HOSPITAL YA BENJAMIN MKAPA KUPANDIKIZA ULOTO JUNI, 2022

Hospitali ya Benjamin Mkapa iko katika hatua za mwisho za maandalizi ya kutoa huduma za kupandikiza Uloto kwa wagonjwa wa Selimundu na watu wote wenye matatizo yanayohitaji huduma hiyo kuanzia Juni mwaka huu.


Hayo yamebanishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali hiyo Dkt. Alphonce Chandika muda mfupi baada ya jopo la wataamu kutoka Itali kufanya ukaguzi wa maboresho ya wodi za kutole huduma hiyo.
“Mwezi wa sita tutaanza kutoa huduma za kupandikiza Uloto kwa wagonjwa wenye selimundu, wataalamu kutoka Itali wameona na kuridhishwa na utayari wetu, baadaye tutatathimini mapungufu madogomadogo tuyakamilishe huduma zianze” alisema Dkt. Chandika.


Awali Dkt. Coronelio Odezo, kutoka Italia alisema wameona vyumba vyenye usalama wa kiwango cha juu cha kuwezesha kulinda wagonjwa watakaopatiwa huduma ya upandikizaji wa Uloto.
“Tofautii na miaka miwili nyuma tumekuta mabadiliko makubwa, katika eneo la vitanda kumi linaloandaliwa kutolea huduma hizo, nimeona vyumba salama, nchini kwetu tumetoa huduma hizi kwa mafanikio makubwa, kwa maboresho haya tuamini wagonjwa watakuwa salama” Alisema Dkt. Coronelio Odezo.
Kwa muda wa miaka miwili hospitali ya Benjamin Mkapa imekuwa katika maandalizi ya kutoa huduma za kupandikiza Uloto kwa wagonjwa wenye Selimundu ikiwa na matarajio ya kutoa huduma hizo rasmi Juni, 2022.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *