RAIS SAMIA AREJESHA TOZO YA SHILINGI 100 ILIYOONDOLEWA KWENYE MAFUTA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameagiza tozo ya TZS 100 iliyokuwa imetolewa kwenye mafuta irejeshwe kwa sababu hesabu zake tayari zilikuwa zimepigiwa kwenye bajeti.

Rais Samia ameyasema hayo wakati akipokea Ripoti za Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na TAKUKURU, Ikulu ya Chamwino Dodoma ambapo amesema kwa mwenendo wa upandaji wa bei ya mafuta duniani, kuondoa TZS 100 hakutasaidia, ila kutainyima serikali mapato.

Alisema kuwa mafuta yameendelea kupanda licha ya kushusha Bei kwa Wananchi na kusema Waziri hakuangalia kwa upana zaidi

“Ile shilingi iliyotoka nimeagiza irudishwe, kulikuwa kuna utata kidogo tumekaa kama serikali tukarekebisha”

Aliongeza kuwa Wananchi waeleweshwe ili kuacha kulalamika juu ya kupanda kwa Bei za Mafuta na kusema Serikali haisemi kitu

“lakini jingine kwenye mafuta ya kula, Nakumbuka nilikuagiza Waziri wa Fedha kwamba katika bajeti yetu tuliingiza kitu kwenye mafuta ya Kula ili kulinda Viwanda vyetu vya ndani kwenye uzalishaji”

Mhe. Samia alisema pamoja na kuzuia Viwanda vya nje visiingize mafuta lakini imepeleka Viwanda vya ndani kufungwa kwa kukosa uzalishaji

Amemuagiza Waziri kwenda kulitazama upya na kuliondoa kama halina msaada

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *