Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Imetangaza kumrejeshea Uanachama wake Bernad Membe baada ya kuomba Mara Tatu
Hayo yamesemwa leo Machi 31, 2022 na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi CCM Shaka Hamdu Shaka wakati akizungumza na Waandishi wa Habari White House Jijini Dodoma kuelezea maandalizi ya Mkutano Mkuu Maalum wa Chama cha Mapinduzi CCM
Akizungumzia kurejeshwa kwa Wanachama hao Shaka alisema kwa kukidhi matakwa ya Kikatiba Ibara ya 102(viii) kazi mojawapo ya Halmashauri Kuu ni kufuatilia mienendo na taratibu za wanachama wake
“Mtakumbuka kwamba Ndugu Bernad camillius Membe amekuwa Mwanachama wa Chama cha Mapinduzi na baadaye alifutiwa Uanachama na kuondoshwa katika chama”
Mwingine aliyerejeshewa Uanachama ni Ndugu. Abdallah Maulid Diwani wa Zanzibar ambaye aliwahi kuwa mwakilishi wa Jimbo la Jang’ombe aliyefutiwa uanachama wake Mwaka 2018
“Ninayo Furaha kubwa kuwajulisha kuwa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa leo March 31, 2022 imewasamehe na imewarudishia uanachama wao, hivyo kuanzia leo Ndugu Brenad Camillius Membe na Ndugu Abdallah Maulid Diwani ni wanachama wa Chama cha Mapinduzi na taratibu nyingine za kuwapatia kadi za uanachama zitafanyika katika maeneo yao kama ambavyo Katiba imeeleza”
Shaka alisema kuwa Membe na Diwani waliandika Barua ya Kuomba Kurejea zaidi ya Mara Tatu na kwa nyakati tofauti walikuwa wakiomba kuonana na viongozi wa Chama ili kuelezea hisia zao na utayari wao wa kurudi

