Na Emmanuel Charles
Kuelekea Mechi ya Mwisho wa Hatua ya Makundi ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika Kati ya Simba Sc na Us Gendamarien Klabu ya Simba yatamba kuibuka na ushindi
Ikiwa zimesalia Siku chache kabla ya kupigwa kwa mchezo huo Siku ya Jumapili April 03, 2022 katika uwanja wa Taifa wa Mkapa Jijini Dar es salaam, Kikosi cha Wekundu wa Msimbazi kimeeleza maandalizi kupitia kwa Meneja Mawasiliano Ahmed Ally
Akizungumza leo mbele ya Waandishi wa Habari, Meneja huyo alisema wataingia kwenye mchezo huo wakiwa na lengo la kupata ushindi

“Tutaingia kwenye mchezo wa jumapili tukiwa na lengo moja tu, USHINDI. Tutaingia kwa nguvu moja, kwa ari ya juu na lengo ni moja tu ushindi. Niseme kwa nia ambayo tuko nayo robo fainali hii hapa.”
Ahmed Ally alisema walishajifunza kutokana na Makosa yaliyopita, hivyo wanaenda kuwakabili USGN FC Wakiwa wanawaheshimu na kutokurudia Makosa yaliyopita
“Mambo ya bonus yapo sawa. Huwa inatokea muda mwingine boss [@moodewji] anawaongezea lakini hata kabla ya ya mechi wachezaji wanajua kabisa kuwa bonus itakuwepo.”
Aliendelea kutamba kwa kusema kuwa Simba haitakuwa na Presha ya Mchezo kwa Kocha maana ni Kocha Mkubwa( Pablo Franco) na Wanajua ana uwezo wa kuivusha Timu salama na hawana mashaka.
“Mpaka jana wanaingia kambini tulikuwa na majeruhi mmoja tu, Hassan Dilunga. Sadio Knaoute ambaye alikosekana kwenye mchezo uliopita jana alianza mazoezi.”
Alizungumzia kuhusu Idadi ya Mashabiki alisema wameruhusiwa Mashabiki 35,000.Awali waliomba kuongeza idadi ya Mashabiki kupitia kwa TFF Lakini kwa Sababu ya mambo ya covid wameruhusu idadi hiyo na mashabiki wanunue tiketi mapema

“Wapinzani wetu USGN watawasili nchini alfajiri ya siku ya Alhamisi. Tumetoa taarifa hiyo kwa kujua wana wenyeji wao hapa nchini ili wakawapokee wageni wao.”
Kwa Upande mwingine aliwashukuru TFF kwa kuwaruhusu wachezaji waliokuwa Timu ya Taifa kurejea kambini kujiandaa na Mchezo huo

“Kambi ilianza jana na mazoezi yalianza jana. Mwalimu amefurahi namna wachezaji wameanza mazoezi. Wachezaji wana morali ya hali ya juu na mwalimu anaamini watakuwa na mwendelezo huo kwenye mchezo wetu wa Aprili 3. Safari hii nyimbo zetu zitapigwa kupitia spika za uwanja na watu wataitikia kwa pamoja, na tayari zimesharekodiwa kwenye mfumo rasmi.”
Katika Mchezo huo Simba inaingia ikiwa inahitaji kupata ushindi ili kujihakikishia kusonga mbele kuelekea katika hatua inayofuata
Picha hapo chini ni Msimamo ulivyo Katika Kundi D ambalo lina Timu za Simba Sc, Rs Berkane, Us Gendamarien, Asec Mimosas
