TETESI ZA SOKA ULAYA, MARCH 26, 2022

Meneja wa Barcelona Xavi anamtaka mshambuliaji wa Liverpool na Misri Mohamed Salah, 29, pale Nou Camp wakati magwiji hao wa Catalan wakionekana kumkosa Erling Braut Haaland ambaye ndio chaguo lao kubwa. (Mundo Deportivo, in Spanish)

Rais wa Barcelona Joan Laporta anasema hataiweka klabu hiyo kwenye hatari na mgogoro wa kifedha kwa kumsajili mshambuliaji huyo wa Norway Haaland, 21 kutoka Borussia Dortmund. (Fabrizio Romano, via Mundo Deportivo)

th

Leeds imeripotiwa kukataa ofa ya £29m kutoka Barcelona kwa ajili ya winga wa Brazil Raphinha, 25, ambaye kipengele cha mkataba wake kinamruhusu kuuzwa kwa £60m. (Sport, in Spanish)

Winga wa Wolves na Ureno Pedro Neto yuko kwenye orodha ya wachezaji wanaowaniwa na Paris St-Germain wakati huu nyota huyo mwenye miaka 22 akirejea kutoka majeruhi ya muda mrefu. (Mail)

Newcastle inajiandaa kuipiku AC Milan katika mbio za kumsajili mlinzi wa kati mholanzi Sven Botman, 22 kutoka Lille, baada ya kushindwa kumsajili mwezi Januari. (The Times, subscription required)

th

The Magpies wanatazamiwa pia kuongeza nguvu kwenye safu yake ya ushambuliaji kwa kumsajili mshambuliaji wa Benfica na Uruguay Darwin Nunez, 22, licha ya Arsenal pia kumtaka. (The Athletic, subscription required)

Manchester United wanamtaka mlinzi wa Switzerland Manuel Akanji, 26, ambaye amekataa kusaini mkataba mpya pale Borussia Dortmund na amewekewa thamani ya £25m na klabu hiyo ya Bundesliga. (Mirror)

Liverpool, Manchester City na Manchester United zinapambana kumsajili mshambuliaji kinda wa Rangers raia wa Scotlanda Rory Wilson. (Star)

Arsenal na Tottenham zinamtaka kiungo mfaransa Lesley Ugochukwu, 18, kutoka Rennes ya Ligue 1 ya Ufaransa. (l’Equipe, in French)

th

Kiungo wa Arsenal na Switzerland Granit Xhaka, 29, anatakiwa bado na meneja wa Roma Jose Mourinho. (Gazzetta dello Sport, in Italian)

West Ham watamsajili nyota waliokua wakimuwania kwa muda mrefu Nikola Milenkovic, 24, huku ripoti zikisema mlinzi huyo wa Fiorentina na Serbia ameingia makubaliano ya awali na wapiga nyundo hao wa London. (TeamTalk)

Ismaila Sarr anaweza kuondoka Watford kujiunga na Liverpool katika majira ya kiangazi. Wakati wekundu hao wakionyesha nia ya kumtaka winga huyo wa Senegal mwenye miaka 24 lakini wanakabiliwa na upinzani kutoka kwa AC Milan. (ECorriere dello Sport)

Tottenham wanamtaka mlinzi wa Ufaransa Boubacar Kamara, 22, ambaye mkataba wake na Marseille unamalizika mwishoni mwa msimu. (Football London)

th

Mshambuliaji wa Real Madrid Eden Hazard atafanyiwa upasuaji wiki hii, utakaomfanya akae nje kwa kipindi cha mwezi mmoja na kufanya zoezi la mbelgiji huyo mwenye miaka 31 kurejea Chelsea kuingia kwenye utata. (Marca)

Mlinzi wa Charlton Lucas Ness, 22, anafuatiliwa na vilabu kadhaa vikiwemo Norwich, Burnley, Coventry City na Plymouth Argyle. (Football League World)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *