Na. Regina Cheleso
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan amesema baadhi ya vifungu vilivyobadilishwa vinaendelea kusaidia chama kwa umakini Zaidi na kuwafikia wanachama moja kwa moja kwaajili ya kujenga nchi

Rais Samia aliyasema hayo leo April, 01, 2022 katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma kwenye mkutano mkuu wa chama cha mapinduzi CCM mara baada ya kumpata makamu mwenyekiti wa chama hicho Mh Abdulrahman Kinana ambaye amepita kwa kura zote 1875 za Wajumbe wote sawa na Asilimia 100

”Katika hili tumeanza kuchukua hatua makatibu wote wa mikoa na wilaya walishapitia mafunzo na mpaka sasa mpango wa huo umeendelea kukamilika na pia mafunzo kwa ajili ya wanachama na viongozi wamendelea kupata mafunzo”

Rais Samia alisema kwa kushirikiana na nchi za nje wamefungua Chuo chenye hadhi ya chuo kikuu kibaha na kufufua vyuo vyote vya chamakatika kila chuo ili wanachama na viongozi waende kupata mafunzo
