YANGA:SISI BADO TUPO,KUSHUKA BADO SANA

UONGOZI wa Yanga umeweka wazi kwamba bado upo nafasi ya kwanza na kwa wale ambao wanafikiria kwamba watapoteza kwenye mechi za hivi karibuni hilo walisahau.

Ikiwa imecheza mechi 17 kibindoni imekusanya pointi 45 haijapoteza mchezo hata mmoja zaidi ya kuambulia sare kwenye mechi tatu pekee na moja kati ya sare hizo ni ile iliyopata mbele ya Simba.

 Ofisa Habari wa Yanga,Hassan Bumbuli alisema kuwa bado wapo nafasi ya kwanza jambo ambalo litawafanya wadumu hapo mpaka ligi itakapokamilika.

“Sisi tupo nafasi ya kwanza na tunazidi kupambana kwa ajili ya mechi zijazo kikubwa ni kuona kwamba tunaendelea pale ambapo tuliishia mzunguko wa kwanza na hilo linawezekana.

“Malengo yetu ni kuona kwamba tunatwaa ubingwa lakini sio kazi nyepesi kwa kuwa kila timu inapambana kuona kwamba inashinda mechi zake hasa inapokutana na sisi ila hilo la ufundi linafanyiwa kazi na benchi la ufundi,” amesema.

Kinara wa utupiaji ni Fiston Mayele akiwa ametupia mabao 10 kibindoni na pasi zake ni tatu.

Chanzo:Spoti Xtra

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *