RAIS SAMIA” WAZIRI BASHUNGWA UKIWAONEA HURUMA UTALIA WEWE”

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amemuagiza Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tamisemi Innocent Bashungwa kuhakikisha anasimamia vyema mamlaka za serikali za mitaa

Rais Samia ametoa kauli hiyo leo March 30, 22 Ikulu Chamwino, Dodoma Baada ya kupokea Ripoti ya CAG na TAKUKURU

Rais alisema bado kuna upotevu mkubwa wa mapato ambapo amemtaka Waziri wa TAMISEMI, Innocent Bashungwa kuwa mkali na kutowahurumia wanaoiba fedha za Serikali.

“Waziri Bashungwa endelea kusimamia, ni kweli kuna waliofariki au ambao wamestaafu na wengine wamefukuzwa kazi lakini bado mishahara ipo, inaonesha bado wanalipwa mishahara”

Mhe. Samia alisema mwaka jana kuna Halmashauri nyingi zimeongeza mapato kutokana na usimamizi mzuri uliofanywa

“Mwaka jana nilipowatimua wakati huo Ummy ndo alikuwa Waziri, kwenye Halmashauri nyingi mapato yaliongezeka, Nimekuongezea Naibu Katibu Mkuu aende akafanye hii kazi,kuzisimamia Halmashauri,”

Alisisitiza kuwa Bashungwa anapaswa kuwa mkali na kutokuwaonea huruma wale wasiofanya kazi

“Inno (Waziri Bashungwa) usione shida kufukuza wale ambao una uhakika wameiba, msiwaonee huruma waende wakaonje maisha nje kuna Vijana wengi wanataka hizo nafasi, anayeharibu fedha za Serikali muweke pembeni akaonje maisha nje chukua mwingine aliye nje weka hapo ndani, tusileane, ukiwalea wanasema anayehofia Mtoto kulia analia yeye, sasa Inno ukiwaonea huruma utakuja kulia wewe and am serious on that”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *