
Ni kawaida kwa watu kuchukua hatua ngumu katika maisha yao, kwa mfano kufuta akaunti zao za mitandao ya kijamii n.k.
Katika makala hii nitakufundisha jinsi gani ya kufuta akaunti yako ya mtandao wako pendwa wa Instagram kwa njia rahisi kabisa.
Jinsi ya kufuta akaunti ya Instagram moja kwa moja
Fuata hatua hizi zifuatazo ili uweze kukamilisha zoezi hili :
1. Fungua instagram kwenye PC au simu kwa kutumia browser. Huwezi kufuta kwa kupitia App ya Instagram
2. Ingia kwenye akaunti yako (log in)
3.Bofya kwenye kiungo hiki =>https://www.instagram.com/accounts/remove/request/permanent/
4. Chagua machaguo kwenye “drop menu” ya kwanini unataka kufuta akaunti yako …….
5. Bofya kwenye ” PERMANENTLY DELETE MY ACCOUNT “
Baada ya hapo utakuwa tayari ushakamilisha zoezi la kufuta akaunti yako ya Instagram moja kwa moja, Pia usisahau kutu-follow kwenye page zetu za Instagram, Facebook na twitter kwa jina la @ngonzitech_