SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WANAOPANDISHA BEI BIDHAA ZISIZO NA HADHI YA KUPANDISHWA BEI

Serikali kuangalia namna ya kuweza kushusha bei za mafuta

Kauli hiyo imetolewa Bungeni Jijini Dodoma na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa wakati akihitimisha hoja za wabunge zilizoibuliwa kwenye Bunge la 12 Mkutano wa 7 kuhusu Hoja ya Bajeti Ofisi ya Waziri Mkuu

Majaliwa alisema kutokana na suala hilo juu ya upandaji wa bidhaa mbalimbali ambapo amesema zimekuwa zikipanda kutokana na matukio mbalimbali yanayoikumba nchi yetu ikiwemo majanga ya Uviko 19 na Vita ya Urusi na Ukraine ambapo amesema yamekuwa na athari za moja kwa moja..
“vikwazo dhidi ya Urusi imepelekea kupungua kwa uzalishaji wa bidhaa na mafuta
bidhaa hizo zitaendelea kuangaliwa na kufuatiliwa kwa umakini zaidi”

Alisema Serikali kupitia kamati za bei zitaendelea kufanya tathimini kupitia wakuu wa mikoa na wilaya na kukagua Bidhaa ambazo hazina hadhi ya kupandisha bei kutokupanda huku serikali ikiimarisha uzalishaji wa bidhaa za ndani ili kukabiliana na mtikisiko wa kiuchumi.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *