Tetesi za soka Ulaya

Arsenal wanatayarisha ofa kwa mshambuliaji wa Manchester United Muingereza Marcus Rashford, 24. (Mirror)

Ligi ya Premia imezuia jaribio la Burnley kutaka kumsajili winga wa Nigeria Victor Moses, 31, kutoka klabu ya Urusi ya Spartak Moscow. (Sky Sports)

Kiungo wa kati wa Leicester City na Ubelgiji Youri Tielemans, 24, anasema anataka kucheza soka ya Ligi ya Mabingwa. (Mirror)

Manchester United na Arsenal zote zimehusishwa kutaka kumnunua Tielemans, ambaye anaweza kuruhusiwa kuondoka Leicester kwa kitita cha pauni milioni35 mwisho wa msimu huu.(Metro)

Southampton na Crystal Palace wana nia ya kumsajili kiungo wa kati wa Uingereza Harry Winks, 26, kutoka Tottenham.(Star)

m

Mshambuliaji wa Argentina Paulo Dybala anaweza kuhama kutoka Juventus kwenda kwa wapinzani wa Serie A Inter Milan, huku Inter wakimpanga mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 kama mbadala wa Muargentina mwenzake Lautaro Martinez, 24.(Mail)

m

Mshambuliaji wa Borussia Dortmund ya Norway Erling Braut Haaland atahamia Manchester City au Real Madrid msimu huu, lakini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 amekataa ofa ya kwanza kubwa ya City.(AS-in Spanish)

Napoli wangetaka euro milioni100 (pauni milioni 83) kwa mshambuliaji wa Nigeria Victor Osimhen, 23, ambaye amepokea nia kutoka kwa klabu kadhaa zikiwemo Arsenal, Liverpool, Manchester United, Newcastle na Tottenham.(Fichajes-in Spanish)

Paris St-Germain wanafuatilia maendeleo ya winga wa Leeds United wa Brazil Raphinha, 25. (Mail)

m

PSG wamemfanya kiungo wa kati wa Manchester United na Ufaransa Paul Pogba, 29, kuwa shabaha yao kuu ya uhamisho. (Fabrice Hawkins,via Express)

Klabu ya PSG ya Ligue 1 pia inaweza kumsajili mshambuliaji wa Chelsea na Ubelgiji Romelu Lukaku, 28, msimu wa joto. (Football Insider)

m

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *