WANA YANGA PUUZENI

Anaandika Haji Manara, Msemaji wa Yanga

Wananchi wenzangu, interest yetu iwe kushinda Championship msimu huu, iwe kushinda FA na iwe kukamilisha Transformation yetu, mengine ni ya kupuuza.

Nipo hapa kushirikiana na nyinyi kushinda Mataji, sipo hapa kujibizana na mtu, tuendelee kuwasamehe wanaotaka vurugu na malumbano coz bila kumtaja Haji kwa ubaya atamtaja nani?

Umoja wetu ndio nguvu tuliyonayo kwa sasa, tusijitoe relini kisa choyo, chuki na roho mbaya, tuwekeni maslahi mapana ya hii Taasisi.

Once again nawashukuru Wanayanga, mmenirudishia umri wangu nyuma, hamjawahi kuniacha toka nilipokuja Club hii kubwa, mwenzenu nimejaaliwa Moyo mgumu wa kustahmili kashfa na karaha na hiyo inanipa ujasiri mkubwa katika kazi zangu.

Chonde Chonde tujiangalie nini tunataka kwa sasa na porojo zote ntawajibia end of May Insha’Allah 🙏🏻🙏🏻🙏🏻

SUBIRA NDUGU ZANGU.

cc, https://www.instagram.com/hajismanara/

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *