KAMANDA AONYA UZEMBE WA ASKARI BAADA YA WATU 6 KUFARIKI KWA AJALI

kufuatia Ajali iliyosababisha Vifo vya Watu sita na wengine kadhaa kujeruhiwa baada ya gari aina ya fuso yenye namba za usajili T 239 AFD walilokua wakisafiria kuacha njia na kutumbukia kwenye korongo katika barabara ya Soni – Mombo wilayani Lushoto mkoani Tanga.

Uhondo Tv imefanya mazungumzo kwa njia ya Simu na Kamanda wa polisi wa mkoa wa Tanga, Safia Jongo ambaye amesema ajali hiyo imetokea leo asubuhi.

Kamanda Jongo aliwataka watumiaji wa vyombo vya moto mkoani Tanga kuendelea kufuata sheria za usalama barabarani ili kuepuka ajali zinazoweza kuepukika.
Alitoa Rai kwa Wananchi kutoa Taarifa kwa Jeshi la Polisi pale wanapoona mwenendo mbovu wa watumiaji wa vyombo vya usafiri

Alisema Madereva waache kuendesha Vyombo kwa mazoea na kuwa makini wawapo Barabarani

“Wafuate sheria za usalama Barabarani, licha kuwakamata lakini bado Ajali zinaendelea kutokea,”

Aliwaonya Askari ambao hawafuati maadili na kuchukua rushwa kwa madereva huku akisema kuwa huo ni uzembe na chanzo cha kuendelea kusababisha Ajali Barabarani

Miili ya watu waliofariki dunia katika ajali hiyo imehifadhiwa katika hospitali ya wilaya ya Lushoto na majeruhi wanaendelea kupatiwa matibabu hospitalini hapo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *