Bodi ya nidhamu ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) imetangaza rasmi kumfungia miezi 12 Afisa wa Club ya RS Berkane ya Morocco Majdi Madrane kwa kosa la kuvamia uwanjani wakati wa mchezo wa Kombe la Shirikisho wa Simba SC dhidi ya Berkane uliyochezwa Benjamin Mkapa na Simba SC kushinda 1-0.
Majdi alivamia uwanjani wakati wa mchezo na kushinikiza wachezaji wake kugoma mara baada ya muamuzi msaidizi kukataa goli lao kuwa off side, CAF pia imeipiga faini Club hiyo ya USD 100,000 (Tsh milioni 232) kwa kosa la Wachezaji wake kumzonga na kumbugudhi Mwamuzi wakati wa mchezo.
Katika Hatua nyingine, michezo ya Mwisho ya Hatua ya Makundi Kombe la Shirikisho Barani Afrika inatarajiwa kufika ukingoni mwishoni mwa wiki hii
Rs Berkane wapo nafasi ya Pili katika kundi D wakiwa na Alama 7, Huku nafasi ya Tatu ikishikiliwa na Simba wenye alama 7 pia
Us Gendamarien wanaburuza Mkia wakiwa na alama 5 pekee huku Asec Mimosas wakikamata nafasi ya kwanza kwa Alama 9 kibindoni.

