AJALI YAMUUA PROF NGOWI

Mwananzuoni mbobezi wa masuala ya uchumi na mhadhiri mwandamizi wa Chuo Kikuu Cha Mzumbe, Prof Honest Ngowi amefariki dunia leo Machi 28, 2022 baada ya gari lao kuangikiwa na kontena eneo la Mlandizi akiwa njiani kuelekea Morogoro.

Katika ajali hiyo, Prof Ngowi alikuwa na dereva wake ambaye naye amefariki dunia.

Kwa mujibu wa RPC Mkoa wa Pwani, Pius Lutumo Prof Ngowi amefia katika Hospitali ya Tumbi na dereva alifariki eneo la ajali.

BOFYA HAPA CHINI KUTAZAMA VIDEO

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *