizana majukumu haya yafanyike na hizo sekretarieti, tuziwezeshe kuwa na wataalamu mahiri na tuwape rasilimali fedha ili zitekeleze majukumu yake na Mawaziri mtulie kufanya maamuzi ya msingi.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *