TETESI ZA SOKA ULAYA LEO JUMANNE MARCH 29, 2022

Mohamed Salah

Jaribio la Barcelona la kutaka kumsajili mshambuliaji wa Liverpool na Misri Mohamed Salah, 29, linatarajiwa kugonga mwamba kwa sababu ya kubanwa na sheria za kifedha za La Liga. (Mirror)

Liverpool itakabiliwa na ushindani kutoka kwa Real Madrid katika mbio za kumsaka kiungo wa kati wa Borussia Dortmund Jude Bellingham, 18. (Bild – subscription required)

Jude Bellingham

Leeds United wamemuwekea dau la £67m (£80m) winga wake wa Brazil Raphinha, 25, huku Barcelona ikiwa tayari kulipa nusu ya kiwango hicho (Mirror)

Leeds inasisitiza kifungu pekee katika mkataba wa Raphinha kinachomruhusu kuondoka ni kile kinachosema aaondoka kama Leeds watashushwa daraja kutoka Ligi Kuu ya England.(The Athletic)MATANGAZOhttps://0f15be04af01b343ebe8eb6c07575330.safeframe.googlesyndication.com/safeframe/1-0-38/html/container.html

Raphinha

Manchester United, Liverpool na Newcastle zinataka kumsajili kiungo wa kati wa Ureno Otavio, 27, kutoka Porto mwishoni mwa msimu. (A Bola – in Portuguese)

Arsenal na Atletico Madrid zinaiwania saini ya mshambuliaji wa Argentina Lautaro Martinez, 24, ambaye Inter Milan itamuuza iwapo itapata ofa ya £58m mwishoni mwa msimu. (Calciomercato – in Italian)

Lautaro Martinez

Liverpool wamefikia makubaliano ya kumsajili mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya England ya chini ya miaka 18 Fabio Carvalho kutoka Fulham, baada ya kukaribia kabisa kumsajili kiungo huyo wa kati, mwenye miaka 19, wakati wa dirisha la uhamisho la mwezi Januari. (Football Insider)

Arsenal wanaandaa ofa ya kwanza ya kumuongeza mkataba wa winga wa England Bukayo Saka, 20, mwisho wa msimu huu. (Fabrizio Romano)

Mshambuliaji Paulo Dybala anataka kujiunga na Atletico Madrid mwishoni mwa msimu huu wakati mkataba wake na Juventus utakapomalizika – na ingawa Inter Milan pia wanataka kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28, wanaweza kufanya hivyo iwapo watamuuza raia mwenzake wa Argentina, Martinez. (Mundo Deportivo – in Spanish)

Paulo Dybala

Ivory Coast winger Nicolas Pepe, 26, has hinted at a summer exit from Arsenal, three years after his club-record £72m move from Lille.

Winga wa Ivory Coast Nicolas Pepe, mwenye umri wa miaka 26, amedokeza kuhusu uwezekano wa kuondoka Arsenal mwishoni mwa msimu, miaka mitatu baada ya kutua kwa uhamisho wake uliowekwa rekodi ya klabu wa £72m. (Sun)

Leicester City imekuwa ikihusishwa na mshambuliaji wa Club Bruges, Charles de Ketelaere. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 amepachika mabao 17 katika mechi 41 msimu huu na kucheza mechi yake ya tano na timu ya taifa ya Ubelgiji katika mchezo wa kirafiki mwishoni mwa wiki iliyopita dhidi ya Jamhuri ya Ireland. (Leicester Mercury)

Kiungo wa kati wa Marekani Brenden Aaronson, 21, bado anataka kuondoka Red Bull Salzburg msimu huu na mazungumzo yanaendelea kuhusu uhamisho wake kuelekea Leeds. (Sky Sport Germany)

Aaronson

Newcastle United inamtaka winga wa Watford Ismaila Sarr, 24, huku Liverpool pia ikimfuatilia mchezaji huyo wa kimataifa wa Senegal. (The Sun)

Wolves, Tottenham na Everton zimeonysha nia ya kumtaka kocha wa Rennes Mfaransa Bruno Genesio, 55. (RMC Sport – in French)

Manchester United wako tayari kuanza mazungumzo ya mkataba mpya na mshambuliaji wake wa England Marcus Rashford, 24, na beki wa kushoto wa England Luke Shaw, 26. (ESPN)

Marcus Rashford

Lakini United hawana mpngo wa kumuongeze mkataba mpya kiungo wa England Jesse Lingard, 29, Mshambuliaji wa Uruguay Edinson Cavani, 35, na kiungo wa zamani wa Hispania Juan Mata, 33. (Fabrizio Romano)

Napoli wana matumaini ya kuzuia usajili wa beki wa kati wa Senegal Kalidou Koulibaly asiondoke bure kwa kumpa mkataba mrefu nyota huyo mwenye miaka 30. (Calciomercato – in Italian)

credit to https://www.bbc.com/swahili

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *