MAANDAMANO YA CCM NA WASANII YATIKISA JIJINI DODOMA

Na. Regina Cheleso

Viongozi na Wanachama wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Dodoma kwa kuambatana na Wasanii Mbalimbali Nchini wamefanya Maandamano ya Amani Kuelekea Mkutano Mkuu wa Chama hicho unaotarajiwa kufanyika Hapo April 01, 2022 Jijini Dodoma

Maandamano hayo yaliyokusanya watu kutoka Makundi mbalimbali waliojitokeza yalianzia Katika Eneo la Stendi ya Zamani hadi Viwanja vya Nyerere Square

Akizungumza Mwenyeji wa maandamano hayo ambaye ni Naibu Waziri wa Kilimo na Mbunge wa Dodoma Mjini Mhe. Antony Mavunde alimshukuru Rais wa Awamu ya Sita wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kulipatia Jimbo lake Zaidi ya Tsh. Bilioni 20 kwaajili ya Ujenzi wa Barabara za Rami

“Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan ametupa heshima kubwa sana Dodoma na inang’ara, hivi sasa bilioni Ishirini(20) tulizopewa tunajenga Barabara ya mzunguko”

Mhe. Mavunde alisema kwa kutambua hilo wao kama wana Dodoma wameona Tukio hilo iwe sehemu ya shukrani kwa Mhe. Rais na kumuunga mkono na kuahidi kuwa wapo tayari kufanya nae kazi katika muda wote

aliongeza Vijana wa Dodoma wako tayari kwa jambo lolote kwaajili ya kuisapoti Serikali ya Awamu ya Sita

Aliposimama kuhutubia Mgeni Rasmi katika maandamano hayo Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi Shaka Hamdu Shaka alisema kuwa chini ya Uongozi wa Rais Samia wataendelea kutoa Huduma Bora kwa Jamii bila kujali Itikadi za Vyama

Shaka alieleza kuwa CCM itaendelea kuendeleza Utu, Umoja na Mshikamano katika Taifa ambapo ametumia nafasi hiyo Kumshukuru Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mhe. Antony Mavunde.

Pia Mwenezi Shaka aliwashukuru Wasanii kwa kuonesha namna wanavyounga mkono na kukubali harakati za kuibadilisha Tanzania kuelekea kwenye mageuzi makubwa ya kiuchumi, kijamii na kisiasa yanayofanywa na Mhe. Rais Samia

“Mimi nataka niwaambie wasanii wote wa Tanzania kuwa ninyi mmethibitisha mmeonesha namna mnavyomuunga mkono Rais Samia na kuonesha hisia zenu.lakini nataka niwaambie uamuzi huu hamtaujutia”

Kwa upande wake Msanii wa Vichekesho Steve Mengere (Steve Nyerere) Alipozungumza kwa niaba ya wasanii aliahidi kuwa wao kama wasanii wamejipanga vyema kwaajili ya kusherehesha katika mkutano Mkuu utakaofanyika kesho April 01, 2022

“Hapa mimi Nimeongozana na baadhi ya wasanii wenzangu, nataka niwahakikishie sisi tumejipanga na tupo tayari kwaajili ya kesho”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *