Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan Amefanya Mabadiliko Madogo ya Baraza la Mawaziri kwa kuwahamisha Mawaziri watatu
Mabadiliko hayo Yamefanyika leo March 31, 2022 ambapo a Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. George Simbachawene amehamishiwa Ofisi ya Waziri Mkuu kwenda kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Bunge, Sera na Uratibu ambapo Aliyekuwa Waziri katika Wizara hiyo ni Dkt. Pindi Chana
Mwingine ambaye amehamishwa ni Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dkt Damas Ndumbaro ambaye amepelekwa kwenda kuwa Waziri wa Katiba na Sheria
Awali Waziri wake alikuwa Mhe. George Simbachawene
Aidha, Mhe Rais Samia amemuhamisha Mhe. Pindi Chana ambaye Alikuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Bunge, Sera na Uratibu kwenda kuwa Waziri katika Wizara ya Maliasili na Utalii
Kabla ya mabadiliko hayo Katika Wizara ya Maliasili na Utalii Waziri wake alikuwa ni Dkt. Damas Ndumbaro




BONYEZA HAPA CHINI KUTAZAMA VIDEO