“UCHELEWESHWAJI WA UMEME KWA TANZANIA NI AIBU”RAIS SAMIA

Na. Regina Cheleso

Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amekasirishwa na kitendo cha Tanesco kuchelewesha umeme kwa wateja
Rais Samia ameyasema hayo leo Machi 30, 2022 Ikulu ya Chamwino Jijini Dodoma alipokua anapokea ripoti ya CAG na Takukuru

alisema ucheleweshwaji wa umeme kwa wananchi wamekuwa wakiilalamikia serikali kusema Tanesco wanakula hela zao


Rais Samia alisema Tanesco haiwezi kuunganisha umeme kwa sababu bei waliyoitangaza sio sahihi na wamekaa na fedha za watu mda mlefu bila kukumilisha mladi huo wa umeme kwa wananchi
“wananchi wanalalamika kuhusu kuwacheweshea umeme na tanesco wamekaa na fedha zao Tanesco hawawezi kuunganisha umeme kwasababu bei walioitaja kwa wananchi sio sahihi kwa kuunganisha umeme.


Mh Rais Samia alieleza kuwa, watu wanatafuta hela kwenda kulipia umeme wengine wanauza kuku ili wapate umeme lakini shida ipo kwa Tanesco hawakuwatajia wananchi bei ya kweli ya umeme na kuwaomba wafanye mchakato wananchi wapate umeme
“Tanesco wafanye mchakato na wapitie kanuni na sheria zao na wahahakikishe wananchi wanapata umeme najua wamepungukiwa hela sisi kama serikali tutawasaidia ili wananchi wapate umeme,”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *