WAZIRI NDALICHAKO AZINDUA BODI KIMA CHA CHINI CHA MSHAHARA, NEEMA KUWASHUKIA WAFANYAKAZI

Na Emmanuel Charles

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Ajira, Kazi, Vijana na Wenye Ulemavu Mhe.Prof Joyce Ndalichako ameiagiza Bodi ya Kima cha chini cha mshahara kwa Sekta Binafsi kujifunza vyema na Kutoa Mapendekezo yatakayosaidia Maisha halisi ya Wafanyakazi
Waziri Ndalichako ameyasema hayo leo April 12, 2022 Jijini Dodoma alipozindua Bodi ya Kima cha Chini cha Mshahara ambapo alisema amefanya Uteuzi wa Wajumbe wa Bodi hiyo kwa kuzingatia Sheria ya Taasisi za Kazi Sura ya 300 ya Mwaka 2014.
“Kazi mtakayokwenda kuifanya ni ngumu nami sina shaka na uzoefu wenu, nina uhakika mtakwenda kufanya kazi kwa usahihi”

Prof Ndalichako alisisitiza kuwa, Bodi hiyo itakwenda kufanya uchunguzi na kutoa mapendekezo kwa Waziri kwa kuzingatia Matakwa ya Kazi na Mikataba ya Kazi ya Kimataifa na kuweka Usawa kwa Pande zote mbili pasipo upendeleo
“Kima cha chini cha mshahara ni suala mhimu linalopaswa kufanyika kwa maslahi ya wafanyakazi na hali halisi ya Maisha na Mzania kwa Pande zote mbili.
Waziri Prof.Ndalichako alisema, Serikali inatekeleza mipango ya Ajira kwa Kipindi cha Miaka Mitano hadi Mwaka 2026 ambayo inatoa mwongozo na Dira kwa wafanyakazi
Alisema lengo la Serikali ni kujenga uchumi wa Viwanda kwa maendeleo ya watu
“Mheshimiwa Rais amedhamiria, anapenda kuona wafanyakazi wanafanya kazi kwa moyo pasipo kusukumwa na kujiona fahari kwa utekelezaji wa majukumu yake na kupenda kile anachokifanya”

Alisisitiza, ni wajibu wa Bodi kufanya kazi hiyo kwa weledi

Kwa Upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Kazi, Ajira, Vijana, na wenye Ulemavu Jamal Adam alisema kuwa wameita wataalamu waweze kupata mafunzo na kuwa na umoja na kufanya kazi kwa mstakabali wa Taifa
“Wajumbe wataandaa mpango kazi wao na kuja na majibu ya mapendekezo juu ya kiwango cha kima cha chini cha mshahara kwa Wafanyakazi”
Alimuhakikishia Waziri Ndalichako kuwa, Timu hiyo ambayo ameiteua itatekeleza majukumu yake kwa ufasaha na Uzinduzi huo utaambatana na mafunzo kwa Wajumbe hao


Aidha, Akitoa neno la Shukrani Mwenyekiti wa Bodi ya kima cha chini cha mshahara kwa Sekta Binafsi Bw. Suleiman Ahmed Rashid aliahidi kuwa watafanya kazi kwa umoja na kutekeleza kwa mjibu wa Sheria ili kufikia lengo na kwa manufaa ya Taifa.
“Wajumbe hapa wana Elimu mbalimbali, sina wasiwasi na tutajitahidi kushirikiana na Wizara yako, nina uhakika mapendekezo tutakayokuletea yatasaidia kuirahisishia Serikali kufanya Kazi”

Uzinduzi huo uliambatana na utoaji wa Vitendea kazi kwa Wajumbe hao

Baadhi ya Wajumbe wakifuatilia Mkutano

Waziri Ndalichako akikabidhi Vitendea Kazi kwa Viongozi na Wajumbe wa Bodi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *