BREAKING: MANGULA AJIUZULU UMAKAMU MWENYEKITI CCM, KINANA ATEULIWA

Halmashauri Kuu ya CCM Taifa imepokea Barua rasmi ya kujiuzulu kwenye nafasi ya Umakamu Mwenyekiti wa Chama hicho Mzee Phillip Mangula
Hayo yamesemwa leo Machi 31, 2022 na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi CCM Shaka Hamdu Shaka wakati akizungumza na Waandishi wa Habari White House Jijini Dodoma

Shaka alisema Mangula amemwandikia Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ambapo amewasilisha mbele ya Kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Kwaajili ya kukidhi matakwa ya kikanuni na Kikatiba
“Ndugu Phillip Japhet Mangula amefikia uamuzi huo ili kukidhi Matakwa ya Kikatiba Ibara ya 9, kifungu kidogo(e) ya Katiba ya CCM ya Mwaka 1977 Toleo la mwaka 2022, pamoja na Kanuni ya 116(e) ya kanuni ya Uchaguzi ya CCM Toleo la Mwaka 2017”

Shaka alifafanua kuwa kwa Vifungu hivyo vya Kikatiba na baada ya Halmashauri Kuu ya CCM Kupokea na kuridhia Barua hiyo, hivyo Nafasi ya Makamu Mwenyekiti imebaki wazi
“Na katika kukidhi matakwa ya kikanuni Makamu mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi atachaguliwa katika Mkutano Mkuu wa CCM Taifa, wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa baada ya kupokea Ombi hilo wamefanya uteuzi wa mwanachama wa CCM ambaye atapelekwa kwenye Mkutano Mkuu kwaajili ya Kugombea nafasi ya Makamu Mwennyekiti wa CCM, Tanzania Bara”

Alisisitiza, Hayo yamefanyika ili kukidhi matakwa ya Kikatiba Hivyo Halmashauri Kuu imemteua Ndugu, Abdulrahman Kinana ambaye ni Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM Kuwa Mgombea wa Umakamu Mwenyekiti wa chama hicho
“Uchaguzi wake utafanyika kesho(April 01 kupitia Mkutano Mkuu Maalum wa Chama cha Mapinduzi”
CCM imemshukuru Ndugu Phillip Mangulla kwa Utumishi wake uliotukuka ndani ya Chama cha Mapinduzi ambaye amefanya kazi ndani ya Chama kuanzia Mwaka 2012-2022

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *